beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,325
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa hakitashirikiana na vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na Nipashe jana, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF Taifa, Juma Kilaghai, alisema chama hicho hakiwezi kushirikiana na vyama hivyo kwa sababu wamejifunza kwa kilichotokea katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Mwaka 2015 vyama vya upinzani viliungana na kuunda umoja wa Katiba ya Wamanchi (Ukawa), ulianza wakati wa mchakato wa katiba mpya mwaka 2014, na kwenda hadi wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu ambao waliingia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja kwenye nafasi mbalimbali.
“Kwa kilichotokea katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilitufundisha, hatuwezi kurudia kosa, sisi tuko tayari kushirikiana na vyama vyenye nia ya dhati na kile wanachokizungumza,” alisema Kilaghai na kuongeza:
“Tulishirikiana na Chadema kwa sababu walisema kwamba wanapambana na rushwa, lakini cha kushangaza walitoka nje ya kile wanachokizungumza na kukaribisha wala rushwa kugombea nafasi za juu ndani ya chama chao, na sababu hiyo ndiyo ilichangia CUF kuvurugana na kina Maalim Seif ambao sasa hivi wako ACT-Wazalendo na wanashirikiana tena.”
Alisema ratiba ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa watia nia kwa nafasi ya urais mwisho ni leo na kwamba mpaka juzi walikuwa na mtia nia mmoja tu kwa nafasi hiyo, Mutayesa Yemba.
Kwa watia nia kwa nafasi ya udiwani, uwakilishi na ubunge alisema wanatarajia kufunga ratiba hiyo Julai 27 na 28 kuanza vikao kwa ajili ya uteuzi wa wagombea.
Alisema mpaka sasa idadi ya watia nia kwa nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi ni kubwa
Chanzo: IPP MEDIA