Kuendelea kupatikana kwa madawa ya kulevya, nani mzembe?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Najiuliza ni nani haswa asiyewajibika kwa kutokomeshwa kwa biashara haramu ya madawa ya kulevya. wengi wameuwana, wengi wamejeruhika kwa biashara hii.

Sijui ni nani hasa anaifanya japo wanaotuhumiwa ni wengi: mtoto wa rais mstaafu, wabunge, madiwani, wafanyabiashara wakubwa kama 'SHKUBA', watoto wa vigogo, madereva bodaboda, makondakta na watu chungu mzima. je, ni kweli serikali imeshindwa?

Sijajua nani hawajibiki ipasavyao kama ni rais, Waziri mambo ya ndani, IGP na kikosi maalumu cha kupambana na madawa ya kulevya au wananchi kutotoa taarifa.

hali ni mbaya kwa vijana wanaojiingiza ktk biashara hii. wacheki akina CHID BENZ, RAY C. tulishawahi kumpoteza MANGWAIR n.k
 
Raia tunao wajibu mkubwa wa kusema NO kwa wauza madawa ya kulevya, kwani sisi ndiyo tunaoishi na wauza madawa ya kulevya na kufurahia pesa haramu ya madawa ya kulevya. Tuwaseme katika vyombo vya dola na wasipochukuliwa hatua tuwakatae katika mitaa yetu.
Kwa hatari ya dawa za kulevya ikibidi raia tupige yowe dhidi yao na kuwakamata na kuwafikisha ktk vyombo vya dola
 
Serikali ndo imeshindwa.Kama tumeshindwa kudhibiti sukari inayo onekana tutaweza madawa serikali si rafiki wa watu.
 
Ukimkamata teja mmoja ukamwambiya akupeleke kwa muuzaji atakupeleka na muuzaji ukam'bana akupeleke kwa bos wake kuna uwezekana wakukupeleka vipi uki muomba mtu aliye acha kutumia akupeleke kwa alie kuwa aki wauzia jee atakataa kukupeleka??? Kama hato kataa basi lawama naziwe niza serikali.
 
Kama China na sheria zao za kunyonga wameshindwa kudhibiti itakuwa sisi?.Mtandao wa madawa ya kulevya unaongozwa na matajiri wakubwa na hata viongozi wazito,ni ngumu kuidhibiti hii biashara kwa100%.

Ni sawa na CHATU kummeza TEMBO!
 
Back
Top Bottom