Kuendesha gari Tanzania ni kukaribisha umaskini wa kupindukia

Rofa

Member
Sep 19, 2015
79
150
Watanzania wengi hatujitambui na bahati ni watanzania kidogo walio na huruma kwa wenzao. Nimeendesha gari toka Arusha kwenda Ngara, nilipofika Babati nikasimamishwa na polisi akasema umepita kibao cha 50 ukiwa na 54 faini 30,000 nikalipa.

Nikatembea taratibu sana kufika Dareda nikakutana na polisi akasema nina picha hapa umepita kibao kwa 50.5 faini. Nikasema we ni mwongo akajibu'tumeelekezwa fedha zote mlizo nazo lazima tuzichue"ni kweli kufika kahama nilikuwa nimeishalipa zaidi ya shill 180,000.

Wananchi nawaakikishia kama hatapatikana mtaalamu wa kutupangia matumizi bora ya hizi speed tena kwenye highway mtanyanyasika sana na tutaendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Najua madereva wengi wanateseka sana. Tunanyaswa na kuonewa bila wenyewe kujua.
 
Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,342
2,000
Watanzania wengi hatujitambui na bahati ni watanzania kidogo walio na uruma kwa wenzao.
Niendesha gari toka Arusha kwenda Ngara ,nilipofika Babati nikasimamishwa na polisi akasema umepita kibao cha 50 ukiwa na 54 faini 30,000 nikalipa.nikatembea taratibu sana kufika Dareda nikakutana na polisi akasema nina picha hapa umepita kibao kwa 50.5 faini. Nikasema we ni mwongo akajibu'tumeelekezwa fedha zote mlizo nazo lazima tuzichue"ni kweli kufika kahama nilikuwa nimeishalipa zaidi ya shill 180,000.wananchi nawaakikishia kama hatapatikana mtaalamu wa kutupangia matumizi bora ya hizi speed tena kwenye highway mtanyanyasika sana na tutaendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.Najua madereva wengi wanateseka sana.Tunanyaswa na kuonewa bila wenyewe kujua.

Kama ni kweli umelipa fine kwenye speed iliyo ndani ya 50 huo ni uzembe wako kwa sababu polisi wenyewe wanakiri kwamba 50-59 ni provisional speed ambayo dereva anakuwa hana kosa. Kwa uzoefu wangu wa kuendesha high way hakuna hata siku moja nilipigwa fine kwa kuendesha gari kwenye speed 50-59 na hata juzi pale bagamoyo nilipigwa fine kwa speed 61 yule traffic police akasema yaan umezidisha 2 tu. Sasa wewe ebu tueleze vuzuri speed zako zilikuwa ngapi
 
Rohombaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
12,104

Dah...Rofa kweli kweli wewe...taratibu sana ndiyo speed gani?......na utalipa hadi unyooke....katengeneze hiyo speedometer bana:cool::cool:
 
haibreus

JF-Expert Member
Oct 1, 2009
295
225
Honestly inaboa sana hali ilivyo sasa hivi na ninadhani soon tunarudi kwenye public transport maana watu haiwezekani Kwa week moja upoteze Karibia laki kwa ajili ya traffic offence? Kimara , Mbezi makonde ,Mabibo external ,Bagamoyo nk ni too much.
Nadhani traffic police wa sikuhizi wana maelekezo maalum kwamba lazima upige fine tu na si vinginevyo, tofauti na zamani unaweza hata kupewa elimu na au hata onyo tu ukaachiwa..Juzi kati pale kitonga kuja comfort nimemuona jamaa kakaa juu ya jiwe refu kama mdunguaji nikasema duh tunakoelekea sasa balaa
 
NAMTUMBA

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,940
2,000
Huko Ngara ni mbali. Nimetoka posta kwenda kibaha kupitia Mwenge nilikuwa na mishe za hapa na pale. Kufika Sarenda bridge naambiwa nimevuka taa nyekundu na nimemkimbia traffic makosa mawili kwa huruma nikaambiwa nilipie kosa moja. Kipande cha Mwenge-Ubungo kulikuwa na sijui msafara Sijui nini jamaa walikuja kwa speed sana pale maeneo ya kivulini kwamba nimesikia king'ora cha msafara sijachukua tahadhari nataka kufanya uhaini nikatishwa tishwa sana kwamba nitafungwa wakazuga wamenihurumia wakanipiga 30. Kufika baruti nikasimamishwa nikaoneshwa torch kwamba nimeoverspeed 53 nikawaambia sijaona kibao ndipo nikaambiwa TOKA POSTA HADI NJIA YOTE NI 50 NA HAKUNA KIBAO wakanichukuli 30. Pale mizani ya zamani maili moja tena nikaambiwa nine overtake sehemu isiyoruhusiwa kumbe nilifanya kwakuwa kuna roli lilipata na waliwasha hazard light na walikuwa wanajiandaa kuwaeka reflectors nikajaribu kujitetea haikusaidia. Yaani utetezi ulikuwa nikupoteza muda kumbe jamaa walishajipanga kuniandikia walikuwa wanasubiri license number tu. Ikawa hadi kufika maili moja nimelipa 120,000. Inaumiza sana sana sana.

Kuna haja na kila sababu ya wananchi kupaza sauti serikali kupitia jeshi la polisi wanatufilisi na kutuletea umasikini.
 
ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
2,096
2,000
Kama ni kweli umelipa fine kwenye speed iliyo ndani ya 50 huo ni uzembe wako kwa sababu polisi wenyewe wanakiri kwamba 50-59 ni provisional speed ambayo dereva anakuwa hana kosa. Kwa uzoefu wangu wa kuendesha high way hakuna hata siku moja nilipigwa fine kwa kuendesha gari kwenye speed 50-59 na hata juzi pale bagamoyo nilipigwa fine kwa speed 61 yule traffic police akasema yaan umezidisha 2 tu. Sasa wewe ebu tueleze vuzuri speed zako zilikuwa ngapi
Ndugu Saju b, inaelekea una uelewa wa hii kitu tafadhali unaweza ukafafanua kiasi haya mambo na sheria ya speed limit highway......
1.Bongo maximum speed kwa private cars ni ngapi?
2.provision speed katika speed wekwa ni ngapi?
3.Vibao vingine barabarani havionekani ila nyangenyange wanataka kukukwangua mshiko.
4. Na sheria au maelekezo ya ziada ya hili tafadhali.

NB: lengo ni kujifunza, kuelewa tu na kuzuia ajali na usumbufu unaoepukika
 
Macos

JF-Expert Member
May 12, 2008
1,936
2,000
Wewe ukiona polisi wanatangaza kila mwezi kuwa leo mkoa wa Dar tumkusanya billion kadhaaa wa kadhaa ujue kuna tatizo kubwa. Sasa barabara na gari zimegeuzwa rasmi kuwa vyanzo vya kodi. Na yapo malengo ya ukusnyaji huo basi ujue kuendesha gari ni kweli imekua nongwa.
Kazi ya trafic sio kuvizia ili apate mwanya kukutoza kodi. Kazi yao ni pamoja na kuelimisha na kujikita maeneo yanayo sababisha ajali.
Leo trafic sign mjini Dar zimewekwa kimtego ili ukosee, hazipo standard kama zilivo nchi nyengine.
Yote haya lengo kutukomoa.
Trafic lights hazipo standard maalum kwa sehemu zote.
Sehemu nyengine kuturn inaonesha mshale , kwengine inaonesha green.
Sehemu moja utaruhusiwa ku filter sehemu nyengine unakamatwa,
Ukipita siku nyengineile uloruhusiwa unakamatwa na ile nyengine unaruhusiwa
Nchi zote huwa zinatoa ripoti za mwenendo wa barabara kila mwezi. Wanatangaza ajali ngapi zimetokea na kama kuna upungufu , watu wangapi wameumia na wangapi wamefarik.
Wanaripoti mchanganuo wa makosa mbali mbali walokamatwa nayo madereva . Sijawahi sikia wakitangaza tumekusanya fedha ngapi.
Sasa statistics zetu ni fedha ngapi tunapata na sio ajali na makosa na sababu za ajali ili kurekebisha.
 
nra2303

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
2,752
2,000
Kama ni kweli umelipa fine kwenye speed iliyo ndani ya 50 huo ni uzembe wako kwa sababu polisi wenyewe wanakiri kwamba 50-59 ni provisional speed ambayo dereva anakuwa hana kosa. Kwa uzoefu wangu wa kuendesha high way hakuna hata siku moja nilipigwa fine kwa kuendesha gari kwenye speed 50-59 na hata juzi pale bagamoyo nilipigwa fine kwa speed 61 yule traffic police akasema yaan umezidisha 2 tu. Sasa wewe ebu tueleze vuzuri speed zako zilikuwa ngapi
Mkuu wanakamata mfn wiki iliyopita nilikua naenda iringa,sawa pale nyuma kabla ya kuanza mbuga hua wanajificha pale nilikua na speed ya 56 na jamaa akakomaa mpk akaniandikia.Ila nashukuru nimejifunza kitu key hiyo provisional speed,IPO kisheria kabisa au?
 
Mavipunda

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
5,980
2,000
Mimi siku hizi natembea mwendo wa kobe.. juzi walikuwa wanavuata magari pale Salender mida ya asbh basi mimi kama kawaida na speed yangu 42 taratibu. Akaja trafiki kunifokea kwa sauti kumbwa ya amri kwa nini sikimbii naweka foleni. Nilichomjibu kwa sauti kubwa hakuamini maana madereva wote wa pembezoni walipiga honi kunishangilia.. Yule trafiki uchwara alifedheheka sana na naamini hatonisahau kwa jibu lile.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom