Uchaguzi 2020 Kuelekea Oktoba 28, kwenu Makamanda na wana Mapinduzi wote

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,226
35,151
Mabibi na mabwana baada ya salaam:

Mapinduzi

Sasa niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuelekea Oct 28 sote na tujiandae kusikia mengi. Kama wanavyolipwa kina konde na kina baba tiffe, huku mitandaoni hali kadhalika.

Propaganda za kila aina zitakuwapo na hasa baada ya bashiri kutambua kuwa hawana hoja yoyote kujibu kiu iliyopo ya haki, uhuru na maendeleo. Itambulike kuwa matatu haya ndiyo ulio msingi imara wa sera za CHADEMA na ACT_Wazalendo.

Kimsingi vyama viwili hivi ni mwamvuli pekee thabiti wa kutuvusha. Kelele zilizopo tokea huu upande wa pili ni jitihada zilizoshindwa za kujaribu kututenganisha.

Hatudanganyiki!

Wanaolengwa ili kujenga hofu na ikibidi wasambaratike au tusiwaamini ni miamba wetu hawa wanne:

1. Lissu
2. Maalim
3. Zitto
4. Kachero mbobezi

Wote kwa pamoja, mmoja mmoja, wawili au watatu, haba na haba hujaza kibaba. Wanataka utengano wa kuwaondoa kwenye imani zetu.

Kwa hilo mbinu ni nyingi zikiwamo hata za kuanzisha nyuzi zisizokuwa na mbele wala nyuma kutuondolea umakini. Hii ikiwamo kuzuka zuka hata vinyuzi nyuzi kama vile vya kula yale mananihii kimasikhara.

Lengo kuu ni moja, kuliondoa gari Moshi kwenye reli. Chochote cha kututoa kwenye habari hii pevu ya ukombozi kwao ni silaha halali ya kutumia. Watatumia kila kitu kwenye hilo.

Mwenye macho haambiwi tazama. Ila ni muhimu wajue mchezo wa safari hii si ndondo tena. Safari hii twala wote sahani moja!

Makamanda na wana mapinduzi, tusikubali kucheza wala kuchezeshwa ngoma zao hizi za kitoto na bila tafakuri ya kutosha. Hawana lolote wala uwezo wa kutosha kupambana na nguvu ya umma inayoratibu mikakati ya ushindi safari hii.

It's either now or never. Huyu bwana akituponyoka hapa, miaka mitano ijayo haitakalika.

Sasa basi ni basi kweli kweli. Kwanza wawarejeshe waenguliwa wote na bila ya masharti yoyote.

Misimamo na mielekeo kamili itatolewa tokea katika ngazi rasmi za vyama hivi na si vinginevyo.

Kwamba kuna waliokatika malipo kutuchanganya? Kwamba kuna na maafisa vipenywa ndani yetu? Mbona yanajulikana kama tulivyo nao wetu kwao?

2020 tunakwenda na uhuru, haki na maendeleo. Treni la Sayuni halina simile.

Viva Lissu, Viva Maalim, Viva ZZK na Viva Membe.

Wameshikika vilivyo tunayoona sasa ni zaidi ya kuweweseka.

Na bado!
 
Walioenguliwa warudishwe wote tusimame na hili kidete.

Kukudokeza tu wakiguswa kwenyewe wote buku 7 na buku 7+ wapya wa bashiri si kununa na kufura kwa hasira.

Ikumbukwe kuwa walioenguliwa hawatarudishwa bila ya kuwapo kwa dhamira halisi kutoka kwetu kuwa we mean business.

Ni kumaanisha biashara huko ndiko kuliko pelekea mapokezi ya amani JKNIA, salama inayoendelea leo na pia hata tume kuridhia wagombea kama kina Tundu Lissu kuwapo bado kwenye orodha hadi sasa na pia kina Juma kuendelea kutulizana.

United we stand.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom