Kuendelea kung'ang'ania ofisi huku muda wa kustaafu umefika inahashiria nini?

Njaa Mbaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
666
175
Watendaji wengi wa ngazi za juu hawataki kustaafu hata muda wao kisheria unapofika, wanafanya mazungumzo na washauri wa raisi ili kuhakikisha wanaendelea kuwepo kwenye nyadhifa hizo hata baada ya umri wa kustaafu kufika. Kwa sasa kuna makatibu wakuu wanahaha huku na kule kuhakikisha wanaendelea na nyazifa hizo watendaji kama wa TRA muda wake ulifika akalobu mpaka akaongezewa muda na wengine wengi. Nasikia hata mzee wa TRA muda wake aliohongezewa unaenda kuisha anafukuzia aongezewe tena sasa tunajiuliza ni lini watapumzika hata kizazi kipya kifanye kazi.

Soma gazeti la uhuru tarehe 10/10/2012 uone miujiza, mpaka gazeti la magamba limewachoka
 
Tangu anaanza kuajiriwa hajawahi kufuga hata chura wa kula,kila kitu analetewa,hajawahi kuuza hata ICE CREAM,ana kikampuni kinapata tenda za usafi bcoz yeye yuko ofcn,sasa akiondoka si atakuwa MATONYA?
 
hakika serikali kwa ujumla wake inabidi ifanye clinic maalum ktk idara zake zote kuna viongozi wanaobuni mbinu za uongo kwa watawala wakijifanya bila wao kazi haziendi hakika ni waongo na wadhambi kabisa nawakumbusha kiongozi ni kiwanda anatakiwa azalishe warithi wake kama kashindwa kufanya hivyo ujue anajiandaa kutotoka ofisini muda wake ukifika naomba clinic maalum iandaliwe wote waende nyumbani
 
wa2 wanataka hadi wafie kazin kwan hela inanoga ackwambie m2 na ndo mana hata umri uende vpi lakin katika suala la kuachia madaraka ni ishu we angalia wazee wengi wa kiafrika ni wabishi mfano akina Mugabe wa Zimbabwe,Kibaki wa Kenya, Museven wa Uganda na wazee wengine wanataka wang'olewe kama akina Gaddafi
 
Yote mliyoandika ni sahihi kabisa kuna mzee mmoja niliwahi kumsikia akisema hivi nikitoka hapa kazi zitaendaje maana sioni wa kuweza kuendesha hii taasisi. Ni mambo ya ajabu unakuta mtu mzee akifika ofisini saa tatu kaisha sinzia lakini bado anakuambia ni yeye tu. nadhani ifike mahali ikifika muda wa kustaafu mtu aondoke kama ana ujuzi wa ziada tumtafute katika usahuri lakini siyo utendaji wa kila siku. Utamuona mzee akishindwa kufanya lobing abaki anibukia kwenye bodi kama si kugombea ubunge jamani utaki kukaa kupumzika na kucheza na wajukuu du madaraka bila kimoko ni hatari mtu mpaka anadhindwa kutofautisha yeye na ofisi
 
wa2 wanataka hadi wafie kazin kwan hela inanoga ackwambie m2 na ndo mana hata umri uende vpi lakin katika suala la kuachia madaraka ni ishu we angalia wazee wengi wa kiafrika ni wabishi mfano akina Mugabe wa Zimbabwe,Kibaki wa Kenya, Museven wa Uganda na wazee wengine wanataka wang'olewe kama akina Gaddafi

msiba kwa dunia hasa afrika
 
Ifike sehemu sisi vijana tuwe tunawatoa ofisini kwa nguvu. We need old men, but not in daily operations. Let them stay at home and come up only when we need them to advise us. Hawa wazee ndo maana kila siku wanatusingizia eti vijana hatuwezi, kumbe ni janja yao tuu ya kutaka waendelee kukaa maofisini. Hawa wazee kwa kweli wanatakiwa wafikirie mara mbilimbili.
 
mfano mzuri nilisoma kwenye gazeti wiki iliyopita, kuna katibu mkuu WIZARA YA UJENZI muda wake uliisha akaomba kuongezewa mwaka nao umeisha mwisho wa mwezi wa tisa....sasaiv hajatoka ofisini na hakuna mikataba anayoingia kisa anasema anamsubiri katibu mkuu kiongozi aje amuongeze muda tena kwa kujitamba kwakua ni ndugu yake.......

swali ni hili hivi wizara nzima hakuna watu wanaofaa kuchukua hiyo nafasi au ?
pili, kujitamba mbele ya watu kama hivyo kuwa ataongezewa muda inamaana serikali kaiweka mfukoni au ?
 
SGB hiyo kitu ni kweli hata mie nimeisoma sema sijui jinsi yakuipata lini......but gazeti lipo
 
Mimi nadhani mwisho wa haya yote nafasi za uteuzi zibaki kwenye vyeo vya kisiasa tu watendaje wapatikane kwa kufanyishwa interview na kushindanishwa na watu wengine itapunguza sana watu kujisahahu na kuona kuwa nafasi aliyonayo ni haki yake kwa kuwa alipewa kwa kujuana na si uwezo
 
Back
Top Bottom