Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Viongozi hawa wajiondoe mapema

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Vuguvugu za kuingia Ikulu, Mjengoni na kwenye Kata, zimeanza kwa pazia la kuelekea Uchaguzi Mkuu kufunuliwa. Tayari baadhi ya vyama vya siasa vimeanza mchakato. Je, ni aina gani ya viongozi watapitishwa na vyama vyao vya siasa ili hatimaye washiriki na kuibuka washindi?

Naorodhesha baadhi ya vigezo ambavyo naamini mwananchi atatumia kushawishika kumpa kura mgombea. Hasa narejea moja ya nasaha za Rais Magufuli kwenye hotuba yake ya kuvunja Bunge. Nanukuu: Kukimbia changamoto ni ishara ya udhaifu, uoga na kutokujiamini - Siku zote njia sahihi ni kukabiliana na matatizo.

Atakayekubalika na wapiga kura ni:
1) Kiongozi shupavu
2) Kiongozi makini
3) Kiongozi asiyekurupuka kimaamuzi na vitendo
4) Kiongozi anayejiamini
5) Kiongozi mcha Mungu
6) Kiongozi mwadilifu
7) Kiongozi mchapa kazi
8) Kiongozi mvumilivu
9) Kiongozi mkweli
10) Kiongozi wa mfano kwa kauli na vitendo vyake.

Katika miaka 5 ya utawala wa sasa nchini, wamejitokeza viongozi ambao kimsingi hawakustahili kuwa wawakilishi wa watu kwani wameonesha dhahiri kuwa ni wachumia tumbo, wabinafsi na wanasiasa uchwara. Utawala wa Serikali iliyoko madarakani umesaidia kuwaonesha wananchi, kwa vitendo, maana ya uongozi wa umma kwa kauli za viongozi wake na vitendo vyao.

Je, wewe mtia nia, umejipima kama unatosha, kabla ya kuchukua fomu, au ndiyo yale yale ya kimazoea? Kila la kheri ukitambua kuwa kichinjio cha wapiga kura kinakusubiri.

UPDATE
Imetokea kwa viongozi ambao hawakusoma bandiko langu jinsi walivyoanguka kama kifo cha mende. Kwa kuwa wana maisha kama sikio la kufa lisilo sikia dawa, hata 2025 watangushwa vibaya. Kutakuwa na Tanzania mpya kuthibitisha wao ndio walikuwa moja ya maendeleo duni katika Jamii na Taifa.
 
Wanasiasa wengi hawana sifa namba 9,ili ushinde,au urudi kwenye nafasi ya uongozi lazima uivunje sifa namba 9.
Ukitongoza ukawa mkweli,mwanamke humpati.!!
Hatuendelei kwa sababu,viongozi wengi hawana sifa namba 9(hawataki kukubali ukweli)!
 
Back
Top Bottom