Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,644
- 119,245
Wanabodi,
Mafundisho yote ya dini yanafundisha kuwa "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu", kwa lengo la kuwathibitishia waumini wote wa dini zote kuwa tawala zozote zilizo madarakani kwa mujibu wa sheria, zimeweza kuingia madarakani kwa baraka na ridhaa ya Mungu, hivyo zinapaswa sio kuabudiwa (wa kuabudiwa ni Mungu pekee), bali zinapaswa kuheshimiwa, kuungwa mkono na kupewa utii wa sheria bila shuruti, taratibu na kanuni, na miongoni mwa hayo ya Kaisari, ni pamoja na suala la kulipa kodi ambapo watu wote lazima walipe kodi ili kuiwezesha serikali kuendesha nchi!. Hivyo vitendo vyovyote vya ukwepaji kodi wa aina yoyote sio tuu ni ukiukwaji wa sheria, bali pia ni dhambi mbele ya Mwenyeezi Mungu!.
Kwa muktadha huo, mimi naiunga mkono bajeti ya Rais Magufuli, kufuta misamaha yote ya kodi, kwa kuwalazimisha wale wote wenye misamaha ya kodi, walipe kwanza kodi, ndipo waombe misamaha, ikithibitika wanastahili misamaha hiyo, ndipo warejeshewe hizo kodi walizolipa!. Hii itaondoa matumizi mabaya ya misamaha ya kodi, kwa wale wakwepaji kodi waliokuwa wakiitumia misamaha mbalimbali kama chaka la kujifichia na kukwepa kodi!.
Naunga mkono kila senti tano itolewayo na serikali kama mapato kwa mtu yoyote lazima ilikatwe kodi, ikiwemo mafao ya wabunge na fedha yoyote inayolipwa kwa yoyote kama mapato, lazima ikatwe kodi, na kukatwa kodi huku kwa mafao kusiishie tuu kwenye mafao ya wabunge, bali kodi ikatwe kwenye mafao yote yatakanayo na fedha za umma yakiwemo mafao ya viongozi wakuu!. No double standards, kama ni kodi, kila mtu akatwe kodi, alipe kodi!.
Katika sheria zetu za kodi, tuna sheria mbili, moja ni sheria ya watu wengine wote kulazimika kulipa kodi, na sheria nyingine ni sheria ya miungu watu, ambapo sheria hii imewatenga baadhi ya viongozi wakuu wa nchi, akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwapa msamaha wa kutokulipa kodi yoyote kwa mujibu wa sheria! Exempted.
Sasa ili kuondoa double standards zozote, napendekeza sheria hiyo kwa baadhi ya vingozi kutolipa kodi, ifutiliwe mbali, lakini kwa vile lengo la sheria hii lilikuwa zuri, kumuwezesha ais wa JMT kuweza kuishi vizuri na kipato chake cha urais, ambacho ni TZS 9.5!. Ili rais na wale watendaji wengine wote ambao hawalipi kodi kwa mujibu wa sheria, napendekeza mshahara wa rais na watendaji hao, iongezwe kwa kiwango cha kutosha kuiwezesha kukatwa kodi, kisha kisi kilichobaki kumwezesha rais kuishi comfortably kwa kuzingatia pia rais anatakiwa kugharimiwa kila kitu na sisi Watanzania, kuanzia kula, mavazi, malazi, na mahitaji yake yote yeye na familia yake yote!, hivyo huo mshahara wake sio kwa ajili ya kuendeshea maisha yake, bali ni wa kufanyia mambo yake binafsi, hivyo alipwe vizuri, akatwe kodi, kibaki kiwango kile kile ambacho angekipata bila kulipa kodi!.
Lengo la hatua hii, ni kumuwezesha rais wetu na viongozi wetu kuyaishi maisha wanayoyahubiri, yaani to practice what you preach, haiwezekani kiongozi ahamashishe kila mtu alipe kodi, huku kumbe yeye mwenyewe halipi kodi!, hili likifanyika pia litaondoa double standards ya kila mtu kulipa kodi, na amini msiamini, mnaweza kushangaa, hata kanisa langu, Takatifu Katoliki la Mitume, likaamua kwa ridhaa yake yenyewe, likalipa kodi kwa fedha za sadaka!, kwa sababu yale pia ni mapato!.
NB. Kwa wasiofahamu kuhusu hili la rais kutokulipa kodi, mnaweza kutembelea hapa.
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti Huyu ...
Namalizia kwa swali, jee rais wetu naye alipe kodi ili kumhamashisha kila Mtanzania kulipa kodi kwa hiyari, au kodi tuendeleee kulipa sisi wananchi tuu, na rais wetu asilipe kodi kwa sababu amesamehewa kodi kwa mujibu wa sheria?.
Nawatakia Jumapili njema!.
Paskali
Baadhi ya Rejea za Mtoa Mada Kumhusu Rais Wetu. Dr. John Pombe Magufuli
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM 2015, Ni Dr. John Pombe Magufuli!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply "A Man of The People!".
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, ni vitendo Bila Kuchelewa!.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kweli Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...