Kuelekea Uchaguzi Mkuu vyama vya siasa vyakumbushwa kukabidhi ratiba zake Mapema - Jaji Mutungi

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1590486790794.png

Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mtungi, amevikumbusha vyama vya siasa kukabidhi ratiba zake za mchakato wa mambo mbalimbali wanapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa vinapaswa kumshirikisha Msajili kwenye ratiba zao ndani ya vyama kuhusu mchakato wa uchaguzi. Jaji Mutungi alisema hadi sasa hakuna mabadiliko ya Uchaguzi Mkuu na kwamba licha ya uwapo wa ugonjwa wa corona, shughuli zitaendelea kama kawaida, lakini kwa tahadhari kubwa.

“Tulishawaandikia kwa mujibu wa sheria ya vyama vikifikia kwenye mchakato wa uchaguzi wakumbuke kutupatia ratiba zao

“Hatuvizii ili wakosee bali tunawakumbusha mapema kuweka wazi ratiba zao ili nasi tushiriki…wakienda kinyume tumepewa nguvu kisheria kuweka pingamizi,” alibainisha.

Hivi karibuni, vyama vya CCM, Chadema na ACT Wazalendo, vilitangaza kuanza michakato ya ndani kuelekea uchaguzi mkuu ambao umebakisha miezi mitano

Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni kusajili chama cha siasa kinachokidhi vigezo vya usajili kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ikiwamo kufuta chama chenye usajili wa muda au kudumu ambacho kwa mujibu wa sheria kimepoteza sifa ya usajili.
 
Aliyetafuna 1.5tr nae tumfanyaje binti wa chaote Lumumba pale

Sent using Jamii Forums mobile app
wewe unazungumzia 1.5tr.bila kujengewa mainterchange na maflyover mengi mengi hapabongo siungebaki onayaona kwenye tv tu wewe.
vimejengwa kwa pesa sio nyinyi chadema mbowe kakwapua bilioni 8.9 kapeleka uswiss badala ya kujenga ofisi ya chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... zinatakiwa mapema ili kuangalia namna ya ku-favor magamba - viwanja, muda, vibali vya polisi; n.k. Kila Chadema ikienda kuomba uwanja fulani watajibiwa uko booked hadi desemba 2020; wakienda kuomba kibali watajibiwa tayari chama dola kilishapewa kibali muda na enao hilo hadi desemba 2020. Be careful!
 
Back
Top Bottom