Kuepesha Ajali za Mabus ya Abiria Madereva wote Wapelekwe Mafunzoni

Bb YangeYange

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
337
184
Uzembe wa madereva wa mabus ya abiria yaendayo mikoani umekuwa janga la taifa kwa kusababisha vifo vya wananchi wengi na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Ifike mahali Serikali ichukue hatua za makusudi ili kutuepusha na janga hili.

Litakuwa ni jambo jema madereva wote wa mabus yanayoenda mikoani wakipewe mafunzo ya nguvu na kufaulu kabla hawajaruhusiwa kuendesha magari ya abiria. Mfano mzuri ni madereva wa Mabus ya mwendo kasi jijini Dar. Ukipanda kwenye mabus haya utajua wazi kwamba wamepitia mafunzo na wanatumia ujuzi wao ipasavyo. Ninaamini hata hao wengine wakipitia mafunzo stahiki ajali za kizembe zitapungua kama sio kwisha kabisa. It can be done....
 
Nakubaliana na wewe asilimia 100%. Niliwashangaa walipositisha haya mafunzo kuwa ya lazima mwanzoni na kila mara.
 
Mpwa Kuna kitu kinaitwa mazoea! Ukishazoea unaanza kufanya kazi kwa mazoea
Umemwambia la maana,hayo mafunzo sio tiba ya ajali kwa hayo mabasi.Na hizo tochi pia sio suluhu kama tulivyoona ajali ya jana.
Suluhu ya hili tatizo ni askari kusindikiza mabasi mkoa mpaka mkoa.
Hii walilifanya kipindi fulsni nipo dodoma gari za mwanza kutokea dsm zilikuwa zinaingia dodoma saa nane na kuendelea wakat kabla ya kufanya hivyo gar zilikuwa zinaingia dodoma saa tano asubuhi zikitokea dsm kwenda mwanza.
Sijui ilikuwaje wakauacha huo mfumo.
Baada ya ajali kuzid ndio zimekuja hizo tochi.
 
Tatizo si mafunzo. Kinachasababisha ajali ni madereva wengi hasa wa mabasi hawafuati sheria za barabarani.
 
Hata abiria nao wanapaswa kupata hyo kozi mana wao kwa namna moja au nyngne kwa mfano kuna siku mimi nimeshushwa kwenye daladala kisa nilimfata dereva na nikamwambia apunguze mwendo na awe makini mana alikuwa na fujo ambazo hata gari angeendesha ngedere asingefanya aliyokuwa anayafanya basi wote wakanijia juu kwa kauli za kebehi kuwa wana haraka basi wakashauri nilidushiwe nauli yangu nikashushwa lkn nikalilipoti lile gari sasa sijui kama walikamatwa au laa.shauri yao
 
Tatizo sisi watanzania tunapenda mizaha kwa kila jambo siyo madereva tu. Tatizo mizaha kwaanzia juu hadi Chini. Rejea kabwe alivyotumbuliwa
 
Bandugu ajali haitokei kwa dk 5 mala nyingi ni sekunde tuu kabla ya dakika hivyo hata kama ulikuwa abiria mda wa kutamka neno ujue imeshatokea. Na kama ukiweza kutamka mana yake mmesave ajali. Madreva wengi walevi sana wa mirungi na viroba. Trafic waanze kwanza kukomesha hili pasiwe na rushwa tutapunguza sana ajali. Mfano kituo flani polis walikuwa wanakagua madreva walevi kabla mabasi hayajaruhusiwa kilichotokea baadhi walikodi madreva wawatole mabas getini kisha waendelee wwnyewe na mabus yao. Suluhisho nafikiri kufunga chombo maalum kama Utrack ndio suluhisho kubwa maana utaweza kucontrol magari popote na kila kinchofanyika katka gari na nje ya gari
 
Back
Top Bottom