Kuendesha gari Tanzania ni kukaribisha umaskini wa kupindukia

Bora ya Tanzania unaweza ukabargain na police. Nenda nchi zenye camera. Ukizidisha dot tu tayari mwenye gari ndani ya masaa matatu atatumia notice ya kulipa faini inayojumuisha mpaka na gharama za kuletewa hiyo notice.

Ni kweli lakini pale huonewi na kila kitu kipo wazi , pamoja na warning za mfano kupunguza mwendo kwa zaidi ya kilimita moja kabla. Pia kuna warning kuwa sehemu hii ina kamera hivyo punguza mwendo. Hapa kwenyu vibao havipo na unakuta traific kajificha kichakani.
Wala wenzetu hakuna trafic kila kona wana simamisha magari hovyo asubuhi unawaji kazini na Unaanza kudaiwa licence, sijui first aid, sijui triangle, mara leta card ya gari ..nje huwezi kusimamishwa kupotezewa muda wako. Mtu unapanga appointment unafika njiani unasimamishwa uanze kupekuliwa kuonesha kama una jacky hio only in tanzania. Hawajali time zetu
 
Wanajaribu ya Singapore na Rwanda kuhakikisha wananchi wanarudi kwenye public transport, basi tu serikali haitaki kuwaambia live imeona itumie ujanja tu wa kupiga fine za kutosha hadi kieleweke.
 
>>> HUWA ninajiuliza HIZI FAINI zinatumikaje AU moja kwa moja mifukoni kwa WAKUBWA na Kwa nn zisitumike Kukarabati Uniform zinazochania na VIATU vya WALINZI wetu >>
 
Kama ni kweli umelipa fine kwenye speed iliyo ndani ya 50 huo ni uzembe wako kwa sababu polisi wenyewe wanakiri kwamba 50-59 ni provisional speed ambayo dereva anakuwa hana kosa. Kwa uzoefu wangu wa kuendesha high way hakuna hata siku moja nilipigwa fine kwa kuendesha gari kwenye speed 50-59 na hata juzi pale bagamoyo nilipigwa fine kwa speed 61 yule traffic police akasema yaan umezidisha 2 tu. Sasa wewe ebu tueleze vuzuri speed zako zilikuwa ngapi
Hapo ni huruma ya trafiki tu mkuu. Kisheria anatakiwa kukukamata, labda aliona tu unalialia saaana, ndo maana akakuchunia, ila sio kwmb ni uzembe wa jamaa. Hata mimi nilishawahi kukamatwa nikiwa na 65, ila yule trafiki mpiga tochi akanielekeza niende kwa bosi wake aliyekuwa pembeni, nikaenda akaniuliza gari yko ni aina gani, nikamtajia ni RAV 4, akaniambia 'nenda tu, 65 kwa Rav 4 sio mbaya sn, ila uwe makini'. Nikaondoka.

Tatizo watu wenye kazi zao fulani kwa mfano mahakimu hawa vijana. Wakikamatwa badala ya kutoa leseni, anatoa kitambulisho, trafiki anatepeta, anamwambia nenda tu mheshimiwa. Hili ni tatizo na wanalilea trafiki wenyewe kwa kutokusimama katika sheria zinazowaongoza.
 
Ila nashauri msikubali kuwalipa, nahisi hizo pesa hazifiki. Nakumbuka kuna siku walinibandika makosa mawili kwanza leseni imeisha, nikamwonesha passport kuwa nimefika jana na hapa naelekea kurenew passport, pili akadai nimepita taa nyekundu nikamuuliza mbona hizo zingine hazipita mpaka sasa? akasema lazima nilipe, nikamsihi akakataa. nilipokuwa natoa hela akaona hela kwenye pochi akadai nilipe pale nikamwambia we andika nina budget zangu. Akaniandika, ajabu nilipoenda kulipa maxmalipo wakaniambia gari langu na leseni havidaiwi, kuna mavitu wanatandika nikipita fresh. Hii sijaelewa mpaka leo ilikuwaje. Ninayo risiti mpaka leo sikulipa. Tuwe makini kwenye hii nji ya wagagagigikoko kila jambo lawezekana
 
Tatizo la nchi hii hatuamini katika utaalamu, kama wingi wa ajali ndio umesababisha Polisi kuregulate speed, basi wangeanza na tafiti kwanza ionekane ni nini hasa kinasababisha kuongezeka kwa ajali, na kama ishu ni speed kulingana na ubora wa barabara wange ascertain ni katika speed gani hasa itakayopelekea mtu kupata ajali! Haya mambo ya 50kph yasingekuepo!
Sasa ajali zikiongezeka na hiyo 50kph Yao si watashusha hadi 20kph?
 
Mkuu nia ya kuweka faini kwenye makosa ya barabarani sio wewe kulipa faini, tii sheria za barabarani, hakikisha gari yako iko safi kuanzia kadi ya gari, motor vehicle, bima,sticker ya usalama, triangle, fire exitinguisher, spare tyre n.k hapo hutokuja kulipa faini.
 
Tatizo ni moja tu.

Tumecopy sheria kutoka Nchi zilizo endelea na kuhamishia hapa Tanzania bila kuangalia mazingira halisi.

Ndio maana sheria nyingi zimekuwa kimtego mtego na yote kwasababu haziendani na mazingira ya Nchi yetu.

Ndio maana hata ukiwaona Polisi wamekaa kidili dili kwa sababu sheria zimekuwa kama mitego ya Panya kwa Wananchi wake.

Naomba tulipie faini na tuwaheshimu Matrafic wetu kwasababu wao pia hawana jinsi ya kutusaidia kulingana na taratibu walizo somea na wanazopewa kama order.

Mungu mbariki Rais wetu, Mungu bariki Tanzania ameni.
 
Pamoja na umuhimu wa usalama barabarani, kitengo hicho sasa kimekuwa ni kikwazo kwa maendeleo. Kusimamisha magari muda mwingi, kuchelewesha watu, kutafuta makosa ambayo kimsingi siyo muhimu, kuvizia madereva n.k ni vitendo vya kudumaza harakati za kiuchumi kwa raia.
Ili tuendelee ni muhimu kupunguza usumbufu kwa raia kwa kupunguza watumishi kero kama askari wa usalama barabarani.
Ni wazi kwamba mshahara wa askari ni mdogo, na kipato chao kwa asilimia kubwa kinapatikana kwa kudhulumu raia (rushwa) ,hivyo kuwepo wengi ni kuongeza kero.
Hata hivyo, unaweza kuanzishwa utaratibu wa kuweka kamera zinazojiendesha zenyewe kupunguza uonevu unaochochewa na tamaa za kibinadamu.
 
Mimi siku hizi natembea mwendo wa kobe.. juzi walikuwa wanavuata magari pale Salender mida ya asbh basi mimi kama kawaida na speed yangu 42 taratibu. Akaja trafiki kunifokea kwa sauti kumbwa ya amri kwa nini sikimbii naweka foleni. Nilichomjibu kwa sauti kubwa hakuamini maana madereva wote wa pembezoni walipiga honi kunishangilia.. Yule trafiki uchwara alifedheheka sana na naamini hatonisahau kwa jibu lile.
Nifundishe hilo jibu mkuu Mavipunda
 
Watanzania wengi hatujitambui na bahati ni watanzania kidogo walio na uruma kwa wenzao.
Niendesha gari toka Arusha kwenda Ngara ,nilipofika Babati nikasimamishwa na polisi akasema umepita kibao cha 50 ukiwa na 54 faini 30,000 nikalipa.nikatembea taratibu sana kufika Dareda nikakutana na polisi akasema nina picha hapa umepita kibao kwa 50.5 faini. Nikasema we ni mwongo akajibu'tumeelekezwa fedha zote mlizo nazo lazima tuzichue"ni kweli kufika kahama nilikuwa nimeishalipa zaidi ya shill 180,000.wananchi nawaakikishia kama hatapatikana mtaalamu wa kutupangia matumizi bora ya hizi speed tena kwenye highway mtanyanyasika sana na tutaendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.Najua madereva wengi wanateseka sana.Tunanyaswa na kuonewa bila wenyewe kujua.
PESA za kubrashi viatu
 
Na msimu huu ulivyo na wasafiri wengi, watapata pesa nyingi sana
Nasikia jamaa wamepewa target na mkulu n ani lazima ifikiwe so kakosa kokote wanakutoza faini.....Si unajua serikali inaongeza wigo wa mapato kwa ajiri ya uchumi wa viwanda
 
Watanzania wengi hatujitambui na bahati ni watanzania kidogo walio na uruma kwa wenzao.
Niendesha gari toka Arusha kwenda Ngara ,nilipofika Babati nikasimamishwa na polisi akasema umepita kibao cha 50 ukiwa na 54 faini 30,000 nikalipa.nikatembea taratibu sana kufika Dareda nikakutana na polisi akasema nina picha hapa umepita kibao kwa 50.5 faini. Nikasema we ni mwongo akajibu'tumeelekezwa fedha zote mlizo nazo lazima tuzichue"ni kweli kufika kahama nilikuwa nimeishalipa zaidi ya shill 180,000.wananchi nawaakikishia kama hatapatikana mtaalamu wa kutupangia matumizi bora ya hizi speed tena kwenye highway mtanyanyasika sana na tutaendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.Najua madereva wengi wanateseka sana.Tunanyaswa na kuonewa bila wenyewe kujua.
Kwanza ume-overspeed no excuse lipa faini. Pili kama umelipa bila kufanya kosa wewe ni zoba! Tatu nani akupangie matumizi ya highway wakati una leseni? Kama uliipata kwa njia za mkato huu ndio muda wa kulipa gharama!
 
Back
Top Bottom