Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 28 Oktoba 2020: Ufahamu mfumo na Mzunguko wa Uchaguzi unaotumika Tanzania

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1602080853629.png

Mfumo wa Uchaguzi Kwa Mujibu wa Jarida la Tume ya Taifa ya Uchafguzi Tanzania Ukurasa wa 8

Tanzania inatumia mfumo wa uchaguzi ambao mgombea anayepata kura nyingi halali kuliko mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi (First – Past – the Post). Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, kifungu cha 35F(8) na 81(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 82(a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Mfumo mwingine unaotumika ni ule wa uwiano wa kura (Proportional Representation) ambao hutumika kupata Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum.

Mzunguko wa Uchaguzi

Ibara za 42 (2) na 65 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na kifungu cha 12 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 zinaelekeza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ufanyike kila baada ya kipindi cha miaka mitano (5

Kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani, katika kuendesha shughuli za uchaguzi, Tanzania hutumia utaratibu wa mzunguko wa uchaguzi ambao umegawanyika katika awamu tatu (3) kama ifuatavyo; kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

WFRCD.PNG

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom