Uchaguzi 2020 Kuelekea uchaguzi mkuu tupaze sauti zetu kwa haya matatizo...

Santieli

Member
Apr 30, 2014
57
75
Asalaam aleykum...

Kwanza kabisa niwatakie kheri ya Eid al Hajji ndugu zetu waislamu.

Nimeona kwamba katika uchaguzi unaogarajiwa kufanywa mwezi October 2020 kuna mambo ambayo yanaumiza na kukera yafanywayo na taasisi binafsi na zile za serikali ambayo kwa ujumla wake yanamuumiza mtanzania ambaye ndiye mpiga kura kwenye uchaguzi huu.

Na kwa makusudi au kwa bahati mbaya mamlaka ziko kimya bila kutoa ufafanuzi au kufanya upembuzi yakinifu kama kwa kiasi gani hizi huduma zitolewazo na makampuni au taasisi hizi yanaumiza wahitataji.

Kwa Mimi nizungumzie makampuni ya simu za mikononi haswa Vodacom Tanzania, Halotel, Tigo, Airtrl na TTCL kwa ujumla wake.

Haya makampuni ya simu yanaongoza kwa kuwa na gharama kubwa katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watanzania hususani huduma za vifurushi vya Dakika, SMS, Internet bundle n.k na hili linafanyika kwa makusudi au kwa sababu ambazo hawajaweka wazi.

Mfano:- Mb100 kwa voda Tsh 500/= kiasi cha fedha ambacho Ni kikubwa ukilinganisua na kiadi cha bundle unachooewa tena kikiwa valid ndani ya saa24.

NB;- Ikumbukwe kuwa kukua kwa teknolojia kunalazimisha baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii kufanywa kupitia internet ili kukuza ufanisi na uokoaji wa gharama na muda. Jambo ambalo Lina kwamisha na kamouni hizi za simu na kufanya wananchi kutumia kiasi kikubwa cha gharama kuendesha shughuli hizo na kuchochea kupungua kwa kipato cha mtu na mtu huku nakampuni hayo yakizalisha kiasi kikubwa cha faida.

Changamoto nyingine licha ya kuwa na gharama kubwa za kimawasilisno lakini pia huduma hizi kuwa chini ya kiwango mfano:-
1. Mtandao kupotea hali ya kua umeunga kifurushi

2. Kupewa kifurushi kwa kukomolewa mfano kinaanzia saa7 usiku hadi saa 12 alfajiri..

3. Kifurushi kuwa na speed ndogo au kuisha haraka

4. Network signal kupotea kabisa kutokana na minara kuisha mafuta hususani vijijini.

5. Kuchelewa kwa SMS au ku fail kwa sms mara kwa mara.

Pia lingine kubwa zaidi Ni gharama za kimiamala ya kifedha .
Kamouni hizi zimekua zikiongeza tozo za kutuma na kutoa fedha mara kwa mara kwa kiasi ambacho Ni kikubwa ukilinganisha na huduma uliyopewa na gharama za maisha za sasa.

Tunakoelekea watu tutaanza kutunza oesa ndani au kuagiza kwa njia ya barua kutokana na kukithiri kwa makato makubwa.

Lingine Ni kutumiwa sms za Matangazo ya, betting, jackoot na nyingine nyingi bila ridhaaa imekua kama sehemu ya matangazo kitu ambacho kina kera na kukulazimisha utazame simu yako mara kwa mara.

Hayo ndio mikngoni mwa kero kubwa kwangu amvayo ningeomba watanzania tuungane kuchagua viongozi watakao onesha kujua matatizo yetu na pia kutupatia mkakati wa bamna ya kuyatatua na muda wa kuyatatua, hao ndio tunaowataka tuwaoe kura ili wananchi tuoate huduma bora za mawasiliano na kifedha kwa kuzingatia gharama rafiki kulingana na mazingira na vipato vyetu.

Hii ndio kero yangu
Kama unayo yako weka hapa pia ili tujuzane sote matatizo yetu na tumjue mwenye nia ya dhati ya kutatua ili tupige hatua.....
It Can Be

2020
 
Humu JF kuna watu wanafiki sana. Kuna mtu aliibuka humu na kudai angeyashitaki Makampuni ya Simu kwa kutufanyia madudu mengi Wateja wake mara kifurushi kuisha muda wake wakati ni bidhaa uliyokwisha inunua na mengine mengi na akatoa siku 90 ili Makampuni hayo yafanye marekebisho, sijui aliishia wapi...!!
 
CCM ni wanafiki sana. Wanajiona kama wao hawaumii na hizi gharama wakati wanamaisha ya ufukara na urofa kuliko hata wa kwetu
 
CCM ni wanafiki sana. Wanajiona kama wao hawaumii na hizi gharama wakati wanamaisha ya ufukara na urofa kuliko hata wa kwetu
Hili tatizo Ni ka wote haswa wale tunaoitwa wanyonge au maskini ....
Watakao mudu gharama hizi bila kuziwazia Ni wale wenye uchumi wa kati.....
 
Hivi hawa wanaochaguaga CCM ambao wanamaisha magumu haswaaa huwa wanapewa dawa ya kichawi? Mbona huwa siwaelewi kabisaaa
 
Hivi hawa wanaochaguaga CCM ambao wanamaisha magumu haswaaa huwa wanapewa dawa ya kichawi? Mbona huwa siwaelewi kabisaaa
Shida hapa huwa Ni uelewa kuwa unapopiga kura unatakiwa uweke mbali mapenzi ya chama ila zingatia sera, mkakati wa utekelezaji wa sera na usikivu na hekima za mtoa sera....
Mbali na hapo huishia kuchagua kwa mapenzi ya rangi, nyimbo, posho, pombe n.k
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom