Uchaguzi 2020 Kuelekelea Uchaguzi mkuu 2020: Tupe tetesi na maoni yako, unapendekeza nani agombee wapi na nafasi gani?

Atajua mwnyewe, atakula jeuri yake kama kuna mahali anajua hakuabudu alijaribu kusaliti arudi akatubu asamehewe kama kina fulani walivyotubu na sasa ni waabudu wazuri tu. Au vipi dawa ya jeuri ni kiburi arudi kwenye mawe ya barabarani akaandike tena MWIGULU RAIS 2020.
 
Mnambua
Unashangaza kidogo! Umeuliza swali na umelijibu mwenyewe! Sasa yeye atatoa majibu yapi tena. Umesema yuko kijijini na anafanya kazi sana. Hilo ungelifurahia maana yuko karibu na wananchi na anawaonyesha mfano wa "hapa kazi tu" mbali ya kuwa ni mbunge. Pia umesema muda wa kujinadi bado yaani umemtetea mwenyewe! Kwamba kuna wapinzani hilo ni jambo zuri kwa maana inaonesha kuwa kuna demokrasia. Jambo moja umesahau. Mwigulu viwango vyake ni vya urais wa nchi na alionesha kwa vitendo. Unadhani mtu wa jinsi hiyo ataogopa upinzani wa ubunge? Kazi kwako.
 
Huyu ikiwezekana akatwe tu kwenye kura za maoni.
January naye akatwe kwenye kura za maoni.
Nape Nnauye naye akatwe kwenye kura za Maoni.
Mwita Waitara akatwe kwenye kura za maoni.

CCM mpya hii haitaki wapiga porojo bali inataka wapiga kazi chini ya Jemedari Dr JPM.
 
Unashangaza kidogo! Umeuliza swali na umelijibu mwenyewe! Sasa yeye atatoa majibu yapi tena. Umesema yuko kijijini na anafanya kazi sana. Hilo ungelifurahia maana yuko karibu na wananchi na anawaonyesha mfano wa "hapa kazi tu" mbali ya kuwa ni mbunge. Pia umesema muda wa kujinadi bado yaani umemtetea mwenyewe! Kwamba kuna wapinzani hilo ni jambo zuri kwa maana inaonesha kuwa kuna demokrasia. Jambo moja umesahau. Mwigulu viwango vyake ni vya urais wa nchi na alionesha kwa vitendo. Unadhani mtu wa jinsi hiyo ataogopa upinzani wa ubunge? Kazi kwako.
Kumbe atagombea urais?
 
Jimbo la kawe nadhani Mtoto wa Warioba Kippi ni wakati wake wa kujipitisha ili tumpe kura. Huyu Halima kwa kweli arudi akagombee kahe au Same mashariki.

Magamba mkimleta Bashite au John sitta kazi itakuwepo. Ni bora Kippi hana makandokando ya watu wasiojulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani iwe kwenu!!

Tutumie thread hii kupendekeza wale wanaofaa kugombea 2020, Tetesi za watu watakaogombea

Mimi naanza na Dr. Tulia, Huyu dada amekuwa msaada kwetu na jamii ya Wana Mbeya kwa ujumla kwani kawasaidia wakina Mama wengi kupata mikopo yenye riba nafuu na vijana wengi kwenda Shule Mimi na awa wenzangu tumeapa kumpigia kampeni bure kabisa Dr Tulia Ackson Mwansansu kuwa Mbunge wa Mbeya 2020.
Namshauri Esther Matiko atafute kazi nyingine ya kufanya maana pale Bunda Mjini hatakiwi wapiga kura wake wanasema huwa wanamsikia tu kila kukicha yuko Mahakamani tena Dar hata kama kesi si ya kwake lakini yupo Mahakamani
 
Ally kazi yake kwa sasa ni NONO sana hawezi wania Ubunge ambao sasa hauna deal kwa sababu Rais wa TZ ndiye pia muamuzi wa mwisho kuhusu posho za wabunge na akaamua kakata posho kibao za kusafiri.za wabunge.
Wabunge wana tengeneza pesa kwa safari lkn sasa hazipo!!
hivi bado yuko kwenye makampuni ya simu..? kama huko si haba
 
Je, Professor Adolf Mkenda, ana andaliwa kugombea ubunge wa Rombo 2020?

Na baadae kuteuliwa kuwa waziri?



Je, Mwanri, ana andaliwa kugombea ubunge wa Siha 2020?

Na baadae kuteuliwa kuwa waziri?
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Sifa kuu 3 zinambeba vilivyo Mwamba wa Afrika na jabari wa mageuzi ya kiuchumi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mpaka kufikia hatua Watanzania kuamua mwaka 2020 aendelee kutuongoza.

*A: UADILIFU*

Rais Magufuli amesimamia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo wanaotuhumiwa kwa ufisadi Papa na ulaji rushwa wamepandishwa Mahakamani

Pia ameimarisha uwajibikaji, uadilifu na uchapa kazi kwa Watumishi wa umma nchini na kusimama kidete kufufua Mashirika ya umma yaliyokuwa taabani. Mfano shirika la ndege, shirika la simu.

Halikadhalika amefanya uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya kwenye sekta ya madini.

Rais Magufuli amedhibiti madawa ya kulevya na ujangili wa Tembo na Faru ambapo wameongezeka kuashiria kupungua kwa biashara ya nyara za Serikali.

Kwenye upande wa masuala ya kidiplomasia ameimarisha mahusiano mazuri na nchi jirani.

Haijawahi kutokea kwani Rais Magufuli ameweka uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za Taifa.

*B: UZALENDO*

Baada ya Mwalimu Nyerere anayefuatia ni Rais Magufuli kutoa Elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari ambapo Serikali hutumia Tsh. Bilioni 23 kila mwezi kulipia elimu bure.

Uonevu, ubabe, ubaguzi umepungua na ni sahihi kusema Rais Magufuli amepunguza uwepo wa matabaka ndani ya jamii.

Ni wazo la Mwalimu Nyerere lakini Rais Magufuli amekuja kulitekeleza la ujenzi wa mradi mkubwa wa Mto Rufiji wa kuzalisha umeme zaidi ya Megawatts 2115.

Rais Magufuli amefanikiwa kudhibiti matumizi ya hovyo ya fedha na fedha kuelekezwa zaidi kwenye miradi ya kimaendeleo.

Pia Rais Magufuli yupo imara na amesimamia ukusanyaji na matumizi sahihi ya kodi. Makusanyo yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 800 hadi kufikia Tsh. Trilioni 1.9 kwa kila mwezi.

Waliojipenyeza kwenye ajira Serikalini bila ya sifa amewaondoa. Hivyo JPM amefanikiwa kudhibiti vyeti feki na mishahara hewa na kubaki historia nchini.

Leo hii Watanzania tunajivunia nchi yetu, viongozi wetu, rasilimali zetu na utaifa wetu. Hivyo JPM Ameimarisha UZALENDO nchini.

Hakuishia hapo amerudisha mashamba na viwanda vilivyobinafsishwa na havikuendelezwa.

Leo Taifa linanufaika na madini kwani amedhibiti usafirishwaji wa makinikia na hayaendi kuchenjuliwa tena nje na madini yanauzwa hapa hapa nchini kupitia masoko ya madini yaliyoanzisha maeneo mbalimbali yenye madini. Huu ni uzalendo wa kuigwa wenye tija vizazi na vizazi.

*C: UCHAPA KAZI*

Leo hii Serikali imehamia Dodoma na mpaka Rais Magufuli nae pia amehamia Dodoma. Walisema haiwezekani lakini nia ya dhati na uchapa kazi wa Rais Magufuli na Serikali yake imedhihirisha inawezekana.

Baada ya reli ya Mkoloni yenye zaidi ya miaka 120, leo hii Rais Magufuli ameanzisha Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme ya SGR ambayo ni reli ya kisasa, yenye kasi na inayobeba mizigo mingi.

Sera ya Tanzania ya viwanda ipo kivitendo. Leo hii kuna ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000.

Rais Magufuli aliapa kuilinda katiba ya nchi ambapo kuna uimarishwaji wa amani na Uhuru wa kidemokrasia ndani ya nchi. Mathalani Umoja wa Mataifa (UN) umempongeza Rais Magufuli kudumisha amani na usalama ndani na nje ya nchi.

JPM amesimamia vyema ukuaji wa uchumi uliokuwa na kufikia 7.1%

Kwenye afya napo pamenoga kuna ujenzi wa vituo vya afya kila kata na ujenzi wa Zahanati kila kijiji.

Serikali ya Rais Magufuli imedhibiti maandamano ya kisiasa na ya kijamii (Mf. Wanafunzi, Madaktari) na sasa yamebaki historia.

JPM amenunua ndege mpya 8 za kisasa na Leo hii ATCL imefufuka inachanja anga za kitaifa na kimataifa.

Ameweka mikakati mizito ya kupunguza foleni kwa Ujenzi wa flyover ya Tazara na interchange ya Ubungo.

*Na Shilatu E.J*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua nini bloo, umeandika sana yaani. Umeandika hadi visivyokuwepo yaani mwamba dah!

Una uhakika mh amedhibiti vyeti feki vyote?
Una uhakika makusanyo ya TRA yamefika 1.9T kwa moon?
Matembo yameongezeka mangapi mkuu chini ya utawala huu?
Dah, mwamba, lini UN walimpongeza Mh?
Mkuu una uhakika chuma kimehamia Dom sasa hivi?

Mengine labda
 
Mleta mada Rekebisha sema kwanini wewe unamchagua sio watanzania, talk about your fu ck en self
 
Back
Top Bottom