Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, upinzani umejiandaje?

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,648
Majigambo na kushutumiana kwa viongozi wa vyama kwa vyama au ndani ya vyama kunaanza kujitokeza, Taifa linapoelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020.

Zitto ameanza kwa kauli nzito kana kwamba ana uhakika wa ushindi kwa sababu tu Seif Maalim kajiunga naye na kundi la wafuasi wake. Kwenye "Tweeter" yake ameandika:

Naona jitihada za watawala kwa kutumia vibaraka wao kupanda mbegu za kutoaminiana kati ya @ACTwazalendo na @ChademaMedia kuelekea 2020. Viongozi, wanachama na wananchi wanaotaka mabadiliko tuwe macho. Tuuimarishe UMOJA tuliouanzisha. #HATUCHOKOZEKI fuatilia kadi #2 ! Mtashangaa

Kilichoamsha shauku yangu kuweka bandiko hili ni kuwauliza mabingwa wa kuchambua masuala ya kisiasa:
Je, Agenda kuu ya vyama vya upinzani ni nini, kuekelea Chaguzi za Kitaifa?

Ukiwasikia vuongozi wa upinzani dai lao kuu ni demokrasia. Si viongozi wa CHADEMA au ACT Mzalendo wenye hoja tofauti. Je, ni kweli Tanzania hakuna demokrasia? Au wana maana demokrasia ya wao viongozi kupanda majukwaani wakiamini kufanya hivyo kunawaongezea wafuasi na wanachama!

Hakuna shaka wanasiasa wanahitaji majukwaa ya mikutano ili kujijenga kisiasa, kupata umaarufu na hatimaye kushawishi wapiga kura kuaminiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli alishasema Mkurugenzi yeyote wa wilaya atakaye mtangaza mshindi wa upinzani atafukuzwa kazi.

Ni wajibu sasa wapinzani kufanya maamuzi magumu, wasusie uchaguzi mpaka itakapo patikana Tume huru na ya haki ya uchaguzi, vingenevyo hawatapata hata kiti kimoja.

Hamna haki, hamna demokrasia, mnashiriki uchaguzi kwenye mazingira haya ili iweje?
 
Ingependeza wakawa wao na wanachama wao tu majukwaani wengne wote tuwe busy na yetu kwani hakutakuwa na jipya tena
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom