Kuendelea kuimarika demokrasia Katika nchi za Afrika Magharibi kunatupa somo gani?

KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
762
1,598
Leo kwa mara nyingine tumeshuhudia chaguzi mbili zikifanyika huko Afrika Magharibi. Ila uchaguzi unaotazamwa sana ni ule wa Nigeria.

Kwa viwango vyovyote vile, uchaguzi wa Nigeria ambayo ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa na pia yenye idadi kubwa zaidi ya watu inaweza kuwa kioo cha kujitazamia kwa hawa watawala waliobakia wachache wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati wanaoamini katika udikteta.

Huku demokrasia ikiimarika katika nchi za Magharibi na kusini mwa Afrika, tunaendelea kujionea katika ukanda huu kuimarika kwa vituko vya demokrasia kuanzia Kongo, Burundi, Rwanda, Uganda, na hivi karibuni Tanzania.

Huku tukisubiri mshindi, dalili za awali zinaonyesha ukomavu mkubwa wa demokrasia katika kanda hizo tofauti na huku kwetu wanaofikiri kuua wapinzani ndiyo njia sahihi ya kubakia madarakani. Inakera lakini huenda ndicho Mungu alichotupangia. Huenda Mungu anataka tuone machungu ya udikteta angalau kwa muda kidogo ndipo tujikomboe wenyewe.

Hayo yalikuwa maoni yangu tu. Je, wewe unapata somo gani kwa uelekeo wa Afrika katika kanda nyingine ukilinganisha na ukanda wetu huu wa maziwa makuu unaotambulika kwa mauaji na vurugu za kila aina na tawala za mabavu???

Karibuni.
 
Nenda Afrika magharibi ukajionee maisha ya watu utashangaa nchi inayozalisha mafuta mengi, lakini wananchi shida tu, tunataka kiongozi anayesimamia Maendeleo na kulinda mali za umma, hatutaki demokrasia mahali palipo jaa rushwa.
 
Nenda Afrika magharibi ukajionee maisha ya watu utashangaa nchi inayozalisha mafuta mengi, lakini wananchi shida tu, tunataka kiongozi anayesimamia Maendeleo na kulinda mali za umma, hatutaki demokrasia mahali palipo jaa rushwa.
Nigeria chini ya madikteta waliokuwa wanajitapa kuleta maendeleo kwa njia ya kuua wapinzani, akina jenerali Sani Abacha ndio waasisi wa mifumo ya ufisadi, uuzwaji wa rasilimali za nchi, mauaji na maovu yote unayoona matunda yake leo. Itawachukua miaka mingi kurudi katika hai ya kiuchumi ya kawaida inayoendana na mifumo ya demokrasia.

Acheni kudanganyika kuwa eti demokrasia inatakiwa ife ndipo tupate maendeleo. Kinachotakiwa ni demokrasia kamilifu inayowapa wananchi uwezo wa kuwapima viongozi na kuwabadili pale inapobidi. Mfano US pamoja na ukuu wao wote, hupata fursa ya kuwapima viongozi kila baada ya miaka miwili (Uchaguzi mkuu, na midterms).

Nakushauri utoke huko gizani ulipo. Njoo kwenye nuru.
 
Buhari ameleta shida zaid kwa naigeria maana alitazamiwa kama atakuja kutatua tatizo LA boko haramu na kuneutralize nchi kati ya Islam na kristus

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda Afrika magharibi ukajionee maisha ya watu utashangaa nchi inayozalisha mafuta mengi, lakini wananchi shida tu, tunataka kiongozi anayesimamia Maendeleo na kulinda mali za umma, hatutaki demokrasia mahali palipo jaa rushwa.
Jibu murua kabisa!,hatutaki demokrasia ya kudumaza maendeleo,tunataka udikiteta wa kutuletea maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom