Uchaguzi 2020 Kuelekea uchaguzi Njombe Mjini, Rushwa yaanza kutumika...

Lwamadovela

JF-Expert Member
Mar 5, 2019
325
235
Habarini wanajamvi. Baada ya salamu nije kwenye mada.

Wote tunajua kuwa tunaenda kwenye uchaguzi mkuu. Msimu huu rushwa hutembea kifua mbele kana kwamba rushwa ni halali 🤔

Mkoani Njombe jimbo la Njombe Mjini kuna mtia nia mmoja ameruhusu viongozi wa chama (CCM) kufanyia kikao kwenye madarasa ya shule yake. Hii imetafsiriwa kama aina ya rushwa kwani yeye ni mtia nia. Asingekuwa mtia nia labda pasingekuwa na shida.

Chama Kata ya Tamadhani kufanyia kikao huko kwa mtia nia haileti taswira nzuri. Katika kikao hicho Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi ndugu Erasto Ngole alihudhuria.

Tunaomba mamlaka husika zidhibiti jambo hili. Mtia nia wa eneo hilo ni Ndugu Alfred Gamaliel Luvanda

Siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya makada wa CCM kukamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa.

Tunaomba na TAKUKURU Njombe mfuatilie hili. Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama alikataa kabisa kufadhili chama hasa nyakati hizi.

Rushwa ni mbaya 🤗🤗🤗2
 
ccm rushwa iko kwenye damu yao...hata huyo magu mbona hata yy anatoa rushwa hadharani?? Takukuru nao ni wala rushwa pia... October mwaga ccm mwaga na pombe yao
 
Acha roho mbaya
Habarini wanajamvi. Baada ya salamu nije kwenye mada.

Wote tunajua kuwa tunaenda kwenye uchaguzi mkuu. Msimu huu rushwa hutembea kifua mbele kana kwamba rushwa ni halali

Mkoani Njombe jimbo la Njombe Mjini kuna mtia nia mmoja ameruhusu viongozi wa chama (CCM) kufanyia kikao kwenye madarasa ya shule yake. Hii imetafsiriwa kama aina ya rushwa kwani yeye ni mtia nia. Asingekuwa mtia nia labda pasingekuwa na shida.

Chama Kata ya Tamadhani kufanyia kikao huko kwa mtia nia haileti taswira nzuri. Katika kikao hicho Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi ndugu Erasto Ngole alihudhuria.

Tunaomba mamlaka husika zidhibiti jambo hili. Mtia nia wa eneo hilo ni Ndugu Alfred Gamaliel Luvanda

Siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya makada wa CCM kukamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa.

Tunaomba na TAKUKURU Njombe mfuatilie hili. Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama alikataa kabisa kufadhili chama hasa nyakati hizi.

Rushwa ni mbaya 2
 
Back
Top Bottom