Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,440
- 113,449
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa.
Niko huku mkoani Mbeya kwenye Nane Nane, tangu nimefika huku, nimekutana na baridi fulani ya ajabu! haswa nyakati za usiku na alfajiri, hata utumie blangeti la chapa nini, au chapa nani, baridi linapenya!. Nikajiuliza hivi nchi wenye winter wanaishije?!. Hivyo tangu nimefika huku Mbeya, hata ulalie kushingilia mchele wa Kyela na maharahe ya Mbeya!, hakuna cha maharage ya Mbeya wala Mchele wa Kyela, kila alfajiri, usingizi unakata na kibaridi, hivyo nakuwa sina jinsi, bali kushika simu yangu na kuperusi mitandao.
Ile kushuka tuu JF, ndio nakutana na bandiko hili la Mkuu Lusungu UTEUZI: Rais Samia ateua Majaji wa Mahakama Kuu lenye mkeka mpya wa majaji
Hizi time za hii mikeka kutoka!. Hawa watu wanalala saa ngapi?!. NB, kwa nile kuna mtu aliishawahi kutanka kuwa yeye na mtu fulani wanafanana kwa uchapakazi, na kuna mchapakazi alikuwa anachapa kazi round the clock na kupelekea kuingia na mafaili hadi room!, tusiruhusu uchapakazi wa hivi kwa mtu wetu!, tutamchosha!. Kazi yes tuchape kazi, ila muda wa mambo mengine, ikiwemo muda wa kupumzika, lazima apumzike!, hata ikitokea mtu wetu hana usingizi, then aangalie hata katuni, lakini sio kwa uchapakazi huu!.
Hongera zao kwa wateuliwa, ila hongera sana kwa mteuzi, kumbe uswa wa kinsia unawezekana kabisa!, katika teuzi hizi mpya za majaji wapya 22, majiji 11 wana majina ya kiashiria cha Kike!.
Huko nyuma nilipouliza swali hili, Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?, watu humu walibeza kuwa Tanzania hatuna!, hata nilipopandisha bandiko hili, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” bado watu bado walipinga hadi pale Mungu alipo fanya kudra zake na hili likawezekana!.
Tena sisi binadamu, tunatabia ya kukana tabia mbaya zetu ili tuu tuonekane wema mbele ya watu!, mimi ni mtu wa kutoka Kanda ya Ziwa, miongoni mwa maeneo ambayo mfumo dume umegangamala, ni Kanda ya Ziwa, hivyo enzi za Blaza, tuliwa kushauri hivi Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa!. Kitu kingine kibaya mimi niliwahi kukishauri ni tufute wabunge wa viti maalum nikiwaitani wabunge wa kubebwa!, Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?
Hivyo huu uteuzi wa 50/50 wa majaji, unathibitisha hili 50/50 ya wanawake kwenye sekta zote, linawezekana!.
Swali ni, ili kuonyeshea kuwa hili linawezekana, Tanzania inao wanawake wenye sifa na vigezo vya kukidhi hoja ya 50/50 kila mahali, jee mnaonaje tukiutumia uchaguzi mkuu wa 2025 kuonyeshea kuwa hili linawezekana?, na likiwezekana kweli, jee kutakuwa bado na haja ya kuendelea kuwa na viti maalum?. vitakuwa ni vya nini?, si tuvifute tuu?.
Paskali.

Mkuu Lusungo , kwanza asante sana kwa taarifa hii, ila kwa vile mimi ni mtu wa media, natatizwa sana na hii mikeka inayotoka time hizi!. Huwa najiuliza kama huu mkeka umetoka time hizi, hawa watu huwa wanalala saa ngapi?!.Habari za usiku huu, mtakapoamka pokeeni taarifa hii maana mteuaji halali wala hasinzii...
Orodha hii chini ni ya majaji wateule. Hongera nyingi kwao.View attachment 2315715View attachment 2315716View attachment 2315717