KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,589
- 4,599
Nikiwa katika mitaa Fulani karibu na ofisi ya chama Fulani cha Upinzani(jina kapuni) kulizuka mabishano makubwa yaliyoambatana na swali " Je, upizani utafurukuta uchaguzi huu kama ilivyokuwa 2015?" Kwa hakika wachangiaji walinifurahisha majibu yao lakini mchangiaji mmoja aliyejinasibu kama mpinzani kindakindaki wa agano na viapo ndio aliyenifurahisha Zaidi alivyosema, namnukuu ' mimi ni mpinzani kabisa lakini sitakaa kuwa adui wa mabadiliko makubwa yanayoletwa na Rais Magufuli nchini, hivyo nitampigia kura yangu'.
Alivyokwisha kusema hayo wanachama wenzake wakamshangilia na kumwambia hakika umechelewa kujua hilo lakini bado hujachelewa kufanya uamuzi sahihi kwa nchi na mjadala ukamalizika kwa kila mtu kusema TUKUTANE OCTOBA, KULA UPINZANI LAKINI KURA KWA MAGUFULI.
My Take:
Tusidanganywe na yanayoendelea mitandaoni juu ya Rais Magufuli, huko mitaani na vijijni Rais Magufuli Magufuli ndio chaguo la vyama vyote, watu hawafichi hisia zao za kweli mitaani.