KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Mkuu 'Ndio walewale',
Kwa sasa hivi, hakuna sera wala kitu kingine chochote kinachozidi mahitaji ya KELELE kuhusu kuwepo uchaguzi ulio "Huru na Haki."
Hizo sera na mahitaji mengine, kwa kweli ni anasa tu kwa sasa.
Kwa hiyo himiza watu kwenye mada yako hii, kuhusu hilo la kuwepo uchaguzi 'HURU na wa HAKI'.
Kura ya kila atakayekwenda kupiga kura ihesabike na viongozi watakaochaguliwa ndio hao hao tutakaowahimiza wabuni sera zitakazokuwa na manufaa kwa nchi yetu.
Ni kazi bure kwa sasa hivi kupoteza mda na kuhangaika na sera ambazo hao watakaoingia kwa kutumia mabavu watakuwa hawana ridhaa ya wananchi kuzitimiza sera hizo.
Kwanza watakuwa hawana habari kabisa na nyinyi, kwa vile kura zenu hazikuwa na maana ya wao kuwepo kwenye madaraka.