Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi: WanaJF tushiriki kutengeneza ilani, sera na vipaumbele. Nini maoni yako? Tupaze sauti, Tanzania ni yetu sote

Mkuu 'Ndio walewale',

Kwa sasa hivi, hakuna sera wala kitu kingine chochote kinachozidi mahitaji ya KELELE kuhusu kuwepo uchaguzi ulio "Huru na Haki."

Hizo sera na mahitaji mengine, kwa kweli ni anasa tu kwa sasa.

Kwa hiyo himiza watu kwenye mada yako hii, kuhusu hilo la kuwepo uchaguzi 'HURU na wa HAKI'.

Kura ya kila atakayekwenda kupiga kura ihesabike na viongozi watakaochaguliwa ndio hao hao tutakaowahimiza wabuni sera zitakazokuwa na manufaa kwa nchi yetu.

Ni kazi bure kwa sasa hivi kupoteza mda na kuhangaika na sera ambazo hao watakaoingia kwa kutumia mabavu watakuwa hawana ridhaa ya wananchi kuzitimiza sera hizo.

Kwanza watakuwa hawana habari kabisa na nyinyi, kwa vile kura zenu hazikuwa na maana ya wao kuwepo kwenye madaraka.
 
Chama che ye sera nzuri ni chadena, wanafuata ccm na kisha act

Lakini watekelezaji wa sera zote hizi ni ccm.kwa sababu bado wanatukia dola kubaki madarakani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana.

Kama wewe unaona hivyo, basi mada nzima haina maana.

Mkuu una maana gani ? Yaani tuweke kando mambo mengine yote hadi tutakapopata tume huru kisha ndio tuanze na mengine ?

Tunaweza kuwa wote tunaitaka tume huru lakini kwa hii staili yako ya kufanya mambo naamini utakua unatania.

Hii ni nchi mkuu, ina mambo mengi sana. Kama tunaweza kufanya mambo mia sita kwa wakati mmoja basi tunatakiwa tuyafanye.
Binafsi nimeshangaa kwanini unasema uzi huu unakosa mashiko kama hautakuja baada ya kupatikana kwa tume huru, lakini nimeyaheshimu mawazo yako.
 
Mkuu kwamba hilo ongezeko la 1% ya VAT iwe ni makato ya bima kwa ajili ya wananchi wote. Yaani wewe ili mradi tu ni mtanzania unakua huna wasiwasi juu ya matibabu maana by default unakua na bima. Kwa maneno mengine hii tunaweza kusema ni MATIBABU BURE KWA WOTE. Nimeyapenda sana mawazo yako mkuu. Ahsante
Matibabu ya bure huku watu wanakatwa kodi???
 
Ila ya CCM itamke wazi kuwa ata wananchi wakitunyima kura hamna shida maana dola itatulinda tu.
 
Matibabu ya bure huku watu wanakatwa kodi???

Duniani kukatwa kodi hakuepukiki mkuu. Nimejaribu tu kuifananisha hali ya kuwa na bima ya afya kwa wananchi wote kuwa sawa na 'matibabu bure'.
Bima ya afya kwa wote kwa sasa haipo, kodi tunakatwa. Bima ya afya kwa wote ikiwepo, kodi tutaendelea kukatwa.

Lengo la msingi la mchangiaji lilikua ni kuweka huo utaratibu ukizingatia umuhimu wa suala la afya ya mtu. Tunaweza tusikubaliane ni wapi hela ya kugharamia hizo bima zitoke wapi, lakini naamini wote tunakubaliana kwamba afya ya mtu ni kipaumbele na bima kwa wote ni hatua muhimu mno katika kuhakikisha watu wanapata uhakika wa matibabu.
 
Mkuu 'Ndio walewale',

Kwa sasa hivi, hakuna sera wala kitu kingine chochote kinachozidi mahitaji ya KELELE kuhusu kuwepo uchaguzi ulio "Huru na Haki."

Hizo sera na mahitaji mengine, kwa kweli ni anasa tu kwa sasa.

Kwa hiyo himiza watu kwenye mada yako hii, kuhusu hilo la kuwepo uchaguzi 'HURU na wa HAKI'.

Kura ya kila atakayekwenda kupiga kura ihesabike na viongozi watakaochaguliwa ndio hao hao tutakaowahimiza wabuni sera zitakazokuwa na manufaa kwa nchi yetu.

Ni kazi bure kwa sasa hivi kupoteza mda na kuhangaika na sera ambazo hao watakaoingia kwa kutumia mabavu watakuwa hawana ridhaa ya wananchi kuzitimiza sera hizo.

Kwanza watakuwa hawana habari kabisa na nyinyi, kwa vile kura zenu hazikuwa na maana ya wao kuwepo kwenye madaraka.

Kuna demokrasia na kuna maendeleo. Hivi vitu vyote ni muhimu sana katika taifa. Hakina kimoja kilicho muhimu kuliko kingine, hakuna kimoja ambacho ni mbadala wa kingine.
Hatuwezi kutopendekeza sera bora za maendeleo, vipaumbele na mikakati kwa sababu hakuna tume huru. Lakini pia hatuwezi kuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu tumetaka ''demokrasia ya kweli''.

Kuna nyuzi nyingi sana humu zinazozungumzia hali ya kisiasa nchini kuelekea uchaguzi na mambo kadhaa yahusuyo tume ya uchaguzi, hapa naomba tuendelee na kupendekeza kama mada inavyojieleza. Amini nakwambia, hatufanyi kazi bure hapa.
 
Mimi ningependelea sera ya Open govt iimarishwe na tupate 1& 1 online intrview na Kiongozi yoyote haswa waziri wa kilimo, Mambo ya ndani, Sheria tuwape maoni yetu na maswali na wayajibu kadri wapendezavyo hapa JF.

Ningependa pia Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Ndugu Kayombo uje tukuweke kitimoto kuhusu TRA hapa online. Ikiwa Balozi wa Uingereza anatambua mchango wa Jamiiforum wewe mswahili wa kawaida ni kwanini usielewe hii ni God given platform ya kukusaidia kuelimisha wananchi wako wakuelewe.

Wahusika kutoka Nssf, Bima ya Afya, Tarura, Tasac mje hapa tuwalige maswali yatawasaidia utendaji wenu wa kazi. Ikibidi hata PR wa sheria na katiba aje ajibu hoja zetu.

Inakuwa kama kipindi fulani Aljazeera cha The stream. Haina kufeli unalizwa watu wanaelewa na wananchi wakielewa tutapunguza kazi na rushwa pia.

Mkuu Paskali jiongeze hapa utengeneze Kitimoto ya online hata App ya Q & A halafu watu wanasubscribe.
Mimi namuomba mkuu Rais Magufuli kuanza kuona JF sio adui wa serikali bali Rafiki, yanayosemwa humu japo sometimes ni kwa lugha ya ukali but still yana lengo la kuijenga Tanzania yetu...sote lengo ni moja kuiona nchi yetu mama Tanzania inasonga mbele..hivyo basi serikali itengeneze urafiki na JF..naamini kufanya hivi kutasaidia sana nchi yetu..JF imekua hewani for more than ten years,watu humu ukiamua kuchunguza michango yao utabaini kuwa mambo mengi sana mazuri yamesemwa ila tuna serikali ambazo sio sikivu,serikali ingeweza kushusha pride chini na ku engage wananchi WOTE ..hata sisi wa online tunaweza kuwa engaged kwa kufanya tunayoshauri humu...nakuomba Magufuli uliangalie hili kama unaipenda nchi yetu Tanzania, kwa kuanza anza na ..skeleton out of closet...mawaziri na staffs wao...wapewe challenge ya kuja na ideas mpya kutoka JAMII FORUMS kila mwezi….LOL...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duniani kukatwa kodi hakuepukiki mkuu. Nimejaribu tu kuifananisha hali ya kuwa na bima ya afya kwa wananchi wote kuwa sawa na 'matibabu bure'.
Bima ya afya kwa wote kwa sasa haipo, kodi tunakatwa. Bima ya afya kwa wote ikiwepo, kodi tutaendelea kukatwa.

Lengo la msingi la mchangiaji lilikua ni kuweka huo utaratibu ukizingatia umuhimu wa suala la afya ya mtu. Tunaweza tusikubaliane ni wapi hela ya kugharamia hizo bima zitoke wapi, lakini naamini wote tunakubaliana kwamba afya ya mtu ni kipaumbele na bima kwa wote ni hatua muhimu mno katika kuhakikisha watu wanapata uhakika wa matibabu.
Sawa mkuu lakini ili neno bure unalitumia vibaya sana...Hakuna kitu cha bure ...apo ni kutumia kodi zetu kugharamia afya za watu ambacho ni kitu kizuri kwakua watu wengi hawana kipato kizuri..ingawa kila kukicha mwenyekiti anasema pesa zipo
 
Mimi ningependelea sera ya Open govt iimarishwe na tupate 1& 1 online intrview na Kiongozi yoyote haswa waziri wa kilimo, Mambo ya ndani, Sheria tuwape maoni yetu na maswali na wayajibu kadri wapendezavyo hapa JF.

Ningependa pia Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Ndugu Kayombo uje tukuweke kitimoto kuhusu TRA hapa online. Ikiwa Balozi wa Uingereza anatambua mchango wa Jamiiforum wewe mswahili wa kawaida ni kwanini usielewe hii ni God given platform ya kukusaidia kuelimisha wananchi wako wakuelewe.

Wahusika kutoka Nssf, Bima ya Afya, Tarura, Tasac mje hapa tuwalige maswali yatawasaidia utendaji wenu wa kazi. Ikibidi hata PR wa sheria na katiba aje ajibu hoja zetu.

Inakuwa kama kipindi fulani Aljazeera cha The stream. Haina kufeli unalizwa watu wanaelewa na wananchi wakielewa tutapunguza kazi na rushwa pia.

Mkuu Paskali jiongeze hapa utengeneze Kitimoto ya online hata App ya Q & A halafu watu wanasubscribe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Haya yamfikie Pascal Mayalla Maxence Melo Paw
 
Mkuu una maana gani ? Yaani tuweke kando mambo mengine yote hadi tutakapopata tume huru kisha ndio tuanze na mengine ?

Tunaweza kuwa wote tunaitaka tume huru lakini kwa hii staili yako ya kufanya mambo naamini utakua unatania.

Hii ni nchi mkuu, ina mambo mengi sana. Kama tunaweza kufanya mambo mia sita kwa wakati mmoja basi tunatakiwa tuyafanye.
Binafsi nimeshangaa kwanini unasema uzi huu unakosa mashiko kama hautakuja baada ya kupatikana kwa tume huru, lakini nimeyaheshimu mawazo yako.
Ingekuwa ni kama hivi unavyoamini, isingekuwa lazima hata kidogo kuwaondoa wakoloni. Tungewahimiza tu kutekeleza sera nzuri tunazowapendekezea wazitekeleze, basi ingetosha.

Mkuu, kuna kasoro kubwa katika dhana yako.
 
Kuna demokrasia na kuna maendeleo. Hivi vitu vyote ni muhimu sana katika taifa. Hakina kimoja kilicho muhimu kuliko kingine, hakuna kimoja ambacho ni mbadala wa kingine.
Hatuwezi kutopendekeza sera bora za maendeleo, vipaumbele na mikakati kwa sababu hakuna tume huru. Lakini pia hatuwezi kuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu tumetaka ''demokrasia ya kweli''.

Kuna nyuzi nyingi sana humu zinazozungumzia hali ya kisiasa nchini kuelekea uchaguzi na mambo kadhaa yahusuyo tume ya uchaguzi, hapa naomba tuendelee na kupendekeza kama mada inavyojieleza. Amini nakwambia, hatufanyi kazi bure hapa.
Mkuu, hapa tunapishana sana kimtizamo.
Mimi nakataa katakata uniletee maendeleo huku ukininyanyasa na kuninyima haki yangu. Nakataa kabisa.

Wewe unakubali unyanyaswe na unyimwe haki yako mradi umeletewa maendeleo.

Historia inayo mifano mingi, ya nchi/watu kuweka maisha yao kutafuta heshima, utu na haki zao.
Sijapata kusikia watu/nchi zinakubali kukandamizwa ili zipate maendeleo.
 
Serikali ipitie upya sera ya elimu na kufanya marekebisho kulingana na uhitaji wa soko la sasa.

Pia, izingatie kuvipa uwezo vyuo vya kati hasa vya ufundi. Sidhani kama kwa sasa haja ya kuwa na utitiri wa university graduates bila pa kuwapeleka na kuwa na elimu isiyokidhi soko la kimataifa. Serikali ikiweza nguvu vyuo vya kati hasa vya fundi itajenga kizazi cha vijana wenye uwezo wa kujiajiri na nchi itasonga mbele kiuchumi na kuwa na fursa ya kukuza technolojia.

Vyuo vikuu viwe na idadi ya wastani ya udahili wa wanafunzi, fani zenye uhitaji mkubwa wa shahada ya kwanza ndio zipewe vipaumbele.
Pia, uwepo mkakati mahususi wa kuendeleza na kukuza utalii kwa kuboresha huduma zinazotolewa kwa watalii ili kuendana sawa na thamani ya pesa inayolipwa na mteja. Mweka walikuwa na mpango wa kuanzisha program ya kuwapiga brush tourism service providers hasa tour guides sasa sijui uliiishia wapi.
 
Mkuu, hapa tunapishana sana kimtizamo.
Mimi nakataa katakata uniletee maendeleo huku ukininyanyasa na kuninyima haki yangu. Nakataa kabisa.

Wewe unakubali unyanyaswe na unyimwe haki yako mradi umeletewa maendeleo.

Historia inayo mifano mingi, ya nchi/watu kuweka maisha yao kutafuta heshima, utu na haki zao.
Sijapata kusikia watu/nchi zinakubali kukandamizwa ili zipate maendeleo.

Labda hauelewi maana ya neno SANJARI mkuu.
Sanjari maana yake ni sambamba, kwa wakati mmoja au kwa mpigo. Kwa kiingereza wanasema simultaneously, concurrently, at the same time.

1. Wewe unasema tuachane na maendeleo kwanza tupate demokrasia ya kweli.
2. Mimi nasema maendeleo yanatakiwa kwenda pamoja (sanjari) na demokrasia.
3. Wewe unanisingizia mimi kwamba nasema tusitishe masuala ya kidemokrasia tufanye ya maendeleo.

NB: Kuna nyuzi nyingi sana humu JF zinazozungumzia tume ya uchaguzi, uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, uhuru wa kisiasa n.k, nadhani si vibaya tukiwaacha watu pia wachangie mambo ya maendeleo kupitia uzi huu maana kwa kufanya hivyo hawazuii mapambano ya demokrasia ya kweli kama unavyodai hapo juu.

#Naheshimu sana mawazo yako
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom