Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba: Kuna uwezekano mkubwa wa Mitandao ya Kijamii kuzimwa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
Wakuu ndani ya Jamii forums. Wageni kwa wenyeji ni vema tukajiandaa kabisa kisaikolojiia na ikibidi kuweza kabisa kuanza mchakato wa kuwa na plan B.

Kadiri fukuto la uchaguzi mkuu linavyoanza kupanda kuna viashiria vya kila aina kwamba kuna mamlaka hazipendi baadhi ya habari kuwafikia wananchi wengi habari zitakazotoka ni zile tu zilizochujwa na ama la kuhaririwa na mamlaka husika.

Tayari vyombo vya ndani vimeshapewa onyo na karipio la kurusha habari kutoka vyombo washirika nje ya nchi ...pamoja na kuathirika kimapato kwa hatua hiyo ...wananchi wataigeukia mitandao ya kijamii yenye nguvu kuliko hata hivyo vyombo rasmi vya habari

Sambamba na hilo tutegemee wakati wowote toka sasa bei za vifurushi vya kuperuzi mitandaoni vikizidi kubadilika na kuwa ghali zaidi...kama mnakumbuka zoezi kama hili lilifanyika kuelekea uchaguzi mkuu 2015 na kamwe hatukuwahi tena kurudishiwa ule unafuu wa data.

Hizi online tv na radio pia zijiandae na haya maumivu...Ilishatolewa tahadhari kubwa kwamba kila unachokifanya mitandaoni kinafuatiliwa kwa karibu sana...watu kidogo wamekuwa makini kwenye hilo...lakini sasa hilo kilikuwa cha mtoto tuuu...maumivu makali yanakuja.

Wito wangu kwa mamlaka husika: kwa heshima kuu naomba muwe na tafakuri jadidi kwenye hili...uhuru wa kupashana habari ni hitaji muhimu na la msingi kwa watu wote...hili husaidia kuepusha hatari nyingi....Fanyeni yote lakini chondechonde msije mkazima mitandao ya kijamii.

Uchaguzi wenye changamoto za ushindi kama huu huwa na fukuto kila upande na kwa kila mmoja....njia pekee ya kupoza hili fukuto ni kutoa uhuru watu waseme lakini bila kuvunja sheria...watu wakisema hupata nafuu kubwa ndani ya miili yao

Kuwazuia kusema ama kuwazuia kupata habari ni sawa na kuruhusu maji kuingia kwenye nyumba isiyo walau na upenyo wa maji kutoka. Matokeo yake ni uharibifu mkubwa

Mungu ibariki Tanganyika na watu wake ili wote kwa umoja wetu tutambue kuna maisha baada ya uchaguzi!!

Jr
 
Wakuu ndani ya Jamii forums...Wageni kwa wenyeji...ni vema tukajiandaa kabisa kisaikolojiia na ikibidi kuweza kabisa kuanza mchakato wa kuwa na plan B..
Acha kutisha watu wewe, Watumiaji wa mitandao ni wachache kuliko wapiga kura,bado hamjaweza kuitisha serikali kwa kutumia mtandao
 
Kipindi kama hiki 2015 ndio vifurushi vya kuperuzi mitandaoni vilipanda bei bila taarifa lakini kwa vile wananchi walikuwa huru kusema hawakuliona hili...ama hawakulizingatia
FB_IMG_1597056129046.jpg


Jr
 
Wakuu ndani ya Jamii forums...Wageni kwa wenyeji...ni vema tukajiandaa kabisa kisaikolojiia na ikibidi kuweza kabisa kuanza mchakato wa kuwa na plan B...

Kadiri fukuto la uchaguzi mkuu linavyoanza kupanda kuna viashiria vya kila aina kwamba kuna mamlaka hazipendi baadhi ya habari kuwafikia wananchi wengi....habari zitakazotoka ni zile tu zilizochujwa na ama la kuhaririwa na mamlaka husika

Tayari vyombo vya ndani vimeshapewa onyo na karipio la kurusha habari kutoka vyombo washirika nje ya nchi ...pamoja na kuathirika kimapato kwa hatua hiyo ...wananchi wataigeukia mitandao ya kijamii yenye nguvu kuliko hata hivyo vyombo rasmi vya habari

Sambamba na hilo tutegemee wakati wowote toka sasa bei za vifurushi vya kuperuzi mitandaoni vikizidi kubadilika na kuwa ghali zaidi...kama mnakumbuka zoezi kama hili lilifanyika kuelekea uchaguzi mkuu 2015 na kamwe hatukuwahi tena kurudishiwa ule unafuu wa data
Hizi online tv na radio pia zijiandae na haya maumivu...Ilishatolewa tahadhari kubwa kwamba kila unachokifanya mitandaoni kinafuatiliwa kwa karibu sana...watu kidogo wamekuwa makini kwenye hilo...lakini sasa hilo kilikuwa cha mtoto tuuu...maumivu makali yanakuja....

Wito wangu kwa mamlaka husika: kwa heshima kuu naomba muwe na tafakuri jadidi kwenye hili...uhuru wa kupashana habari ni hitaji muhimu na la msingi kwa watu wote...hili husaidia kuepusha hatari nyingi....Fanyeni yote lakini chondechonde msije mkazima mitandao ya kijamii....

Uchaguzi wenye changamoto za ushindi kama huu huwa na fukuto kila upande na kwa kila mmoja....njia pekee ya kupoza hili fukuto ni kutoa uhuru watu waseme lakini bila kuvunja sheria...watu wakisema hupata nafuu kubwa ndani ya miili yao

Kuwazuia kusema ama kuwazuia kupata habari ni sawa na kuruhusu maji kuingia kwenye nyumba isiyo walau na upenyo wa maji kutoka......Matokeo yake ni uharibifu mkubwa

Mungu ibariki Tanganyika na watu wake ili wote kwa umoja wetu tutambue kuna maisha baada ya uchaguzi..!!!!

Jr
Miaka mitano jamaa anatba mwenyewe kwenye runinga lakini baada hajiamini
 
Katika Jambo ambalo nilikataliwa ni kutoaddiwa kwa jf WhatsApp group Mana admin ni ndugu yangu na kakataa Hata kwa ela na manguli wapo Tena wale malegend nawaonaga tu
 
Back
Top Bottom