Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,896
- 4,495
Tanzania ni nchi yetu sote kwa umoja wetu sisi kama watanzania, nchi hii itajengwa na kuendelezwa na watanzania wote bila kujali tofauti zetu.
Linapokuja suala la kuijenga nchi, tofauti zetu za kisiasa, kidini, kiitikadi, kiuchumi n.k zinapaswa kuwekwa pembeni. Taifa hili linahitaji mchango wa kila mmoja wa raia wake ili kuendelea. Maendeleo ni majumuisho ya juhudi za wananchi, mipango mizuri, utekelezaji pamoja na usimamizi wa rasilimali mbalimbali katika nchi husika.
Hivyo basi haijalishi wewe ni nani, una wadhifa gani au unafanya nini, kwa nafasi yako na kwa namna fulani una mchango katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Kwa kuwa Jamiiforums ni miongoni mwa mitandao ya kijamii inayoheshimika na pengine ndio kinara nchini kwa hoja na mijadala iliyoshiba na yenye tija, pia inajumuisha viongozi, wasomi, wanasiasa, watunga sera n.k, naomba tuutumie uzi huu kutoa maoni yetu kuelekea uchaguzi mkuu 2020. Maoni hayo yalenge sera na vipaumbele vinavyopaswa kujumuishwa kwenye ilani za vyama mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu ili viwe ndivyo vipaumbele vyetu kama taifa.
Chama chochote kitaruhusiwa kuchota (kudesa) mawazo kutoka katika uzi huu, na ninaamini sisi kama wanaJF tuna mawazo mengi sana ya kujenga na yatawafikia wahusika wote. Karibuni sana wadau tutiririke….