Kuepuka mzigo wa madeni ya kijinga Tanesco itangaze imefilisika

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
Dowans kuifilisi Tanesco


picture-11.jpg

Na Jabir Idrissa - Imechapwa 15 December 2010

tanesco_219.jpgSHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) liko hoi kiuchumi na halikopesheki, MwanaHALISI imeelezwa.
Akizungumza katika mkutano wa 41 wa Baraza la Wafanyakazi wa Tanesco mjini Morogoro wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo alisema shirika lina hali "mbaya sana" kifedha.
Taarifa kutoka ndani ya shirika zinasema hali hiyo inayoendelea kwa muda mrefu sasa, inatokana na Tanesco kukabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni huku gharama za uendeshaji zikiongezeka kwa kasi.
Kwa sasa, mapato ya mwezi ya Tanesco hayazidi Sh. 30 bilioni.

Wakati linakusanya mapato hayo, lenyewe linatumia kiasi cha Sh. 566 milioni kila siku kulipa makampuni ya kufua umeme ya Songas na IPTL. Fedha hizo hulipwa kama gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge.

Jairo aliwaambia wafanyakazi wa Tanesco kwamba utekelezaji wa mkakati wa kupunguza matumizi yake lazima uanze huku shirika likifuatilia madeni inayodai wateja wake.

Alisema, "nilichokisema ni kwamba lazima wajitahidi kuliweka Shirika katika hali ya kukopesheka zaidi."
Habari hizo zinaibuka wiki tatu tangu kufichuka kwa taarifa kuwa Tanesco imeshindwa katika shauri lililofunguliwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi na kampuni ya Dowans Tanzania Limited.

Katika uamuzi wake, mahakama hiyo imeamuru Tanesco kuilipa Dowans Sh. 185 bilioni kutokana na kosa la kuvunja mkataba.

Mkataba wenyewe ni ule wa kufua umeme wa dharura ambao Dowans iliurithi kutoka kwa kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company (RDC). Ulisainiwa mwaka 2006.

Kwa msingi huo, hata kama Tanesco itaamua kutumia mapato yake yote hayo, bado itachukua zaidi ya miezi sita kumaliza kuilipa Dowans.

Aidha, taarifa hizo zinakuja wakati Tanesco ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa umeme hivyo kulazimika kuendelea kuitegemea mitambo ya kukodi ili kuongeza umeme katika Gridi ya Taifa.

Kwa mfano, wakati mahitaji ya umeme kwa wateja wake ni Megawati (MW) 906, shirika lina uwezo wa kuzalisha megawati 705 tu.

Megawati hizo zinazalishwa kupitia mabwawa ya Kidatu (MW 204), Kihansi (MW 180), Mtera (MW 80), Pangani (MW 68), Hale (MW 21) na Nyumba ya Mungu (MW 8).

Umeme mwingine unapatika kwa nguvu za mitambo iliyopo katika vituo vya Tanesco vya Ubungo (MW 100) na Tegeta (MW 45).

Wakati uzalishaji wa umeme ukiwa megawati 705, mahitaji katika mkoa wa Dar es Salaam pekee, ni MW 455.

"Kimsingi, Tanesco inakabiliwa na hali mbaya sana kifedha na miundombinu. Uzalishaji hauendani na mahitaji. Naona hata hicho wanasiasa wanachokiita ‘kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha', ni kiini macho," amesema kiongozi mmoja wa Tanesco aliyekataa kutajwa.

Kadhalika, Tanesco inakadiriwa kuwa na malimbikizo ya madeni yanayofikia Sh. 700 bilioni.
Katika kukabiliana na ukata, tayari uongozi umewasilisha mapendekezo Mamlaka ya Usimamizi wa huduma za maji na nishati (EWURA), maombi ya kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 34.6 kuanzia 1 Januari 2011.

Tanesco wanataka ongezeko jingine la bei la asilimia 13.8 litolewe kwa mwaka 2012 na ongezeko la tatu la asilimia 13.9 litolewe kwa mwaka 2013.

Kwa hali hiyo, bei inayopendekezwa EWURA kuanzia mwakani kwa wateja wadogo wanaotumia nishati hiyo chini ya kWh 40 kwa mwezi, ni Sh. 2,692 kutoka Sh. 2,000.

Hiyo maana yake ni watumiaji wa umeme nchini kulazimika kulipa kiasi cha Sh. 692 zaidi kwa kila Kwh kulinganisha na bei ya zamani.

Gazeti hili limeelezwa pia kwamba kutakuwa na ongezeko la gharama kwa wateja watakaotaka kuwekewa mita za LUKU au kuunganishiwa umeme majumbani.

Taarifa zimesema mapendekezo ya bei mpya yaliyowasilishwa EWURA Agosti mwaka huu, yanasubiri uamuzi wa Bodi ya EWURA.

Bodi hiyo inatarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa kupitisha maombi hayo.
Gazeti toleo na. 219
Chanzo: Mwanahalisi


Nimesoma hiyo habari hapo juu. Ninadhani kuwa njia pekee ya kuinusuru Tanesco na madeni yake sugu na ya kifisadi ni kutangaza kuwa imefilisika. Kutangazwa kwake kuwa kumefilisika kutaiwezesha kuondokana na sehemu kubwa ya madeni na hivyo kujipanga upya. Nawaomba ndugu zangu tulivalie njuga suala hili ili kulinusuru taifa letu kwani kila uchao madeni yanazidi kuongezeka wakati uwezo wa kulipa haupo. Sisi kama Watanzania hatuwezi kufuga ujinga kama huu. Sheria za Kufilisika ziko wazi na mtu anapokuwa amefilisika huzitumia ili kuweza kujiondoa katika mzigo wa madeni.

Huku Marekani kampuni kama GM, Chrysler na nyinginezo nyingi walitumia sheria za kufilisika kuweza kufuta sehemu kubwa ya madeni yao. Nasi Tanzania tunazo sheria kama hizo ni lazima tuzitumie na tusibakie kusema kuwa hatuna ujanja wa kuondokana na deni la Dowans. Kwani kutangazwa kwa Tanesco kuwa imefilisika, ambao ndio ukweli mweupe, kutaifanya si tu iondokane na mikataba yote ya shanga na ya kifisadi iliyosaini na kampuni za IPTL, Dowans na Songas bali pia na wale wote ambao wanaidai madeni hewa na ya kifisadi.
 

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
5,355
6,379
Hilo ni jambo zuri lakini ni lazima tuelewe mkataba maana wakati mwingine mikataba inakuwa inahusisha serikali pale ambapo Tanesco haiwezi kulipa. Hii ndiyo ubaya wa kuwa na kampuni za serikali!. Je Tanesco ni kampuni binafsi au??
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,531
5,357
That was my sentiment too. Lakini these fisadis will try to hold the government/treasury at ransom. Mbona Vallambia hajalipwa na hivi sasa ni zaidi ya miaka 20? Tungekuwa na serikali makini tngeweza kuwachenga hawa matapeli, lakini hao hao ndio waliomweka Kikwete Magogoni. They will have their pound of flesh.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
That is one option we would consider to save our DEAR Taxes from flowing into evil hands with a view to be USED IN STEALING FUTURE ELECTIONS in our country at our bitter undoing.

Many thanks for your PAINFUL CARE to think of a possible way out!! Huu ni msiba wa Taifa na hasa kwetu sisi walipakodi ambao wengi wetu wala hatujui utamu wa huduma za shirika hili la TANESCO.
 

Wameiba Kura

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
390
3
Hivi who said Dowans watalipwa? hawatakiwi kulipwa ni matapeli na sisi hatuitambui ICC ni mafisadi court, na file AG still analo, watanzania we are very keen kwa hili huu ni UWIZI MKUBWA, tutaandamana hadi kwa huyu dowans tumkamate au atoroke nchini, kwanza hana uchungu na nchi yetu,
hafai kuishi nchi yetu, najua rais kakaa kimya, tunasubiri watoe tamko, CDM na wananchi wote ni mayoweeeeee na mitaani hatukubali & is what we are waiting, huu uwizi hatukubali
 

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
Hilo ni jambo zuri lakini ni lazima tuelewe mkataba maana wakati mwingine mikataba inakuwa inahusisha serikali pale ambapo Tanesco haiwezi kulipa. Hii ndiyo ubaya wa kuwa na kampuni za serikali!. Je Tanesco ni kampuni binafsi au??

Tanesco ni shirika la umma kwa misingi ya kwamba serikali inamiliki hisa zote lakini ni kampuni ambayo inatakiwa iendeshwe kibiashara kwani imesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya makampuni ya mwaka 2002 hivyo ina kinga na haki zote ambazo kampuni nyingine nchini zinazo ikiwa ni pamoja na kutangazwa kuwa imefilisika. Ninasisitiza kuwa kutangazwa kama imefilisika kama kutafanywa kutokana na kuendeshwa kwake kihasara na kushindwa kulipa madeni yake kutaiwezesha Tanesco kuondokana na madeni hayo na hivyo kuundwa upya na kufanya kazi bila mzigo wa madeni.

Ubaya ni kwamba viongozi wa serikali hawataki kufanya uamuzi muafaka ambao unazingatia sheria. Mfano, mkataba wa serikali na IPTL unasema wazi kuwa wabia wa IPTL wanapokuwa katika ugomvi serikali ina haki ya kuvunja mkataba. VIP-Engineering ina ugomvi na wabia wenzake wa Malaysia katika IPTL licha ya serikali kuelezwa haki zake katika mkataba huo imekataa kufanya hivyo. Kwa sababu gani? Wakubwa ambao walisaini mkataba huo na ambao wananufaika nao wamehakikisha kuwa hilo halifanyiki. Hoja hii haifuti ile kauli yangu kuwa mkataba huo unakiuka Katiba ya Nchi kwani hakuridhiwa na Bunge. Lakini hata zile haki ambazo ziko katika mkataba huo hewa hatuzitumi na badala yake tunalipa mabilioni ya pesa ili kuwanufaisha mafisadi. Aibu mbona aibu!
 

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,804
276
Mnajua sheria za MUFILISI kwa kampuni? Hapo usiguse, mtalia watanzania. Yaan WADAI itabidi wagawane mali za Tanesco... Si wameshndwa kulipa madeni. Dawa hapa ni KURUHUSU MAKAMPUNI BINAFSI KUZALISHA NA KUUZA UMEME. EWURA ibaki kuwa chombo cha ku-regulate prices. Electricity is no lönger public good, lets transform to private and commercial bases.
 

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,518
1,336
Wasiwasi wangu ni kuwa ili fuifilisi iitabidi kufuata sheria ya makampuni kwani Tanesco imeanzishwa chini ya sheria hiyo, itabidi wanahisa kuteua liquidator. Moja ya Kazi za liquidator ni kulipa madeni kwa wadeni kutokana na kipaumbele cha sheria na uzito wa madeni kisheria (secured and unsecured). Shareholder ni Serikali, kwa hiyo liquidator atateuliwa na serikali na huyo liquidator atafanya kazi kwa maagizo ya serikali, hasa inapofika katika kulipa madeni.

Kwa option hiyo basi usishangae kusikia dowans na richmond wanapewa mtera, kidatu, nyumba ya mungu na jumba la ubungo(HQ) ili kufidia madeni hayo, the rest is obvious

The worst option I would ever iamgine, we shouldnt attempt.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom