Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Wakati Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo akiomba Serikali ipunguze tozo za kuingia katiba hifadhi ya wanyama ya Serengeti, Spika wa Bunge Job Ndugai naye amesisitiza ombi hilo akiitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia viwango vyao kwani grafu ya utalii inashuka.
Hata hivyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amesema viwango hivyo haviwezi kushuka kwa kuwa hifadhi ya Serikali ni bora zaidi duniani alipokuwa akijibu swali la Gambo leo Jumatatu Februari 8,2021 bungeni jijini Dodoma.
Dk Ndumbaro alisema tozo ya sasa katika hifadhi ya Ngorongoro ni dolla 60 ambazo ni ndogo ukilinganisha na ubora na viwango vya vivutio ndani ya hifadhi hiyo.
Katika swali la nyongeza Gambo amehoji ni kwa nini Serikali isione umuhimu wa kupunguza tozo hiyo ili kuwavutia watalii.
Gambo alitolea mfano wa Kenya na Rwanda kwamba wamepunguza tozo kwa ajili ya kuwavutia watalii ambao wamepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na tishio la ugonjwa wa Uviko.
"Ni kweli kuwa ugonjwa wa korona umepunguza idadi ya watalii kuingia nchini ni kwa nini msilione hilo kama walivyofanya mataifa mengine jirani," amehoji Gambo.