Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

AK-47

JF-Expert Member
Nov 12, 2009
1,373
199
[FONT=Arial, sans-serif]Hii nimeipata sasa hivi
[/FONT]
Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vimewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC na kutothubutu kupinga matokeo hayo na kusababisha vurugu.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Luteni Jenerali Abdurahmani Shimbo ametoa tamko hilo leo Jijini Dar-Es-Salaam kufuatia kuwepo kwa taarifa za vyama vya kisiasa kujiandaa kukataa matokeo yatakayotangazwa na tume ya uchaguzi.

Luteni Jenerali Shimbo amesema vyombo vya usalama vimejipanga kukabiliana na hali yoyote ya vurugu ambayo itajitokeza na kuwaonya watu kutoshiriki katika vurugu zozote baada ya kutangazwa matokeo.
 
Tuliona nchi kibao Wanajeshi wakitishia na kuuwa watu. Kama watu wamechoka basi hilo wala halitasaidia.

Hata Warusi na Roho mbaya zao bado walinyenyua mikono na kukimbia kama Jogoo lililodundwa....
 
Mbona yaliyotokea ULAYA Mashariki yana-prove Lt Gen Shimbo wrong?

People's Power care less on any Military intimidation!
 
CCM nao watangaze kuwa watakubali matokeo. Siyo hizi kauli za ushindi at any cost.
 
Hii kali, ina maana mwaka huu uchaguzi utalindwa na jeshi? Huku ni kufilisika kifikira, ni wehu, ni uendawazimu au ni kitu gani? Who is Shimbo katika mambo ya uchaguzi? Ina maana Mwema amestaafu. Atuondolee uchuro wake hapa. Yaani JWTZ ndiyo inayoshughulikia usalama wa uchaguzi? Kwani IGP anafanya nini? Ameshindwa kukamata maharamia wa Somalia na wahamiaji haramu anataka kushughulika na uchaguzi. Hii serikali ya Kikwete kweli imepinda!! Kama ndiyo hivyo, bora tu tuingie vitani wasitubabaishe hapa tushachoka na mfumo wa kibepari na kandamizi wa CCM.
 
Hii kauli ya shimbo inakihusu zaidi chama cha ccm kwani ndio chama chenye kauli mbiu kwamba ushindi ni lazima. Maana yake ni kwamba hata wakishindwa hawapo tayari kukubali matokeo. Ccm mwaka huu imeshikwa pabaya kiwewe kimewaingia, hawawezi tena hata kupambanua lipi ni lipi. Jeshi la Tz ni la wananchi hivyo halina budi kuyaheshimu matakwa ya wananchi. Likinasa katika mtego wa kikundi cha watawala wachache basi lijue linakosa ridhaa ya wananchi na hivyo lijiondoe kabla ya kuondolewa na nguvu za wananchi hao hao.
 
Wameona hawajapigana muda mrefu toka Idd Amin sasa wanataka kuanzisha vita na wananchi wanaowalinda. Ila hawa jamaa si wapo jirani na yule mwenye kipetupetu inawezekana jamaa kamtangazia kuingia msituni kama Makame akimzingua kumtangaza!!! Hahaaa, kanyaga twende no retreat no slender"
 
Inakuwaje jeshi linajitokeza katika hili ilhali nafasi yake ni kwenye mipaka na usalama wa taifa dhidi ya maadui wa nchi?

Kwendeni zenu huko, na aliyetoa tamko hilo ni mwehu!!! akapimwe akili
 
Hao wakina Shimbo wameshiba hela ya JK, hawana shida.

Yeye ansema haya kama nani? IGP yuko wapi? Katika hii nchi watu wamelewa maisha ya kifisadi ya JK.

Watawapiga CCM tu, this time NO to JK & CCM
 
Mbona wanaanza kuvuka mipaka ya utawala waliojiwekea?????. Hiyo si kazi yao kuna wahusika wa kupiga virungu ni polisi ndo tunawajua JWT msitutishe.Hawa jeshi la wananchi kazi yao kulinda mipaka.Mambo ya ndani wamuachie Masha.Na wajue kwamba tanzania ya leo si ya kutishana na kudanganyana.Naona pressure inapanda pressure haishuki tena.HATUDANYIKI
 
Unajua utawala wa JK umekuwa kama ulimwengu wa Kambale ata kakambale kadogo nako kanazaliwa kana tundevu.
Yaani hakuna discipline kabsaaaaaaaaaaaa.
Yaani mtu akishahongwa anabwabwaja tuu bila kujari anaongea nini na wapi?
Kama mna hamu ya kupigana si mwende somali au sudani.
Naona tukishazipiga Tz ndo discipline itakuwepo
 
CHADEMA wamshashinda vita, kwani wameweza kujua jeshi la adui lina silaha gani. Pia baadhi ya silaha adui ameshazitumia na zimegundulika ukali wake na ANTI-yake imetayarishwa naDr.Slaa na kutolewa kwa wannachi na viongozi wa dini silaha hizo ni.
  • Waraka kwa wakuu wa serikali za mikoa, wilaya na halmashauri
  • Maagizo kwa TISS/UWT
Silaha iliyokuwa imebaki ni kuwatisha wanachi kupitia JWTZ imetoka leo.CHADEMA wakipata Anti-ya hiyo silaha baaasi kwishaaaaaaa kaziiiiiiiiiii
Mwaka huu ya Zanzibar yanahamia Bara.Kwa uwezo wake Bwana Yesu watashindwa na tutakuwa huuuuuuru
 
Who is shimbo anyway!kibaraka wa jk,hajui humohumo jeshini kuna chadema,cuf,ccm na wasio na vyama?kuwa mwanajeshi hakuondoi ukweli hata wao ni binadamu kama sisi.na wasijidanganye askari wa kweli tunao mtaani...kama wanaweza wakapambane na wasomali tuone,wenyewe wakalia kutunisha vitambi tu.
 
Kwani mmesahau kuwa JK alikuwa mujeshi kabla ya kujikita katika siasa. Sasa wana wenzake wanamkazia buti jamaa asijeanguka!
 
Tutawashitaki kwa wakuu wa madhehebu yetu kwani wao ndiyo walezi wetu kiroho na kimwili.umuhimu wa jeshi ni mdogo sana kwetu kulinganisha na wachungaji wa kondoo wa bwana.Bwana yesu asifiwe Daimaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom