Kuelekea Siku Ya Posta Duniani, 09 Oktoba 2021

Sep 13, 2016
49
23
MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE KUFIKISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJINI.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Bi Justina Mashiba ametoa taarifa fupi ya kazi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote katika semina kwa watoa huduma za Mawasiliano.

Semina hiyo imefanyika Jijini Dodoma katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta duniani huku Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Semina hiyo akiwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi.

Bi Justina Mashiba amesema kuwa mwaka 2006 Serikali iliona Kuna haja ya kupeleka Mawasiliano Vijijini hapo ndipo ulianzishwa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Serikal ilitunga Sheria na Mwaka 2009 ikatunga kanuni ambazo zitaongoza Mfuko huo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ulianza shughuli zake za kupeleka huduma za Mawasiliano Vijijini.

Katika kipindi cha miaka 10 Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umefanya mambo makubwa katika kuboresha na kufikisha huduma za Mawasiliano Vijijini. Mpaka kufikia mwezi disemba 2021 mfuko wa mawasiliano kwa wote utakuwa umewafikia watanzania milioni 12.9 kutokana na miradi mbalimbali inayotekelezwa na mfuko huo.

Kwa upande wa Shirika la Posta Mfuko umetekeleza miradi mbalimbali inayohusiana na Posta. Lakini pia Mfuko una jukumu la kuhakikisha watoa huduma za vifurushi ambao wamesajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)wanafika Vijijini.

"Tulianzisha mradi mmoja wa kutengeneza njia za kuwezesha kufikisha mizigo, kama mnavyojua wizara yetu ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ina mradi wa anwani za makazi, lakini mtu anafikaje huko? Tulifanya kazi na wenzetu wa posta na kutengeneza ramani ambayo itawezesha makazi kufikiwa kwa urahisi na ramani hiyo itatumika kwa watoa huduma za mawasiliano wote." Alisema Bi Justina

Aidha Bi Justina ameendelea kwa kusema mbali na miradi hiyo pia waliweza kushirikiana na Shirika la Posta katika miradi ya TEHAMA.

" Tumeshirikiana na wenzetu wa Posta kupeleka vifaa vya TEHAMA kwa watoto walio Vijijini ili kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali kama vile matokeo ya mitihani yao na kupata habari mbalimbali kwenye vituo vya Posta, Tumewezesha vituo 10 vya Posta vifaa vya TEHAMA na vinafanya vizuri" alisema Bi Justina
IMG-20211008-WA0053.jpg
 
Tumeshirikiana na wenzetu wa Posta kupeleka vifaa vya TEHAMA kwa watoto walio Vijijini ili kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali kama vile matokeo ya mitihani yao na kupata habari mbalimbali kwenye vituo vya Posta, Tumewezesha vituo 10 vya Posta vifaa vya TEHAMA na vinafanya vizuri" alisema Bi Justina
 
Back
Top Bottom