Kuelewa ujumbe wa Rais Xi kuhusu amani na maendeleo duniani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
NA Morris Ochieng

Uwazi na uaminifu, ushirikishaji na ustawi wa pamoja, na ushirikiano na maendeleo ya amani.

Haya ni mambo makuu matatu ambayo hujitokeza katika hotuba za Rais wa China Xi Jinping wakati wa safari zake za kimataifa.

Mambo hayo huenda kwa pamoja na ni kama nguzo zinazotegemeana.

Mtu hawezi kuwa wazi bila kuwa mwaminifu.

Ili mtu awe na mafanikio ya pamoja, lazima kuwe na umoja.

Na hakuna maendeleo ya amani bila ushirikiano.

Hii ni baadhi ya mikakati ambayo China imeitumia kwa zaidi ya miongo minne kuwaondoa zaidi ya watu milioni 800 kutoka katika umaskini.

China ina utamaduni uliokita mizizi wa kushirikiana na kusaidiana.

Kusaidiana kuna maana kuwa , unapopata maendeleo, hupaswi kuwaacha nyuma ndugu zako au walio karibu nawe.
Huu ndio ustawi wa pamoja ambao Rais Xi amekuwa akiueleza popote aendapo.

Mara tu baada ya kuingia madarakani Machi 2013, Rais Xi alifanya ziara yake ya kwanza akiwa rais mijini Moscow nchini Urusi.

Katika safari hiyo, aliweka wazi msimamo wa China katika masuala ya amani, maendeleo na ushirikiano wenye kunufaishana.

"Ni ulimwengu ambapo amani, maendeleo, ushirikiano na manufaa ya pande zote vimekuwa mtindo wa nyakati…Ni ulimwengu ambapo nchi zimeungana na zinategemeana kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana hapo awali,” alisema Xi na kuongeza,

“Mwanadamu anaishi katika dunia ambayo imekuwa kijiji kwa enzi hizi ambazo historia na ukweli hukutana, maisha ya kijamii kuwaleta watu pamoja.”

Hii inaonyesha juhudi za makusudi za kimkakati za China za kutaka kuimarisha msingi wa kutafuta maendeleo ya amani.

Prof Zhong Xin wa Chuo Kikuu cha Renmin cha China anatoa maoni kwamba kwa sababu ya kuwa kiongozi wa zaidi ya watu bilioni 1.4, Rais Xi, ambaye mtazamo wake umekita mizizi katika utamaduni wa China, anawakilisha dira ya China nzima.

"Hayo ni mawazo na mila zetu. Hivyo yanaweza kupokelewa vyema na watu wa China,” anasema Prof Zhong.

Kila kitu kinakuwa na ufanisi kutokana na uongozi thabiti na maono mazuri na mpangilio unaosaidia watu kufanya kazi ili kufikia malengo, anasema Prof Zhong.

Kituo cha pili katika ziara ya Rais Xi kilikuwa Tanzania, Machi 25.

Afrika ina mambo mengi yanayofanana na China. Ndio maana kuna ushirikiano wa karibu kati ya China na nchi za Afrika.

Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Rais Xi alisema uhusiano kati ya China na Afrika haukujengwa mara moja.

Alisema ni ushirikiano uliojengwa hatua kwa hatua kwa miongo kadhaa ambao umepitia misukosuko mingi.

"Mapitio ya kipindi hiki cha historia yanaonyesha kuwa sifa kuu za uhusiano kati ya China na Afrika ni uaminifu, urafiki, kuheshimiana, usawa, kunufaishana na maendeleo ya pamoja," Xi alisema.

Hii inaeleza uhusiano wa karibu wa China na nchi za Afrika ikiwemo Kenya, anakotoka mwandishi huyu, ambao umechochea maendeleo ya haraka katika miundombinu na maeneo mengine katika nchi za Afrika.

Zaidi ya yote, Rais Xi anathamini amani ya dunia na hii inaweza kupatikana kwa uhusiano wa ushirikiano wa mataifa makubwa kama vile China, Marekani na Urusi, na si uhusiano wa washindani.

Hii inatokana na ukweli kwamba ili maendeleo yaendelee ni lazima kuwe na amani.
 
Back
Top Bottom