Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

Mitanzania bwana, je kama Shimbo anamaanisha hata JK akishindwa akubali matokeo? Hapo itakuwa sawa? Au bado mtabwatuka?

Naona nawe bado unawabwatukia tu bure Watanzania!! Hata kama ni Prof. Lipumba au Dkt. Slaa anashinda; kama ushindi huo si wa halali Watanzania wanahaki ya kupinga matokeo. Niambie kwanini hii 'mitanzania' iyakubali tu matokeo kwa vile tu yametangazwa hali vielelezo vya kuchakachuliwa vikiwepo??!

Plus... yeye kama Mnadhimu, na kwa kuzingatia profession yake; haihitaji kipaji cha sayansi za anga kujua kuwa kutoa tamko kama hilo katika kipindi hiki cha uchaguzi is simply unprofessional!!
 
[FONT=Arial, sans-serif]Hii nimeipata sasa hivi
[/FONT]
Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vimewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC na kutothubutu kupinga matokeo hayo na kusababisha vurugu.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Luteni Jenerali Abdurahmani Shimbo ametoa tamko hilo leo Jijini Dar-Es-Salaam kufuatia kuwepo kwa taarifa za vyama vya kisiasa kujiandaa kukataa matokeo yatakayotangazwa na tume ya uchaguzi.

Luteni Jenerali Shimbo amesema vyombo vya usalama vimejipanga kukabiliana na hali yoyote ya vurugu ambayo itajitokeza na kuwaonya watu kutoshiriki katika vurugu zozote baada ya kutangazwa matokeo.

Sikio la kufa alisikii dawa, Mwalimu Nyerere alituhasa kuwa JK hafai lakini hatukusikia na tulisema ni 'handsome'. Sasa anabinafsisha na JWTZ kuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa maslahi ya familia. Kwani baada ya Ridhiwani kunusurika kipigo huko Iringa sasa anatangaza hali ya hatari (state of emergency) wakati hata hizo vurugu hazina ushahidi wa kutokea kwake!

Rais wa awamu ya tatu, Mkapa alisema pigania haki yako hata kama ikibidi kufa ufe. Sasa kura ni haki yangu, kwa nini niwe tayari kufa?
 
shimbo katumwa... na kila anayeijua nchi atapata wasiwasi kudhania vinginevyo!!! tumepata shida kadhaa zilizohitaji intervention yao lakini alikaa kimya, pamoja na hayo, yeye ana mpini na lazma hilo lieleweke

vita isiyo na limits haiwezekani na slaa jeshi ndio limit yake: ingekua poa kwa yeye kudharau kauli za mjeshi na kuendelea kuhimiza watu wapige kura kwa wing, wazilinde tena kwa amani ya bwana

Huo ulinzi wa kura ndiyo unaotafsiriwa na wapuuzi kama shimbo kuwa kuleta fujo.
 
Luteni+Jenerali+Abdulrahman+Shimbo+Mnadhimu+Mkuu+wa+JWTZ.jpg


A Poor General......

Huyu jamaa ni mmoja kati ya wale makada wachache sana wa CCM ambao walipanda juu sana jeshini. Wenzake ni akina JK,Chiligati,Makamba,Kinana ambao hawakuvuka ukanali....siasa hazijamtoka...ni kaka wa yule mgombea wa ubungo CCM....inadaiwa kuwa JK akisoma kule Tanga School alikuwa akihifadhiwa na Baba wa huyu jamaa
 
Luteni+Jenerali+Abdulrahman+Shimbo+Mnadhimu+Mkuu+wa+JWTZ.jpg


A Poor General......

Huyu jamaa ni mmoja kati ya wale makada wachache sana wa CCM ambao walipanda juu sana jeshini. Wenzake ni akina JK,Chiligati,Makamba,Kinana ambao hawakuvuka ukanali....siasa hazijamtoka...ni kaka wa yule mgombea wa ubungo CCM....inadaiwa kuwa JK akisoma kule Tanga School alikuwa akihifadhiwa na Baba wa huyu jamaa

Halafu amekaa kama chapombe fulani hivi. Hivi ana elimu gani huyu mbwiga?
 
Ndugu Wana JF,

Nimekuwa nikitafakari ushiriki wa JWTZ na tamko la Chief Joint of Staff Luteni Jenerali ABDALAH. A. Shimbo kuhusiana na mwenendo wa kampeni za uchaguzi na kushinikiza vyama vya siasa kukubali matokeo ya aina yoyote kabla hata ya kura hazijapigwa! Kwa wachambuzi wengi wa mambo na mwenendo wa hali ya kisiasa ya nchi wameweza kudokeza wasiwasi mkubwa kutokana na tamko hilo la JWTZ kupitia Luteni Jenerali A. A. Shimbo, Kitu ambacho hakijawahi kutokea toka misingi ya taifa letu miaka 50 iliyopita.

Hivyo basi, tukizingatia kuwa mpaka hivi sasa hakuna hali ya hatari ambayo inatoa nafasi kwa JWTZ kutoa tamko zito namna hiyo, kwani kampeni za mzunguko wa kwanza zimekamilika bila ya kuwa na matukio yoyote makubwa ya uvunjifu wa amani na matukio yote yalio jitokeza yamo ndani ya uwezo wa jeshi la polisi. Sasa wananchi wengi tunajiuliza kulikoni JWTZ?

Watu wengi tunaelewa kuwa mgombea wa CCM KANALI MSTAAFU WA JWTZ JAKAYA MRISHO KIKWETE anakabiliwa na upinzani mkubwa sana toka kwa wagombea wa CHADEMA DR WILBROAD SLAA NA MGOMBEA WA CUF PROF. IBRAHIM LIPUMBA na upepo wa kisiasa umewapa kibarua kigumu chama cha mapinduzi kutetea rekodi yao ya miaka 50 wakiwa madarakani. Hivyo basi kila dalili zinaonesha kuwa CCM na mgombea wao KANALI MSTAAFUU WA JWTZ JAKAYA KIKWETE kuna uwezekano mkubwa wa kuanguka kwenye uchaguzi utakaofanyika tarehe 31st october 2010,

Hivyo kumekuwa na jitihada na mikakati mingi ya kuujaribu kukinusuru chama hicho kikongwe kutoweka katika ulimwengu wa siasa za africa baada ya anguko, na mikakati mingi ni kutumia rasilimari nyingi za umma kama vyombo vya habari vya umma kutoa upendeleo wa coverage kwa chama tawala, kutumia nguvu ya viongozi wa umma na serikari kama wakuu wa mkoa na wilaya, kutumia siasa chafu za majitaka, matuumizi makubwa ya pesa lakini yote hiyo haijasaidia kubadilisha upepo wa kisiasa kwa kiasi kikubwa kama walivyotegemea.

Wananchi wengi wameonesha kutokukiunga mkono chama hicho tawala kutokana na hali ya uchumi kuwa mbaya zaidi toka raisi anemaliza mda wake Kanali mstaafu wa jeshi Jakaya Mrisho Kikwete, wananchi wengi wameathirika vibaya sana na mfumuko wa bei na bidhaa kupanda bei kwa zaidi ya 100% wakati vipato vyao vimebaki kuwa chini , hivyo basi kutokana na jitihada ndogo ambazo haazijazaa matunda za serikari ya ccm kukabiliana na mfumuko wa bei!

Hali kadhaliika hasira za wananchi wengi dhidi ya serikari ya JK ni kuhusiana na scandal za ufisadi na jinsi uwezo wa serikari ya ccm chini ya JK ilivyo kabiliana nazo, hii nayo imekuwa mwiba mkubwa ndani ya chama tawala ambapo hata baadhi ya wanachama wengi wanaweza kupigia vyama vya upinzani kati ya CHADEMA na CUF, kutokana na ukosefu wa dhamira ya dhati ya kupambana na UFISADI, ni hii imewavunja moyo wana ccm wengi kuona RAISI KANALI MSTAAFU WA JWTZ JK akiwapigia debe hadharani watuhumiwa wakuu wa ufisadi ambao wengine walishawahi kuwajibishwa na bunge na kujiuzuru nyadhifa zao na wengine wakiwa na kesi mahakamani! hii imewachanganya watanzania wengi ambao wapo kwenye mapambano ya ufisadi hususani wana CCM.

Swala lingine linalokitikisa chama hiki tawala na kukiweka katika mazingira ya kushindwa uchaguzi ni makundi yaliyotokana na mtandao wa JK mwaka 2005 na majeruhi wa kula za maoni ambazo zilitawaliwa na kila irregularity.

Hivyo basi kutokana na tathimini iliyofanywa na CCM na wachunguzi mbalimbali inaonesha kuwa watanzania wako tayali kwa mabadiliiko na kutomchagua mgombea wa CCM wa uraisi na wagombea wengi wa ubunge toka chama hicho tawala, tafiti za baadhi ya taasisi zilionesha hilo ijapokuwa vilizuliwa kutoa matokeo ya utafiti huo kwani ungeweza kukiweka chama hicho katika hali ngumu zaidi.

Hivyo basi CCM wanatambua ndoto za kushinda katika uchaguzi ulio huru na wa haki kwa kutumia ballot paper hazitawezekana, hivyo wameamua kutumia njia zisizo rasmi kuhakikisha wanaendelea kubaki madarakani na kulindana. Mkakati wa kwanza ulio chukuliwa na wana CCM ni kuwaandaa ki saikolojia wananchi kuwa CCM LAZIMA ITASHINDA NA KUWAKATISHA TAMAA WANANCHI WENGI KUWA VYAMA VYA UPINZANI HAVINA NAFASI YA KUSHINDA. Hayo yalianza na kituko cha mhariri wa gazeti la serikari kutoa statement kuwa the "TRUTH IS DR. SLAA SHALL NEVER BE THE 5TH PRESIDENT OF UNITED REPUBLIC OF TANZANIA" Serikari imekaa kimya mpaka leo haijakanusha habari hiyo kuwa matokeo yamekwisha pangwa kabla hata ya uchaguzi kufanyika, hivyo statement ya mhariri wa serikari kwenye gazeti la serikari ni kauli ya serikari kwani serikari haijachukua hatua yoyote mpaka hivi leo.

Lakini CCM na mgombea wao KANALI MSTAAFU JAKAYA KIKWETE WAMEKWENDA MBELE ZAIDI KWA KUHAKIKISHA HUO USHINDI WA LAZIMA HATA KAMA KUWAPORA UAMUZI WANANCHI WALIO WENGI KWA KUTUMIA JESHI LA WANANCCHI KUWATISHA WANANCHI, HUU UNAONEKANA NI MPANGO ULIOPANGILIWA VIZURI NA KWENDA KWA AWAMU ILI KUPORA USHINDI WA WANANCHI,

HIVYO BASI NAPATA WASIWASI SANA KUONA JESHI LA JWTZ LIMEINGIZWA SANA KWENYE SIAASA HUSUSANI MAAFISA WENGI BAADA YA KUSTAAFU HUPEWA NYADHIFA ZA U RC NA DC, AU UKURUGENZI WA BOARD MBALI MBALI HUKU WAKIENDELEA KUWA MAKADA WAAMINIFU WA CCM. HUU NI MKAKATI MAALUMU WA CCM KUHAKIKISHA UPINZANI KAMWE HAWEZI KUPATA UONGOZI WA NCHI HII, TUMESHUHUDIA JUZI JINSI Luteni Jenerali A. A. Shimbo ALIVYO UONESHA DHAHILI KUKINGIA KIFUA NA KUHALALISHA USHINDI WA MEZANI WA CCM UNAPATIKANA BILA JASHO! HIVYO HII INADHIHILISHWA NA WANAJESHI KUSHIKA MADARAKA YA NCHI NA POST MUHIMU SERIKALINI, TUANZE KUWACHAMBUA WANAJESHI WALIO KWENYE SIASA, TUKIANZIA NA KANALI MSTAAFU JAKAYA KIKWETE, MWENYEKITI WA KAMPENI YA JK NI KANALI MSTAAFU ABDULAHAMAN KINANA, KATIBU MKUU WA CCM NI LUTENI MSTAAFU YUSUPH MAKAMBA, KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI KAPTENI JOHN CHILIGATI, NA WENGINE WENGI,

HIVYO BASI KUWA NA WANAJESHI WENGI KWENYE SYSTEM YA SIASA NDO INADUMAZA DEMOKRASIA YETU, KWANI UCHAGUZI WA MWAKA HUU UTAAMULIWA NA JWTZ NA SIO TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI-NEC NA WANANCHI WATAKAJITOKEZA KUPIGA KURA, KWANI USHIRIKI WA JWTZ NI MKUBWA SANA KUANZIA UGAWAJI NA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA KUPIGIA KURA. HIVYO HII INAONESHA KUWA SAUTI ZA MABADILIKO ZA WATANZANIA ZITAPORWA NA JWTZ KWA KUWATAKA KUKUBALI MATOKEO YA AINA YOYOTE NA KUWATISHA WANANCHI! HII NI HATALI KWA AMANI NA UTULIVU KWANI HALI KAMA HII IMEKWISHA TOKEA MATAIFA MBALIMBALI NA MADHARA YAKE TUNAYAJUA, PALE UMMA UNAPOAMUA KUFANYA MABADILIKO LAKINI KIKUNDI CHA MADIKTETA WACHACHE KUPORA USHINDI WA WANANCHI.

WATANZANIA WAKIFUMBIA MACHO KITENDO CHA JWTZ KUANDAA MAZINGIRA YA KUPORA USHINDI WA UMMA NA KUZIMA SAUTI YA UMMA NI DHAHILI KABISA TUNAWEZA KUWA TAIFA WAHANGA WA UDIKTETA WA JWTZ KWANI WANAJESHI WENGI WAMEJIINGIZA KWENYE SIASA NA WAKLIO JESHINI WANA MPANGO WA KUINGIA KWENYE SIASA KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI, TABIA HII YA JESHI KUINGILIA SIASA INAWEZA KUMFANYA JK KUWA DIKTETA, HATA 2015 JESHI LINAWEZA KUTENGENEZA MAZINGIRA ILI AENDELEE KUONGOZA, KWA KUTANGAZA HALI YA HATARI NA KUILISHA UCHAGUZI INDEFENETELY, HIVYO KUWA NA RAISI AMBAYE NI DIKTETA.

KITENDO CHA KANALI MSTAAFU JAKAYA MRISHO KIKWETE KUTUMIA JWTZ KUTOA VITISHO NA KUSHURTISHA WANANCHI KUKUBALI MATOKEO KABLA YA HATA KURA NA MATOKEO KUPIGWA NA KUTANGAZWA HIYO NI CONSPIRACY YA HALI YA JUU NA INAONESHA HULKA YA UDIKTETA YA KANALI MSTAAFU JAKAYA MRISHO KIIKWETE. HIVYO BASI NI MTU HATARI KWA USTAWI WA TAIFA HILII KWANI YUPO RADHI KUREJEA MADARAKANI KWA HILA NA DHULMA.

HIVYO TUPAMBANE NA HIZI HUJUMA ZA JWTZ NA TUMKATAE DIKTETA KANALI MSTAAFU JAKAYA MRISHO KIKWETE NA MASWAIBA WAKE.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA



KUTANA NA DICTATOR KANALI JAKAYA MRISHO KIKWETE NA VITISHO VYA JWTZ
 
Ni Luteni Kanali Kikwete sio KANALI mkuu....hakufikia hicho cheo kwa kuwa ali-abscond course kule Monduli....bado ni AWOL wa Jeshi
 
Kama hawajapigana muda mrefu waombe wapelekwe hapo Mogadishu kuna Alshabab. Waache raia wafanye uchaguzi wao kwa amani.
 
Hivi wanajeshi wa vyeo vya chini katika JWTZ wanajua jinsi makamanda wao wanavyotumbua maisha wakishirikiana na mafisadi walioko madarakani? Wao wanabaki kulala nje wakiwalinda makamnda wao wakiga wana nyara za taifa hili.Hivi ni kweli kuwa wakiamriwa watuuwe kwa sababu tunataka kuikomboa nchi yetu kwa njia za kura kutoka makucha ya wakoloni weusi CCM watatii amri haramu hii? KIKWETE AMESHA KUWA DIKTETA NA FASHISTI MKUBWA. Rejeeni yaliyotokea Ivory Coast, wanajeshi walimuambia bosi wao Gen. Henry Gaule kuwa hawataendelea kuuwa wananchi ambao ni baba zao,mama zao kaka zao dada zao watoto wao, eti kwa kulinda masilahi yake, walimuodoa, sasa na nyie wavuja jasho wa JWTZ mwambieni hivyo Shimbo na shoga yake Kikwete kuwa HAPANA, silaha hizo ni kwa ajili ya kuwalinda na si ku wadhuru.
 
jeshipolice.jpg
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo

Elias Msuya
MAMBO yalikuwa yametulia kabisa, lakini sasa yametibuka baada ya viongozi wa majeshi kuanza kutoa kauli za vitisho kuelekea uchaguzi mkuu.

Hivi karibuni, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo akiwa na baadhi ya viongozi wa jeshi la Polisi walitoa onyo kali kwa wanasiasa kujiepusha na vurugu wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu. Shimbo alidai kuwepo kwa dalili za kuvurugika kwa amani kutokana na taarifa za baadhi ya vyama vya siasa kujiandaa kukataa matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.
Alisisitiza kuwa hakutakuwa na umwagikaji wa damu na kuwa jeshi hilo litahakikisha kuwa amani inatawala wakati wote wa uchaguzi.

Pamoja na ukweli kuwa suala la amani ni la muhimu, siyo tu wakati wa uchaguzi, lakini hadi sasa sijaelewa lengo la onyo hilo la viongozi wa majeshi wakati huu.
Kwani kama jeshi limejipanga kulinda amani wakati wa uchaguzi, kuna haja gani ya kuwatangazia wananchi?
Badala yake naona Shimbo anatafuta maneno zaidi kwani sasa amejiingiza kwenye mijadala na wana siasa jambo ambalo hata yeye mwenyewe alikiri kuwa jeshi halihusiki huko.

Jambo jingine ninaloliona hapa ni upotoshwaji wa neno hili “Amani”. Baadhi ya watu (akiwamo Shimbo) wanadhani amani huja kwa kuwatisha watu kwa kuwaamuru kutii kila linalosemwa hata kama halina msingi.
Ndiyo maana Shimbo alisema kuwa ana taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya vyama vya siasa vimejipanga kukataa matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.
Hadi hapo mimi sioni dalili yoyote ya kuvunjika kwa amani, kwasababu mtu huwezi kukubali matokeo yasiyo sahihi eti ili tu kulinda amani.

Kabla sijaenda mbali, kwanza tuona maana ya amani. Nakumbuka mwezi Februari wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini, Jaji Mkuu Augustino Ramadhan alifafanua vizuri maana ya amani.
Alisema, (namnukuu) “Amani ya kweli ni pale haki inapotawala, vyombo vya dola havihitajiki, utunishaji wa misuli siyo lazima, bali wananchi wenyewe wanakuwa watulivu kwa sababu kila mmoja au wengi wao wanakuwa wamekinai.”
Kwa maana hiyo, Jaji mkuu, alimaanisha kwamba amani haiji kwa vitisho au kuwa na majeshi mengi, bali watu waridhike na kile wanachokitaka.

Sasa kitendo cha viongozi wa majeshi kutishia kuwa watahakikisha amani inadumishwa wakati huu wa uchaguzi, siyo dawa, tena wasipoangalia ndiyo itavunjika zaidi.
Kitu cha msingi wanachopaswa ni kuhakikisha kuwa kila mtu anaridhishwa na mwenendo wa uchaguzi. Tangu wakati huu wa kampeni, wakati wa kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo, watu waridhike.

Kama kutakuwa na upendeleo, au uvunjwaji wa sheria yoyote na vyombo vinavyosimamia uchaguzi tusitegemee kuwa na amani.
Hata kama majeshi yatafanikiwa kuwatisha wananchi, hiyo haitakuwa na amani bali ni ukandamizwaji wa haki za biandamu.
Ieleweke pia kwamba, vyama vya siasa au wagombea kupinga matokeo, siyo kosa na ndiyo maana zipo taratibu za kuwasilisha malalamiko yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi na mahakamani.

Ingawaje, sheria inakataza vyama au mgombea kupinga matokeo ya rais mara yanapotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hata hivyo haijazuia watu kutoa maoni yao kama iliyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nawakumbusha viongozi wa majeshi kuwa makini na matamshi yao katika kipindi hiki kwani badala ya kutibu yanaweza kuamsha ugomvi usiokuwa na sababu za msingi.

Tunakumbuka uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, aliyekuwa mkuu wa jeshi la Polisi, Omar Mahita akupokuwa akitoa kauli zenye utata dhidi ya vyama vya upinzani.
Aliwahi kusema kuwa “kama wao ni ngangari, sisi ni ngunguri’ akikiponda chama cha upinzani kilichokuwa kiktumia neno hilo.
Siku moja kabla ya uchaguzi akadai kuwa kuna visu na silaha nyingine zimekamatwa zikiwa na alama ya chama fulani cha upinzani.

Baada ya uchaguzi ule, Chama cha Wananchi, CUF kililalamika kuhujumiwa kwa kauli za Mahita.
Inatia shaka kuona viongozi wa majeshi ambao ni wateule wa Rais ambaye pia ni mgombea wa CCM wanapotoa kauli za vitisho kwa wananchi. Kauli hizi zinaweza kutafsiriwa kuwa ni maagizo ya mgombea huyo.

Wakati mwingine viongozi wa jeshi wanajipendekeza tu ili baada ya uchaguzi kupita au watakapostaafu wakumbukwe kwenye uteuzi wa nafasi mbalimbali serikalini, kama vile ukuu wa mikoa, wilaya au vitengo mbalimbali serikalini.
Viongozi wa majeshi wanapaswa kuwaachia kazi za propaganda wanasiasa. Hata kama wamegundua hali mbaya, wanapaswa kuwashauri viongozi wa serikali, badala ya kuanza kulumbana na wanasiasa.



Chanzo: Kauli za viongozi wa majeshi zinatia mashaka
 
Ni kibaraka wa JK huyu. Kwanza tayari ile deal ya power tillers inawaumiza wakulima tayari kwani ni bomu (Daily News 7/10/10). Sasa kwa kulia kwa wakulima namna hii Dr. Slaa akishinda Shimbo atapona kweli? Hiki ndio chanzo kiwewe chake.

Waziri Hussein Mwinyi anamtetea Shimbo kwa sababu naye anahusika kwenye deal hizi kwa namna moja au nyingine!
 
Kama watz tuliowengi tunataka amani ibaki, idumu na iendelee kudumu.
Mataifa mbalimbali hutafuta amani kwa njia ya gahrama kubwa.tz mungu ametupa.
kitendo cha wanaharakati kuanza kupayuka kuhusu amani yetu kinatutia mashaka
watu wenye kutunza amani ni vyombo vya usalama.
baadhi ya nchi wanaharakati huwa ndio chanzo cha migogoro na kuhatarisha amani.
baadhi ya mataifa wanaharakati wamewekewa sheria kali.
baadhi ya nchi baadhi ya taaisisi za wanaharakati zimefungwa.
nadhani sisi watz wenye amani tusifike Huko. lkn na sisi watz wanyonge tunaotaka amani tusikilizwe na wanaharakati. tunataka amani ilindwe na vyombo vyetu vya usalama.
leo hii kuna mtanzania anashatkiwa marekani. hakuna mwanaharakati aliejitokeza kuzungumza, hakuna alienyanyua mdomo. huyo ni mtanzania, amezaliwa tanzania

Amezaliwa Tanzania, akakulia Tanzania na kuwaua watanzania kama kuku (1998). wamechelewa kuua kwa sindano ya sumu. Ni impurity asirudi hapa
 
Huwa na wasiwasi kama huyu jamaa ni mtanzania halisi..!
 
sasa hapo ndipo mnaponiacha hioi? unauhakika gani alifanya yeye? sasa kama mnapiga kelele hizo? kwanini jeshi letu liszuie machafuko?

Kama siyo yeye ni watu wanaofanana naye. Kusaidia kufanikisha mpango ndio kushiriki kwenyewe. Auwawe kwa kiti cha umeme. afadhali ya mafisadi wa CCM wanatuachia miili zetu kuliko yeye anayeteketeza uhai na miili
 
Nimeamini huyu bwana ana matatizo ya akili, amani inaanzia kwenye moyo wa mtu, kama hakuna amani moyoni mwako hata wakija na vifaru haitapatikana!
 
Kama watz tuliowengi tunataka amani ibaki, idumu na iendelee kudumu.
Mataifa mbalimbali hutafuta amani kwa njia ya gahrama kubwa.tz mungu ametupa.
kitendo cha wanaharakati kuanza kupayuka kuhusu amani yetu kinatutia mashaka
watu wenye kutunza amani ni vyombo vya usalama.
baadhi ya nchi wanaharakati huwa ndio chanzo cha migogoro na kuhatarisha amani.
baadhi ya mataifa wanaharakati wamewekewa sheria kali.
baadhi ya nchi baadhi ya taaisisi za wanaharakati zimefungwa.
nadhani sisi watz wenye amani tusifike Huko. lkn na sisi watz wanyonge tunaotaka amani tusikilizwe na wanaharakati. tunataka amani ilindwe na vyombo vyetu vya usalama.
leo hii kuna mtanzania anashatkiwa marekani. hakuna mwanaharakati aliejitokeza kuzungumza, hakuna alienyanyua mdomo. huyo ni mtanzania, amezaliwa tanzania

Akasaidiwe na Al Qaeda
 
Back
Top Bottom