Kuendesha gari na sandles kwa traffic ni kosa?

uduzungwa

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
551
1,000
Wakuu salama za sikukuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.

Nimetoka zangu gereji naingia tu. Main road hapa maeneo ya mianzini. Nikasimamishwa na traffic. Kaanza na mambo yambo yake, naomba leseni yako, nikampatia. Akanibambikia makosa yake kaanza eti naongea na simu nikalichomoa,
kubwa kuliko akaniambia naendesha nikiwa nimevaa sandles (nimevaa viatu vyisivyo na kamba ya nyuma).
kanikomalia hapo, afu hapo faini ya 30 sina.
Nikabembeleza balaa.

Jamani naomba kuuliza eti ni kosa kuendesha gari ukiwa umevaa sandles.

Wenye ujuzi wa makosa ya barabarani. Hili nalo lipo kwenye list.
 
EP PRO

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
7,687
2,000
Strange, ila sina hakika na sheria hiyo.

Ngoja tusubiri majibu zaidi.

Ila jamaaa anaweza kuona una woga na kukosa kujiamini so akawa ana jisemea analotaka tu
 
Akotia

Senior Member
Dec 16, 2016
138
250
Wakuu salama za sikukuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.

Nimetoka zangu gereji naingia tu. Main road hapa maeneo ya mianzini. Nikasimamishwa na traffic. Kaanza na mambo yambo yake, naomba leseni yako, nikampatia. Akanibambikia makosa yake kaanza eti naongea na simu nikalichomoa,
kubwa kuliko akaniambia naendesha nikiwa nimevaa sandles (nimevaa viatu vyisivyo na kamba ya nyuma).
kanikomalia hapo, afu hapo faini ya 30 sina.
Nikabembeleza balaa.

Jamani naomba kuuliza eti ni kosa kuendesha gari ukiwa umevaa sandles.

Wenye ujuzi wa makosa ya barabarani. Hili nalo lipo kwenye list.
Kwa kumbukumbu zangu ni kosa,VP ulisomea kupata leseni kweli au ndo zile leseni zetu za kilo unusu?
 
John-Q

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
562
1,000
Sijui kisheria kuhusu hili ila kiusalama nadhani sio vizuri kwa sandles. Ilishanikuta sandle ilinasa bado nikashindwa kutoa mguu kuweka kwenye brake ni bahati tu
 
Yumbayumba

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,206
2,000
Ni kosa, na sio gari tu hata pikipiki kwakifupi chombo chochote cha moto huruhusiwi kuendesha ukiwa umevaa kiatu cha wazi
 
MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
2,510
2,000
Kwa miaka ya nyuma ilikuwa kosa kuendesha chombo cha moto ukiwa na ndala ila kadri miaka inavyoenda tunaendesha tu na tunaendesha tukiwa na yeboyebo, bukuta na kaoshi.
Hata mzungu anaendesha ndege akiwa na bukta na sandle.
 
Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,707
2,000
Ndiyo maana kila siku mnaambiwa mkasomee sheria za barabarani siyo siku mbili umeshajua kuweka D na R unajiona umemaliza udereva ni utii wa sheria tu kwa usalama wa gari lako na wewe pia na watumiaji wengine wa barabara na siku hizi gari zenye mfumo wa Manual zimekuwa adimu ni bwerere tu
 
kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,327
2,000
notification yako imeandikwa kosa namba gani? notification inaandikwa koda la barabarani ulilolitenda,nyuma ya karatasi vipo vifungu na makosa yake! SANDALS HAMNA.

HATA UKIWA UCHI UNAWEZA KUENDESHA TU!
 
Mr. Django

JF-Expert Member
Jul 25, 2014
1,821
2,000
Sijui kisheria kuhusu hili ila kiusalama nadhani sio vizuri kwa sandles. Ilishanikuta sandle ilinasa bado nikashindwa kutoa mguu kuweka kwenye brake ni bahati tu
Your username "John Q" is my favourite movie from D. Washington.

Ni kosa kisheria kuendesha gari na Sandles. Kama huna viatu bora uendeshe peku.
 
Jick

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
474
500
Kwa swali lako bila shaka hiyo leseni uliipata ukiwa Garage.

FYI sandal sio sehemu ya vazi rasmi sehemu yoyote. Wala sio vazi la kufanyia shughuli yoyote isipokuwa kuogea

Katika jiji LA Kigali uukionekana na Sandal mtaani unapata adhabu Kali.
 
Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,716
2,000
Ni kosa ila cha kushangaza makosa yote police wanacharge bei moja wakati ilivyo makosa wengine ni onyo tu na kuna ya 20,000 au 25,000 na jela au yote kwa pamoja
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom