Kuendekeza matumizi haya ndio mwanzo wa kuharibu lugha na kuwa nyuma ya Wakenya.

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Watanzania tubadilike,tuipende na kuilinda Lugha yetu! Utakuta mtu anaandika "ivi" badala ya hivi,"una ela" badala ya huna hela, "ujui" badala ya hujuwi, nk uharibifu huu (mwingine angeandika "u")wa maneno katika lugha ya kiswahili ("kiswaili") unachefua hasa unapofanywa na Watanzania tena mbaya zaidi wasomi na zaidi vijana!? Huko ("uko") tunapoipeleka lugha yetu Tukufu ni pabaya, tubadilike na tujivunie utamaduni wetu! Na humu humu ("umu umu") Jf watu hao ("ao")wamo halafu ("alafu")wanajiita Ma-great thinker! Aibu na upuuzi mtupu!
 
Umenena. Kuna haya pia - cku (siku), ctaki (sitaki), 7bu (sababu)...

Unajua, mbali na kupotosha lugha, pia namna ya uandishi au uongeaji wa mtu unaakisi tabia yake. Unaweza kuonekana ni mtu usiye makini. Ni vizuri tuepukane na hivi vikosa vidogo vidogo katika lugha.
 
Wengi humu wanajidai ma-great thinker, lakini uandishi wao tu unakufanya ufahamu ni watu wa kukurupuka. Utaanza kuonekana kama ni 'great thinker' hata kwa jinsi unavyoandika chambuzi au mada zako. Lakini ukiboronga kwenye lugha tu, inakuondolea sifa hiyo. Ni wakati sasa wa kufikiri kwa makini kile unachoandika kimekaa kwenye lugha sahihi? Au shule ulikuwa unapelekwa-pelekwa tu?
 
Back
Top Bottom