Kuelekea Tanzania ya Viwanda PSPF kujenga mji mpya wa kisasa Singida kuvutia wawekezaji

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Katika uchaguzi Mkuu Rais wa Tanzania Dr Magufuli aliahidi kuubadili Mkoa wa Singida na kuwa mji wa kibiashara kama ilivyo Dubai kwani ni mji pekee ambao upo katikati ya Tanzania unaounganisha Mikoa yote kwa Barabara.

Katika kufanikisha Mkoa wa Singida kuwa center ya Biashara PSPF imeamua kujenga mji mpya wa kisasa katika manispaa ya Singida ambao ujenzi unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo katika mwaka huu wa fedha kwani eneo la ujenzi lenye zaidi ekari 200 zimepatikana na kuwekewa mipaka

Mji huu unatarajiwa kuvutia wawekezaji wa Viwanda katika Mkoa wa Singida na wafanyabiashara wakubwa

wahi fursa ya kukua na kutajirika na Mkoa wa Singida ambao unatarijiwa kuwa mji mzuri zaidi kuliko Arusha, Dar, Mwanza, Dodoma na Mbeya. Wekeza katika Mkoa wa Singida kwa maendeo ya haraka
 
Aisee kama wamefanya analysis nawakaona payback period na return in investment italipa basi sawa.
 
Singida??...bora wakajenge arusha au mwanza...uko pakame nan ataenda...wanapoteza pesa yao bure
 
Habari njema hii, mpaka sasa Singinda kuna viwanda Vya Alizeti.

Lkn najua Nyumbu Wa ufipa kwa kuwa wameapa kupinga kila kitu, watakuja kupinga hili wazo zuri
 
Singida wameliwa,pesa IPO northern circuit bora wangefanya manyara.Sasa sijaelewa wanajenga viwanda au watajenga epz yao watu wakawekeze au watauza viwanja etc???
 
Mhhh!
-Tanzania ya Viwanda na mji wa kisasa?,mi nikajua labda kuna viwanda vinajaanzishwa huko

-Mji wa kisasa kwa ekari 20,huo ni mji wa kisasa au mtaa wa kisasa?
 
Kwahiyo kwa akili yako ekari 20 zinajenga mji wa kisasa? Kwa singida wanapoteza hela yao badae waje wawadhulumu wafanyakazi wanaodai mafao yao bure mana hawatarudisha hela yao
 
Bora wangeanza na Kigoma , reasons: epz wameanza ujenzi, bandari kubwa ya kissasa inajengwa kibilizi, bandari kavu inajengwa kupokea mizigo ya DRC na Burundi, kiwanja cha ndege kinapandishwa hadhi kuweza kupokea Ndege nyingi etc, nawahi Kigoma, nitakuwa mwenyeji wenu.
 
Bora wangeanza na Kigoma , reasons: epz wameanza ujenzi, bandari kubwa ya kissasa inajengwa kibilizi, bandari kavu inajengwa kupokea mizigo ya DRC na Burundi, kiwanja cha ndege kinapandishwa hadhi kuweza kupokea Ndege nyingi etc, nawahi Kigoma, nitakuwa mwenyeji wenu.
yaan huko ndo kwenyewe ila watu jawajui tu
 
MNA maliza pesa zetu mwisho wastaafu wanakosa pesa zao.wewe unajenga singida wapi na wapi yangu link.Dodoma tu bado issue.chukueni mawazo ya raid wetu.wekezeni kwenye viwanda na siyo Majengo na madaraja .viwanda utazalisha na utaajiri watu
 
NSSF wameshindwa Kigamboni, ndiyo itakuwa PSPF singida, hayo yatakuwa maajabu ya dunia
 
Back
Top Bottom