Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,131
- 44
Najua kama mwanachama wa CHADEMA sikitendei haki chama changu kuanzisha hii thread ya kujadili kuhusu nafasi za uongozi za kitaifa katika uchaguzi mkuu ujao wa CHADEMA. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa taratibu za chama changu sasa ni wakati wa chaguzi za ngazi ya chini za msingi na matawi. Hatujafika hata ngazi ya kata, jimbo, wilaya nk. Kwa mujibu wa taratibu za chama chetu kampeni za uchaguzi wagombea huzifanya katika kikao husika ili kuepusha utamaduni wa ufisadi ambao CCM imeulea wa wagombea kuchafuana kabla, wagombea kupitia mikoani kuhonga kwa wajumbe na pia kufanya kampeni kutokuwa na uwanja sawa kati ya wenye nacho na wasio nacho, wenye cheo na wasio na cheo. Ndio maana ukiondoa Chacha Wangwe ambaye ametangaza kugombea uenyekiti hakuna kiongozi mwingine wa CHADEMA ambaye ametangaza kugombea nafasi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katika mkutano mkuu wa Disemba 12 mwaka 2008. Akitangaza ratiba ya uchaguzi iliyopitishwa na baraza kuu mwishoni mwa mwaka jana, waandishi wa habari walimbana Mwenyekiti Mbowe atangaze kama atagombea au la lakini mwenyekiti alisema kabisa kwa mujibu wa taratibu za chama hayo si masuala ya kuzungumziwa kwa sasa bali kila mwanaCHADEMA ajadili jinsi ya kujenga oganizesheni ya chama mbadala CHADEMA katika ngazi ya mitaa na vijiji kupitia misingi na matawi. Hata hivyo, nimeshawishika kuibua huu mjadala kupata maoni ya umma baada ya kujitokeza kwa hoja kwamba kuna ombwe la uongozi katika chama chetu. Hivyo naombeni maoni yenu kuhusu nani ni nani katika CHADEMA kwenye kikosi kitachokiongoza chama kuelekea uchaguzi wa mitaa na vijiji 2009 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 katika nafasi zifuatazo:
Nafasi za kugombewa na Mkutano Mkuu Taifa:
1. Mwenyekiti
2. Makamu Mwenyekiti(Bara)
3. Makamu Mwenyekiti(Znz)
Nafasi za Kugombewa kwenye baraza kuu(kwa mapendekezo ya majina mawili mawili kwa kila nafasi):
1. Katibu Mkuu
2. Naibu Katibu Mkuu(Bara)
3. Naibu Katibu Mkuu(Znz)
Nafasi za kugombewa katika Mkutano Mkuu wa Wazee:
1. Mwenyekiti wa Wazee(Nafasi hii haipo kwa sasa, itagombewa kwa mara ya kwanza 2008)
Nafasi ya kugombewa katika Mkutano Mkuu wa Vijana:
1. Mwenyekiti wa Vijana(kama hapo juu)
Nafasi ya Kugombewa katika mkutano Mkuu wa Wanawake
1. Mwenyekiti wa Wanawake(Kama hapo Juu).
Nafasi za kuteuliwa na Kamati Kuu:
1. Wakurugenzi( Fedha na Utawala, Oganizesheni na Mafunzo, Rasilimali, Mahusiano ya Kimataifa, Habari na uenezi, Kampeni na Uchaguzi, Ulinzi na Usalama, Sheria na Haki za Binadamu).
2. Makatibu wa Mabaraza( Wazee, Vijana, Wanawake).
Chini ya Katiba Mpya ya CHADEMA toleo la 2006 ambayo ita-replace Katiba ya Mwaka 2004 hapatakuwa na nafasi zifuatazo:
1. Mkurugenzi wa Wazee( Kwa hiyo Kimesera hatakuwepo tena katika nafasi hiyo)
2. Mkurugenzi wa Vijana(Kwa hiyo Mnyika hatakuwepo tena kwenye nafasi hiyo)
3. Mkurugenzi wa Wanawake(Kwa hiyo Mama Kaihula hatakuwepo tena kwenye nafasi hiyo).
Tujadili, NANI NI NANI? KWA NINI?
Asanteni kwa ushirikiano wenu
Asha