Kuelekea uchaguzi mkuu 2020: Je, masheikh wa Uamsho ndio karata ya turufu Zanzibar?

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,988
22,379
Habari wadau,

Kama ijulikanavyo, Zanzibar waislam ni 99% ya watu wote. Ni nchi yenye idadi ya watu inayokaribia 2M kwa sasa. Kikawaida kwa waislam, wao huwa ni waislam kabla ya mengine yote yaani kama ni utaifa basi wao ni waislam kabla kuwa Wazanzibari, kama ni mambo ya mipira , basi wao ni waislam kabla ya U-Yanga wao au U-Simba wao, kama ni uchama basi wao ni waislam kabla ya U-CCM wao au U-ACT wao.

Swali langu ni je, suala la Masheikh wa Uamsho linaweza likawa ni turufu kubwa ya uchaguzi huu kwa upande wa Zanzibar?

Nimesikia kwamba kuna mpango wa Mahakama kuwarudisha Zanzibar masheikh waje waendelee na kesi yao kule Zanzibar, uamuzi huu unawezekana ukawa umeshajihishwa na muelekeo wa hali ya siasa ulivyo kwa sasa visiwani humo?

Sisi wengine si wajuvi wa haya mambo. Wataalam hebu tusaidieni.

Nguruvi3
dos.2020
Kichuguu
Mmawia
Jumbe Brown
Zitto
Gavana
Sky Eclat
Mshana Jr
Magonjwa Mtambuka
Ado Shaibu
CUF Habari
Kikwajuni One
zanzibakwetu
Zanzibar-ASP
zanzibar huru
Erythrocyte
 
Hakuna kubahatisha hapo. Yaani wanahusika na ishu za Kibiti bila kubahatisha. Nahisi wale madogo walibanwa wakasema kila kitu
 
Kama hujui kitu ni bora kukaa kimya, unasema 'Wanahusika na ishu za Kibiti bila kubahatisha" Halafu hapo hapo unasema "Nahisi wale madogo walibanwa.... wakasema kila kitu"

Kumbe una hisi tu!

JF ni fact tu na sio hisia za mtu, Mambo ya kuhisi peleka kwenye vijiwe vya kahawa huko sio hapa.
 
Wazenj hawadanganyiki na wameshasema wanataka Nchi yao. Kuwapora tena ushindi kama 2015 haiwezekani au kutakuwa na maafa makubwa sana.
Unahisi kwamba Wazanzibari bila kuangalia itikadi zao za vyama kwa pamoja wataamua kukipigia kura kile chama kinachoonyesha angalau nia ya kutenda haki kwa masheikh wao???
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Habari wadau,

Kama ijulikanavyo, Zanzibar waislam ni 99% ya watu wote. Ni nchi yenye idadi ya watu inayokaribia 2M kwa sasa. Kikawaida kwa waislam, wao huwa ni waislam kabla ya mengine yote yaani kama ni utaifa basi wao ni waislam kabla kuwa Wazanzibari, kama ni mambo ya mipira , basi wao ni waislam kabla ya U-Yanga wao au U-Simba wao, kama ni uchama basi wao ni waislam kabla ya U-CCM wao au U-ACT wao.

Swali langu ni je, suala la Masheikh wa Uamsho linaweza likawa ni turufu kubwa ya uchaguzi huu kwa upande wa Zanzibar?

Nimesikia kwamba kuna mpango wa Mahakama kuwarudisha Zanzibar masheikh waje waendelee na kesi yao kule Zanzibar, uamuzi huu unawezekana ukawa umeshajihishwa na muelekeo wa hali ya siasa ulivyo kwa sasa visiwani humo?

Sisi wengine si wajuvi wa haya mambo. Wataalam hebu tusaidieni.

Nguruvi3
dos.2020
Kichuguu
Mmawia
Jumbe Brown
Zitto
Gavana
Sky Eclat
Mshana Jr
Magonjwa Mtambuka
Ado Shaibu
CUF Habari
Kikwajuni One
zanzibakwetu
Zanzibar-ASP
zanzibar huru
Erythrocyte
hata wakiwaachia, it's already too little too late.... haiwezi kupindua meza ya Maalim!!
 
Kama hujui kitu ni bora kukaa kimya, unasema 'Wanahusika na ishu za Kibiti bila kubahatisha" Halafu hapo hapo unasema "Nahisi wale madogo walibanwa.... wakasema kila kitu"

Kumbe una hisi tu!

JF ni fact tu na sio hisia za mtu, Mambo ya kuhisi peleka kwenye vijiwe vya kahawa huko sio hapa.
Nadhani hili ni jibu sahihi kabisa.

Hadhi ya JF iko juu, hivyo ukiongea tena hususan ukiongelea baadhi ya mada unatakiwa uwe deep na sio kuhisi hisi tu
 
Sielewi kwa nini uliniweka hapo, ila mimi mambo ya udini na taifa huwa sijui!
Mwandishi ameandika kulingana na hulka chaguo maisha ya wa Zanzibar hakuna Udini hapo kwasababu maisha ya wa Zanzibar 99% ni muslim katika hili kitu kidogo kinachohusiana na maslahi ya uislamu linagusa maisha ya itikadi zao kwa ujumla.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom