Kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa; CHADEMA mna nafasi ya kujijenga ngome ya CUF Kusini

abubakar MT

Senior Member
Jul 31, 2017
139
230
Jana nilikuwa wilaya ya kilwa, ni ktk wilaya ambayo ni ngome ya CUF asili.

Nilipata fursa ya kuongea na baadhi ya viongozi na wafurukutwa wa CUF juu ya mustakbali wa wao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Majibu yalionyesha kuwa watu waliokwisha kata tamaa na kusema hatutoshiriki tunawaachia CCM

Msingi wa sintofahamu hii ni baada ya CUF asili kusambaratika, ingawa kwa sababu za kimaslahi viongozi waliopo sasa inabidi tu wajiite CUF Lipumba kwa kuwa tu kuna wabunge, madiwani na wenyeviti wa Serikali za mitaa na vitongiji waliochaguliwa kupitia CUF.

Chanzo cha maongezi yetu ni baada ya kusikia kuwa Prof. Lipumba alikwenda kuwatembelea wiki chache zilizopita.

Alikwenda kuomba kuungwa mkono tena huku akimtaja Maalim kuwa ndie alikuwa kikwazo ndani ya CUF, hata hivyo viongozi na wafurukutwa hawakumuelewa na miongozi mwa maswali waliyomuuliza ni "kama ulimuona nyoka ndani ya nyumba kwanini yeye kama baba aliamua kukimbia nyumba na kuwaacha watoto pasi ma usaidizi? Ila baada ya nyoka kuondoka ndio urudi tena nyumbani unadhani wewe kama mzazi watoto watakuelewa vipi?

Swali hili Profesa alijitafuna tafuan kwa muda mrefu na alipomaliza kujibu, yule muuliza swali akamkumhusha tena ajibu swali aliloulizwa na kama hujalielewa basi aurudie tena kumuuliza. Hata hivyo Prof alishindwa kuwashawishi hadhira. Hivyo ni dhahiri kuwa ngome ya CUF kusini imesambaratika.

Na hoja hii inapata nguvu baada mimi kuwauliza wale viongozi na wafurukutwa mnajiandaa vipi na uchaguzi wa serikali za mitaa? Jibu lao lilikiwa rahisi tu tutaaacha Fisiem wafanye wanavyotaka kwani wao hawatoshiriki kabisa.

Ni dhahiri pia kuwa viongozi wa sasa wa CUF watahamia ACT mara baada ya bunge kuvunjwa, yaani mwezi July 2020 kama sijakosea. Lkn wananchi wa kawaida wanaichukia Fisiem zaidi ya ugnjwa wa Ebola. Na wanasuburi chama kitakachowapa hamasa sasa ili waonyeshe hasora zao kwa Fisiem.

Hivyo nafasi hii inaweza kuwa nzuri kwa CHADEMA kwenda kukewa kambi na kujiimarisha sasa.

Hata hivyo lazima CHADEMA waikumbuke na kuiboresha sera yao ya majimbo naamini ni nzuri sana ktk ile dhana ya kila mtanzania awe ni msingi wa maamuzi ya nchi.


Na hakuna anaeachwa nyuma.

Dhana hii Mafisiem hawaitaki, yaani so watamzania wote ni msingi wa maamuzi ya nchi yao. Bali mafisiema wameweka kuwa 80% ya dini moja tu ndio msingi wa maamuzi ya nchi, kwa pile wanachokijata kuwa ni sababu za kihistoria ambapo kimsingi sababu hizo hazipo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom