Kuelekea uchaguzi mdogo Arusha mjini -CHADEMA iwatendee haki makamanda hawa wa polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea uchaguzi mdogo Arusha mjini -CHADEMA iwatendee haki makamanda hawa wa polisi

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by isotope, Apr 6, 2012.

 1. i

  isotope JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wale waliofatilia uchaguzi mkuu wa 2010 watakumbuka michango ya waliokuwa RPC hawa; Simon Siro (Mwanza) na Basillio Matei (Arusha) katika kujenga demokrasia. Kutokana na jinsi walivyosimamia haki, wakuu wao waliwarudisha makao makuu wakasome magazeti. Jambo la kushangaza, sijawahi kusikia chadema ikiwaenzi watumishi hawa licha ya michngo yao mikubwa.nimehudhuria mikutano mingi ya chadema (ya hadhara) ila cjapata kusikia. Nafikir ni wakati sasa wa kujali mchango wa kila mmoja ktk kuleta mabadiliko nchini mwetu!
   
 2. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kamanda, wajitaidi kuwatetea!
   
 3. i

  isotope JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  nimeandika haya baada ya kutafakari matukio yanayoikumba chadema Arusha na Mwanza tangu kuhamishwa kwa makamanda hawa. Wote tunajua alichokifanya Andengenye mara tu baada ya kuhamishiwa Arusha (Mauaji ya Arusha) na sasa Barlow (polisi kushuhudia wabunge wakikatwa mapanga). Tusipowatia moyo wale wanaojitoa kusimamia haki tunadhoofisha dhamiri zao. Natamani kusikia japo majina yao yakitajwa mara kwa mara kama mfano wa kuigwa na polisi wote.
   
 4. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Walizidiwa na nguvu ya umma.

  CDM wasipoteze muda wa kuwapongeza. Ilikuwa wajibu wao kama walifanya hivyo kweli.
   
 5. p

  pembe JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Maadamu walitenda haki kama maadili yanavyosema Mungu atawalipa maradufu tu. Mara nyingi mshahara wa kutenda haki ni kutotendewa haki wewe mwenyewe!
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  chadema ipongeze nguvu ya umma na si vinginevyo!
   
 7. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakistaafu wajiunge na umma kuoonyesha njia na kurahisisha mabadiliko ////////:clap2:
   
 8. N

  N series Senior Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yani polisi akimtendea wema raia anatakiwa kupoozwa na chochote?????
  hayo ni maswala ya magamba, ile ni moja kati ya duties na responsibility zao, kwanza hao ma RPC wali perform chini ya kiwango,
   
 9. i

  isotope JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hapo juu nimetoa mfano wa Andengenye na Mauaji ya Arusha, mpaka sasa jamaa anadunda mzigo na kutanua kwa kodi zetu. Hata wao wangeweza kuua watu kadhaa kuwaridhisha wakubwa wao na kulinda ajira zao ila hawakufanya hiyo. Kwa nchi ambayo polisi wake hawajui wajibu wao, wale wachache wanaoonyesha japo punje ya uadilifu tunapaswa kuwatia moyo. Acknowledgement sio lazima umpatie kitu, neno tu linatosha!
   
 10. i

  isotope JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sehemu nyingi nguvu ya umma ilipofanikiwa bila umwagaji damu imetokana na uadilifu wa polisi na jeshi. Tuiona Misri, jeshi liliposupport nguvu ya umma. Kwa taarifa yako hata huko Mwanza wakati 2010 G.E polisi waliwasupport raia.
   
 11. i

  isotope JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Okay, tuamini nguvu ya umma pekee iliyofanya kazi Arusha october 2010. Ni kitu gani kilisababisha nguvu hiyo hiyo ya umma ishindwe kufanya kazi katika mauaji ya Arusha januari 2011, miezi miwili tu baadae!!? Chadema kama chama lazima kitafutwe kuungwa mkono na watendendaji waadilifu wa vyombo vya dola ili kiweze kufaidi vema nguvu ya umma inayokisupport.
   
 12. L

  Laban Boaz Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cdm wamekupata mkuu kama ni stahili kupongezwa watapongezwa tu. Kuwa mwenye subira.
   
Loading...