Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi Mkuu; CHADEMA Moshi wataja Orodha ya Mafisadi

Kamende

JF-Expert Member
Mar 1, 2008
416
45
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika mji wa Moshi yametajwa majina ya madiwani 12 wa CCM ambao wamengoza kwa kutoa, kutetea na kunyamazia hoja zinazodhoofisha maendeleo ya Moshi.

Majina hayo yamesomwa katika mkutano wa hadhara ambao uliohudhuriwa na Mhe. Philemon Ndesamburo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro na mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini.

Hatua ya kusoma majina hayo imefikiwa baada ya kuridhika kuwa madiwani hao 12 wa CCM ni sababu kubwa ya kila tatizo la Halmashauri ya manispaa ya Moshi.

Mkutano huo uliohudhuriwa na watu wengi sana ulipambwa na mamia ya vijana wa CHADEMA waliovalia sare nzuri za fulana za rangi nyekundu na light blue

Akihutubia mkutano huo Ndesamburo alihoji kitendo cha rais na viongozi wa juu kabisa wa serikali kuchangisha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukomboa jimbo la Moshi wakati sheria ya uchaguzi hairuhusu zaidi ya TSH 50,000,000 kutumika kwa jimbo moja.
"Hawa wanatunga sheria; lakini wakiikumbuka Moshi na Ndesamburo wanaisahau hiyo sheria kabisa" Alisisitiza.







 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom