Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu,Upinzani Ufanye nini kukomesha hujma za Tume ya uchaguzi ,Wakurugenzi...

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
Sina shaka kuwa upinzani utapata kura nyingi za kuwafanya washinde uchaguzi.

Upinzani watapata kura nyingi za Urais,ubunge na Udiwani.

Swali ni je? Watatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi?

Upinzani wana mkakati gani wa wazi unaoweza kuwajengea imani wananchi kuwa maamuzi yao yataheshimiwa?

Upinzani unawaandaaje wapiga kura kuwa kura zao zitalindwa.

Hapa kwenye usalama wa kura za wananchi ndio inatakiwa iwe ajendaa kuu ya vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu 2020.

Why?

Kuna propaganda zinaenenezwa kwa kasi kuwa Hakuna mkurugenzi atakaemtangaxa Mbunge wa upinzani hata kama atashinda kwa kura.

Kuwa hayo ndio maelekezo ya serikali na hivyo ili Mkurugenzi aendelee kuwa mkurugenzi aralazimika kuulinda ukurugenzi wake kwa kutangaza mgombea wa CCM hata kama arashindwa kwa kura.

Kupitia propaganda hii,Upinzani utakosa wagombea wazuri ambao wanaona kugombea kupitia upinzani n sawa na kupoteza muda na fedha.

Yaani mtu anaona kwanini apoteze muda kugombea,kupiga kampeni,kuwalipa mawakala halafu mwisho hatangazwi hata kama ameshinda?

Athari nyingine ya Propaganda hii inayoenea kwa kasi,ni kuwa wananchi wengi wanakata tamaa,wengine wanajiapiza kutopiga kura kwa madai kuwa wanaemchagua hatangazwi.

Hivyo hainaja kuamka usiku na kushinda kwenye foleni ndefu halafu kumbe mshindi ameshapangwa bila kujali maamuzi ya wapiga kura.

Hapa naona ndio eneo linatakiwa kufanyiwa kazi kwa Upinzani kuwahakikishia wananchi kuwa maamuzi yao hayatachepushwa .

Karibuni kwa mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kubwa ilishafanywa na wapinzani kilichobaki ni sisi wananchi kuchukua hatua dhidi ya udhalimu wa ccm ni muda wa kusimama na kudai haki kwa nguvu
 
Back
Top Bottom