Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi: WanaJF tushiriki kutengeneza ilani, sera na vipaumbele. Nini maoni yako? Tupaze sauti, Tanzania ni yetu sote

Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,896
4,495
Tanzania ni nchi yetu sote kwa umoja wetu sisi kama watanzania, nchi hii itajengwa na kuendelezwa na watanzania wote bila kujali tofauti zetu.

Linapokuja suala la kuijenga nchi, tofauti zetu za kisiasa, kidini, kiitikadi, kiuchumi n.k zinapaswa kuwekwa pembeni. Taifa hili linahitaji mchango wa kila mmoja wa raia wake ili kuendelea. Maendeleo ni majumuisho ya juhudi za wananchi, mipango mizuri, utekelezaji pamoja na usimamizi wa rasilimali mbalimbali katika nchi husika.

Hivyo basi haijalishi wewe ni nani, una wadhifa gani au unafanya nini, kwa nafasi yako na kwa namna fulani una mchango katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Kwa kuwa Jamiiforums ni miongoni mwa mitandao ya kijamii inayoheshimika na pengine ndio kinara nchini kwa hoja na mijadala iliyoshiba na yenye tija, pia inajumuisha viongozi, wasomi, wanasiasa, watunga sera n.k, naomba tuutumie uzi huu kutoa maoni yetu kuelekea uchaguzi mkuu 2020. Maoni hayo yalenge sera na vipaumbele vinavyopaswa kujumuishwa kwenye ilani za vyama mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu ili viwe ndivyo vipaumbele vyetu kama taifa.

Chama chochote kitaruhusiwa kuchota (kudesa) mawazo kutoka katika uzi huu, na ninaamini sisi kama wanaJF tuna mawazo mengi sana ya kujenga na yatawafikia wahusika wote. Karibuni sana wadau tutiririke….
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Chana kiasi Hokies na sera nzuri ni ccm tu Jawas Audie ila wamesajili Makatibu Waikiki wa zamani wa chadema
 
Vyama vya siasa viwekeze kwenye afya za wananchi. Bima ya afya iwe ni haki ya msingi kwa kila mwananchi kwa gharama nafuu na ijumuishe tiba kwa magonjwa yote na kipindi chote mgonjwa anapopata huduma ikiwa ni pamoja na kulazwa. Nashauri VAT iwe 19% ili hiyo 1% iingie kwenye mfuko wa bima!
 
Chana kiasi Hokies na sera nzuri ni ccm tu Jawas Audie ila wamesajili Makatibu Waikiki wa zamani wa chadema
Mkuu nadhani prediction ya keyboard ya simu yako imekuhujumu. Hatujapata vilivyo ulichokikusudia.
 
Vyama vya siasa viwekeze kwenye afya za wananchi. Bima ya afya iwe ni haki ya msingi kwa kila mwananchi kwa gharama nafuu na ijumuishe tiba kwa magonjwa yote na kipindi chote mgonjwa anapopata huduma ikiwa ni pamoja na kulazwa. Nashauri VAT iwe 19% ili hiyo 1% iingie kwenye mfuko wa bima!

Mkuu kwamba hilo ongezeko la 1% ya VAT iwe ni makato ya bima kwa ajili ya wananchi wote. Yaani wewe ili mradi tu ni mtanzania unakua huna wasiwasi juu ya matibabu maana by default unakua na bima. Kwa maneno mengine hii tunaweza kusema ni MATIBABU BURE KWA WOTE. Nimeyapenda sana mawazo yako mkuu. Ahsante
 
Hoja mujarabu hii yafuatayo ni lazima yawe kipaumbele kwa chama tawala maana naaamini CCM itashinda 2020.

1.Urasimu kwenye utoaji wa huduma ufutwe kabisa kuwe na controls na uwazi ili wananchi wasipate shida sehemu kama Ardhi, Police, mahakamani, Hospitalini,Tanesco, Maji, uhamiaji, Nemc n.k ikiwezekana kuwe na elimu kwa umma kuhusu upatikanaji wa huduma fulani. Mfano Mtu anataka kufunga mita mpya anaenda Tanesco anaambiwa lete kitambulisho, barua serikali ya mtaa, kiapo cha mahamani hili kama tunahitaji wananchi wakue kwenda uchumi wa kati halitakiwi liwepo dunia ya leo. Kitambulisho cha nida kinatosha sana kumtambukisha na sio kumzungusha mtu na kumpotezea muda.

2. Ajira hili suala linahitajika sana na lipatiwe ufumbuzi au kupunguzwa. Ajira zilizopo hazitoshi na sekta binafsi inasinyaaa sana nadhani masuala ya kodi yameimarishwa sana kiasi kwamba wafanyabiashara hawapumui. Lakini kubwa ni kuminywa kwa mzunguko wa fedha benki binafsi na hata ufungwaji wa maduka ya kubadilishia fedha kigeni.

3. Afya lazima kuwe na kitu kama obama care bima ya afya kwa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sera za kwenye uchaguzi (kila baada ya miaka 5 inakuja sera mpya) ni Rushwa ya kutaka kuchaguliwa hazitoweza kuboresha uchumi wa Taifa. Tunataka mipango ya Kitaifa ya muda mrefu na inayoelewaka na kuwekwa wazi kwa kila mtanzania.
 
Na ndio maana uzi huu una lengo la kukusanya mahitaji ya wananchi ili yatumike kutengeneza sera bora kwa maendeleo ya taifa zima. Karibu sana mkuu kama una lolote, taifa hili litajengwa na wote.
 
Hoja mujarabu hii yafuatayo ni lazima yawe kipaumbele kwa chama tawala maana naaamini CCM itashinda 2020.

1.Urasimu kwenye utoaji wa huduma ufutwe kabisa kuwe na controls na uwazi ili wananchi wasipate shida sehemu kama Ardhi, Police, mahakamani, Hospitalini,Tanesco, Maji, uhamiaji, Nemc n.k ikiwezekana kuwe na elimu kwa umma kuhusu upatikanaji wa huduma fulani. Mfano Mtu anataka kufunga mita mpya anaenda Tanesco anaambiwa lete kitambulisho, barua serikali ya mtaa, kiapo cha mahamani hili kama tunahitaji wananchi wakue kwenda uchumi wa kati halitakiwi liwepo dunia ya leo. Kitambulisho cha nida kinatosha sana kumtambukisha na sio kumzungusha mtu na kumpotezea muda.

2. Ajira hili suala linahitajika sana na lipatiwe ufumbuzi au kupunguzwa. Ajira zilizopo hazitoshi na sekta binafsi inasinyaaa sana nadhani masuala ya kodi yameimarishwa sana kiasi kwamba wafanyabiashara hawapumui. Lakini kubwa ni kuminywa kwa mzunguko wa fedha benki binafsi na hata ufungwaji wa maduka ya kubadilishia fedha kigeni.

3. Afya lazima kuwe na kitu kama obama care bima ya afya kwa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo kwenye namba moja hapo kwa kweli hata mimi natilia mkazo, huduma za serikali kwa wananchi zirahishishwe zaidi na kuwa rafiki kwa mtumiaji. Uhamiaji, Uhamiaji, Uhamiaji....
 
HAYO BADAE TUTAYAJADILI KWA SASA TUME HURU YA UCHAGUZI NDO TUNAWAZA
 
Tuna tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira haswa kwenye ukusanyaji wa takataka, utupwaji na matumizi endelevu ya takataka na uhifadhi.

Sasa hivi fukwe za bahari kuanzia msasani mpaka ununio zimejaa takataka zinazotupwa ovyo na wananchi miferejini na mitoni.

Halmashauri ya jiji imeshindwa kabisa kuchagua wazabuni wenye uwezo,akili na Ari ya kuzoa takataka mitaani. Mvua ikinyesha Dampo la pugu, au Bunju burumawe hayaendeki na hii hupelekea takataka mitaani zisizolewe kwa wakati na kuoza na kuchagua mazingira Hali kadhalika kusambazwa mitaani na watu au hata kunguru.

Hili la takataka lingetiliwa mkazo lingetoa ajira nyingi kwa recycling. Wapi watengeneza Mkaa mbadala wachache wanarecycle taka lakini haitoshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi namuomba mkuu Rais Magufuli kuanza kuona JF sio adui wa serikali bali Rafiki, yanayosemwa humu japo sometimes ni kwa lugha ya ukali but still yana lengo la kuijenga Tanzania yetu...sote lengo ni moja kuiona nchi yetu mama Tanzania inasonga mbele..hivyo basi serikali itengeneze urafiki na JF..naamini kufanya hivi kutasaidia sana nchi yetu..JF imekua hewani for more than ten years,watu humu ukiamua kuchunguza michango yao utabaini kuwa mambo mengi sana mazuri yamesemwa ila tuna serikali ambazo sio sikivu,serikali ingeweza kushusha pride chini na ku engage wananchi WOTE ..hata sisi wa online tunaweza kuwa engaged kwa kufanya tunayoshauri humu...nakuomba Magufuli uliangalie hili kama unaipenda nchi yetu Tanzania, kwa kuanza anza na ..skeleton out of closet...mawaziri na staffs wao...wapewe challenge ya kuja na ideas mpya kutoka JAMII FORUMS kila mwezi….LOL...
 
suala LA elimu liwe ni suala la serilari kuu katika kujenga miundombinu ya elimu kama shule na vifaa vya kujinfunzia......serikali ihakikishe hakuna mwananchi atachangishwa pesa kwa ajili ya ujenzi was madarasa.... kama ilivyo tanroad awepo wakala wa ujenzi wa shule za umma....
 
Back
Top Bottom