GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Najua Watu wengi humu tunatumia usafiri wetu huu wa kawaida wa daladala kwenda katika mizunguko yetu mbalimbali. Ila ikumbukwe kuwa hasa katika jiji letu hili la Dar es Salaam usafiri wa daladala huwa ni wa shida mno na ukipanda na kupata siti basi siku hiyo hutaisahau maishani mwako.
Pamoja na hayo yote kuna jambo linanipa ukakasi na nimeona leo nililete kwenu ili mwenye kujua atupe maarifa zaidi na kama kuna tahadhari basi tuanze kuichukua mapema. Jamani humu katika hizi daladala huwa tunatabia ya kujazana kiasi kwamba mara nyingine ikatokea mmoja wenu kajamba kishikaji hamuwezi kumjua au mtu akiibiwa kwa kupigwa ndole kumjua mwizi ni tatizo na wakati mwingine baadhi yetu hupitishwa kituo unachotaka kushuka.
Leo naomba tu kuwauliza hivi kwa jinsi vile ambavyo huwa tunajazana mpaka pomoni ( nyomi / wengi ) mule ndani ya daladala halafu wengi wetu tunakuwa tumepeana migongo kimuelekeo na hasa hasa makalio ( matako ) yetu mara nyingi yamekuwa yakikutana / yakigusana tena kwa ukaribu wa kutukuka. Je hali hii kiafya haina madhara?
Naomba mwenye kujua hili atusaidie kwani nataka sasa kufunga kila kilokuwa changu nianze safari kwenda kugombania daladala na nijue leo nitagusanisha kalio na abiria gani hasa ukizingatia kuna mvua jijini hivyo usafiri leo utakuwa ni wa shida, tabu na kukomoana.
Naomba kuwasilisha na karibuni tujadili.