Cicero
JF-Expert Member
- Jan 20, 2016
- 2,924
- 3,072
Juzi katika pita pita zangu mjini, nikaona agizo la serikali la kutumika kwa nembo (bendera na wimbo) za Afrika Mashariki katika ofisi zote za serikali limetekelezwa vizuri. Ofisi za wizara zote hivi sasa ukiangalia pembeni mwa bendera ya taifa utakuta bendera ya Afrika Mashariki nayo inapepea. Tulivyoingia ndani kabla ya kuanza kikao ukapigwa wimbo wa taifa wa Tanzania then wimbo wa Afrika Mashariki.
Kama mtanzania na mwana afrika mashariki, nilifurahishwa sana na hilo, na ni vyema nikatoa pongezi za dhati kwa serikali ya awamu ya tano kwa hatua hiyo muhimu.
Haipendezi kuona Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza kuridhia itifaki ya umoja wa fedha wa Afrika Mashariki wakati watanzania walio wengi hawajui hata bendera wala wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Isitoshe, mchakato wa kuandikwa katiba ya shirikisho la kisiasa uko full speed!
Kazi bado ni kubwa, na ni vyema serikali ikaendelea na kasi ii hii tutafika tu!
PROUDLY EAST AFRICAN!