Kuendelea kwa taifa lolote ni kujitegemea kwake, huwezi kujitawala kama hujitegemei

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
609
1,000
Maendeleo yote ya binadamu yametokana na gunduzi alizofanya, kwahiyo tunapozungumzia maendeleo ya binadamu hatuwezi kuepuka kuongelea gunduzi alizofanya na ukuaji wa kiakili wa jamii husika.

Huu ugunduzi na uzalishaji mali ndio ulikuwa chimbuko la maendeleo na biashara katika jamii nyingi. Jamii zilizozalisha zaidi zilifanya biashara na kupata faida. Waliuza bidhaa walizogundua na kujiongezea mitaji na mahitaji pia ya malighafi yaliongezeka, yaliyowafanya watoke kutoka katika nchi zao kwenda nchi nyingine kuyatafuta, pamoja pia na kutafuta masoko ya bidhaa zao.

Kwahiyo pasipo gunduzi maendeleo ya binadamu yangeendelea kuwa duni. Kwahiyo tukizungumza maendeleo tunazungumza ''material things'' na mara nyingi hatumzungumzii binadamu mwenyewe bali vitu alivyofanya na mali anazomiliki.

So mahitaji ndio yaliyofanya watu kufikiria kugundua na ndio hapo maendeleo yalipokuja haya tunayoona ya vitu. Mahitaji ya kukabiliana na baridi yaliwafanya watu wagundue moto. Katika kila changamoto ilipotokea wapo watu waliofikiria na kupata jibu lake. Tutazungumza hivyo hivyo kwenye magari, ndege, meli na vitu vingine vingi ambavyo vimesababishwa na mahitaji yaliyowafanya binadamu kufikiri na kugundua. Binadamu ni tofauti na wanyama kuna kitu ndani yake cha kipekee kinachomtofautisha yeye na wanyama. uwezo wake wa ku form image katika akili yake ni wa kipekee { imagination power}.

Kitu kinachomtofautisha binadamu na wanyama wengine ni uwezo wake wa kufikiri na kuchanganua mambo. Changamoto za mvua, jua na wanyama wakali ziliwafanya binadamu wafikirie kujenga nyumba kwahiyo kila changamoto ilipotokea binadamu alifikiri na kujaribu kutatua changamoto hiyo.

Na hapa ndipo chanzo cha utajiri wa mataifa ulipoanza. Wale watu ambao akili zao ni duni walioshindwa kukabiliana na changamoto waliachwa nyuma na wengine kumezwa na mazingira na kupoteza maisha kwa baridi, magonjwa nk. Wale waliotumia nguvu zao za akili vizuri walizishinda changamoto zao na kuwatawala mazingira yao. so binadamu wa kale sio huyu tuliyenae bali akili zake zimekuwa evolve generation hadi generation and manifestation of it, is the things we see.

The product of mind in action. Binadamu anakufa lakini akili haifi inaendelea kuwepo kwa watu wengine. Ni akili hii hii inayotusaidia kuishi maisha yetu hapa duniani vizuri au vibaya kulingana na tunavyoitumia ni upanga wa pande mbili. Inazalisha ubaya na wema.

So waliogundua wanawauzia wasiogundua kutokana na mahitaji ya bidhaa zilizogunduliwa kwa jamii yao. Lakini waliogundua they are always superior zaidi ya wale wasiogundua. Kwahiyo Afrika ni ngumu kuendelea wamegundua vitu vichache na technologia yao ni ya chini, inayoonyesha level ya maendeleo yao na uwezo wa akili zao. So dependency yetu ya technologia ni kubwa kitu ambacho viongozi wetu wanapaswa kufikiria na kuzinduka sasa na kuwekeza kwenye research and development.

Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea kuuza raw materials. Viongozi lazima wafikirie hili hakuna nchi iliyoendelea kwa raw materials. Hakuna super power hata moja iliyoendelea kwa sababu ya raw materials. But invention zilifanya mataifa kuendelea. Watu lazima wapeleke mkondo wa mawazo yao huko. Demand for raw material zilitokana na invention walizofanya watu. Kwahiyo bila invention raw material hazina thamani zingeendelea kubaki ardhini. Ni muhimu sana kuwekeza katika mind za watu na kuzi shape kuwa bora na sharp like razor.

Tusitegemee kwamba kwasababu tuna raw materials ambazo hatujahangaikia wala kutoa jasho tumezikuta ardhini tutafaidika nazo kuliko wale waliohangaika kwa jasho na akili nyingi kufanya gunduzi hadi hizi raw material kuwa na thamani. Wakati sisi tukiwa tumelala usingizi au tukiwa tumekaa kijiweni tukinywa kahawa.

Wameunda mashine za kuchimba hizo raw material kwanza pili wameweza kutengeneza hizo raw material kuwa kitu useful alafu wewe unategemea ufaidike kuliko yule aliyegundua machine za kuchimba mafuta kwa mfano na kutengeneza gari kweli? utapata kidogo sana. Hiyo mali ardhini hujaihangaikia hata chembe, hujatoa jasho lolote ipo tu ardhini.

Na pengine ulikuwa hujui kama ina thamani hadi ulipofanyika ugunduzi. Kwahiyo lazima tujue sehemu yetu ni ndogo sana kwenye hizi raw materials hadi tuwe na uwezo wa ki technologia. Hatuwezi endelea kwa kuwa na raw material peke yake. Lazima tuwe na watu wenye akili.

Kwahiyo akili za watu, nidhamu na jinsi gani wako organized is the key kwa nchi ndogo kuendelea. Kwanza ni lazima iwepo dhamira ya dhati ya kutaka kuendelea kama taifa. Na sio kuishi sababu ya mkate. Dhamira hiyo iwepo kwa wananchi na kwa viongozi kujenga nchi yenye malengo. Kwenye kutafuta mkate watu watavurugana kwasababu watu wanaishi kwa tumbo wanashindwa kuruhusu akili zao kufanya kazi kwa faida ya taifa. Kuna umuhimu wa mabadiliko ya kimtizamo.

Tujiulize kwa hakika ni kweli tunataka kuendelea kama taifa? Dhamira zetu na utashi wetu ni mkubwa kiasi gani kutaka taifa hili liendelee? je tabia zetu zinaonyesha kwa kiwango gani nia yetu ya kutaka taifa hili kuendelea? tuko serious kwa kiwango gani? Tufanye research kidogo tujue thinking za vijana wetu zikoje tukienda kwenye mitandao ya kijamii na mitaani? AU TUNALALA NA KUAMKA NA KULA NA BORA LIENDE na kushikiria fikra za kibinafsi na sio utaifa?

Kuendelea kwa taifa lolote ni kujitegemea kwake. Huwezi kujitawala kama hujitegemei. kwahiyo lengo letu kama taifa ni kujitegemea kwetu na hicho ndio kiwe kipimo cha maendeleo yetu. Hauwezi kujidanganya kujipima kwa kipimo kingine chochote. Kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zetu wenyewe kwa kutumia nguvu zetu na akili zetu wenyewe. Kipimo cha maendeleo ni kujitegemea kwetu. Na hatuwezi kuwa huru tusipofikia uwezo wa kujitegemea kama taifa.

Pengine tujiulize tutakuwa omba omba na watu wa kulia lia hadi lini? Tunapaswa kutimiza majukumu yetu. Sasa hivi watu wanafikiria kugundua kinga ya covid tunawasubiri watuletee! Tumekuwa wavivu wa fikra. Na pengine ndio sababu ya wao kutudharau na kutuona kama ni watu ambao hatujafanya chochote kuleta mapinduzi katika dunia hii. Tumekuwa watu wakufundishwa tu na sio kufikiri na kugundua na kufundisha wengine. Tumekuwa watu wa kupokea zaidi kuliko kutoa.

Kwahiyo tusijidanganye tumeendelea wakati hatujaondoa basic needs za wananchi. Bado kuna shida ya malazi, shida ya mavazi, shida ya chakula na mahitaji mengine ya muhimu kwa binadamu ili raia wa nchi hii aishi a comfortable standard life. bado kuna maradhi, bado kuna ujinga bado kuna umaskini. lakini kubwa kuliko yote ni ujinga na kuwa na watu ambao akili zao hazijapevuka wengi. Na wengine hata kama wameenda shule. We see it in their conduct. Kwakuwa tabia ambazo wanaonyesha hazisaidii taifa kuendelea.
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Azimio la Arusha: ".... Kujitawala ni kujitegemea, kujitawala kwa kweli hakuwezekani iwapo taifa moja linategemea misaada na mikopo kutoka taifa jingine kwa maendeleo yake."

Hivi Tanzania ingeanzia wapi bila misaada na mikopo?
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Pengine tujiulize nchi kama uingereza na nyingine ziliwezaje kuendelea?

Ni swali la kifalsafa hilo......Misaada na mikopo ilipoanza kutolewa kwa nguvu kwa chini masikini mwishoni mwa 1960s kila mtu alitegemea matokeo mazuri ya misaada hiyo. Miaka 50 baadaye ndio tunaona kuwa mambo yalikuwa ni mazito....Hivyo hilo ni swali ambalo tulitakiwa kujaribu miaka ya 60....Kuna nchi zilizojaribu kama China, Romania ....lakini hizi zilikuwa angalau hata na ujuzi wa kutengeneza sabuni...
 

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
609
1,000
Ni swali la kifalsafa hilo......Misaada na mikopo ilipoanza kutolewa kwa nguvu kwa chini masikini mwishoni mwa 1960s kila mtu alitegemea matokeo mazuri ya misaada hiyo. Miaka 50 baadaye ndio tunaona kuwa mambo yalikuwa ni mazito....Hivyo hilo ni swali ambalo tulitakiwa kujaribu miaka ya 60....Kuna nchi zilizojaribu kama China, Romania ....lakini hizi zilikuwa angalau hata na ujuzi wa kutengeneza sabuni...

So misaada na Mikopo inatupeleka kwenye kujitegemea kwetu?
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
So misaada na Mikopo inatupeleka kwenye kujitegemea kwetu?
Tunaweza kujitegemea hata leo kama tutahamua hivyo. North Korea, Cuba, and Iran wanajitegemea. Kujitegemea maana yake ni uwezo wa kuendesha shughuli zako bila msaada wa nchi nyingine.

Kitu ambacho hatuwezi ni kujitegemea tukiwa na ubora wa maisha tunayoyataka. Tunataka tuwe kuendesha V8s, tuishi kwenye nyumba za kisasa. Tupeleke watoto shule nzuri. Kwa ujumla tunataka tuwe na mambo ambayo uchumi wetu hauwezi kuyafanya.

Na kwa sababu tunatumia zaidi ya uwezo wa uchumi wetu ni lazima tukope au kuomba misaada.
 

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
609
1,000
Tunaweza kujitegemea hata leo kama tutahamua hivyo. North Korea, Cuba, and Iran wanajitegemea. Kujitegemea maana yake ni uwezo wa kuendesha shughuli zako bila msaada wa nchi nyingine.

Kitu ambacho hatuwezi ni kujitegemea tukiwa na ubora wa maisha tunayoyataka. Tunataka tuwe kuendesha V8s, tuishi kwenye nyumba za kisasa. Tupeleke watoto shule nzuri. Kwa ujumla tunataka tuwe na mambo ambayo uchumi wetu hauwezi kuyafanya.

Na kwa sababu tunatumia zaidi ya uwezo wa uchumi wetu ni lazima tukope au kuomba misaada.
Lakini tunamahitaji tutajitegemeaje pasipo kuwa na uwezo wa kutimiliza mahitaji yetu?
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Lakini tunamahitaji tutajitegemeaje pasipo kuwa na uwezo wa kutimiliza mahitaji yetu?

Ni swali ambalo tumesumbuana nalo toka uhuru upatikane. Waingereza uliotolea mfano hawakuwa na matatizo hayo. Wao walikuwa wa mwanzo au miongoni mwa mataifa ya mwanzo kugundua vitu au kufanya vitu ambavyo vime-define modern society. Hivyo vitu yote waliyokuwa nayo yalitokana katika mazingira yao na kukidhi mahitaji yao. Na walikuwa na competitive advantage ambayo waliilinda.

Kwa upande wetu vitu vingi ambavyo vina-define modern society yetu ni kutoka nje. Kwa mfano ni lazima tutunue magari kutoka Japan. Lakini Japan haina ulazima wowote wa kununua kitu kutoka kwetu. Na kama Japan ingekuwa na ulazima wa kununua vitu kutoka kwetu, basi tungeweza kumwambia kuwa thamani tunayotumia kununua gari kutoka Japan, Japan itumie thamani hiyo hiyo kununua mahindi kutoka kwetu. Kwa uwiano kama huu, pesa zinazotumika kuagiza vitu kutoka nje vyenye ku-define modern society yetu zinalingana na pesa zinazoingia ndani ambazo zingesaidia kuongeza mzunguko wa pesa ambao ungefanya watu wawe wabunifu zaidi.

Hicho nilichoandika ni kizingizio. Ukiondoa visingio, na sisi tunawajibu wa kuelewa kuwa kila taifa linajaribu kulinda maslahi yake kwanza. Na hili tulinde maslahi ya taifa kuna vitu muhimu vya kuangalia. Kwanza ni kuangalia priorities zetu. Kama moja ya priority ni kujitegemea, basi ni lazima tuwe na nidhamu katika matumizi yetu.
 

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
609
1,000
Hivi Tanzania ingeanzia wapi bila misaada na mikopo?
Watu wanaana kwanza kwa kufanya kazi ili wapate capital, Capital ni product of work. Hii misaada na mikopo tunayoshangilia watu walifanya kazi na kupata surplus ya kutosha. Na surplus ndio huleta maendeleo kwasababu ndio hiyo hufanya watu wa invest zaidi. Kama hatuzalishi zaidi kama taifa lazima tuwe maskini na lazima tusaidiwe KWASABABU productivity yetu ni ndogo. Kusubiria mikopo tu na hii sio akili nzuri sana. Hakuna Taifa lililoendelea kwa mikopo. Tatizo we don't utilize our human resource well. Wakati mwingine matumizi ya akili zetu huwa ni madogo tunakimbilia shortcut kwenye maendeleo. Ukweli ni kwamba hatuwezi kusimama kama taifa kwa mikopo. We will be always slaves kwa wale wanaotukopesha ila kujitawala itakuwa ni ndoto. Walioendelea walihenyeka, walitumia akili, nguvu, maarifa, jasho na damu na hakukuwa na mjomba wa kuwakopesha. They toil. They use their mind to bring progress to their Nations. Na hii mikopo italiwa tu na viongozi wasio na dira.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom