Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,582
Wanabodi,
Jumamosi ya leo, nimepata fursa kuangalia mjadala wa 'Jicho Letu Ndani ya Habari" unaondeshwa na Star TV kila Jumamosi asubuhi, kipindi kikiongozwa Dotto Emmanuel Bulendu kule Mwanza, na Angalieni Mpendu kwa Dar es Salaam, ambapo mmoja wa waalikwa, mwandishi mkongwe, Dereck Murusuri, amesema wazi, kuwa japo haijaandikwa popote katika vitabu vya waandishi, lakini tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, ufike wakati vyombo vya habari vitangaze wazi kuunga mkono upande fulani, au kumuunga mkono mgombea fulani, na akatolea mfano mchini Uingereza wakati Tony Blair akigombea kupitia Labor Party, alimuomba Rupert Murdoch (Reginald Mengi wa UK) media yake imuunge mkono, na kwenye Murdoch akakubali, wakatangaza rasmi kuwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Rupert Murdoch, ikiwemo TV ya Sky News na Fox News, magazeti ya The Sun, The Times (London), The New York Post, The Wall Street Journal, The Daily Telegraph, The Herald etc na ndiye mmiliki wa kampuni ya filamu ya 20th Century Fox vinamuunga mkono Tony Blair na kuunga mkono Labor Party.
Hapa Tanzania tayari gazeti ya Uhuru, Daily News na Habari msimamo wao unajulikana, gazeti la Tanzania Daima linafahamika na Gazeti la Mtanzania pia linajulikana lina simama na nani.
Kwa upande wa TV, TBC inajulika inasimama na nani!, jee huu sasa ni wakati wa Media za Tanzania to declare interest wazi wazi kwa kufanya endorsement ya wagombea urais kama wafanyavyo media za UK na US?!.
Mzee wetu Reginald Mengi aombwe rasmi kutangaza kuwa media zake zinamuunga mkono mgombea fulani?!
Mada kuu ilikuwa ni kwa nini media hazisemi ukweli?, Dereck Murusuri amesema hakuna ubaya media zikijitokeza waziwazi kuunga mkono mgombea fulani kwa ukweli na uwazi kuliko kuuunga mkono kimya kimya kama hali ya meia zetu ilivyo.
Jee is it the right time sisi watu wa media to take sides, ili ikibidi hata mimi Pasco wa jf, nijiunge na chama cha siasa, tutangaze wazi wazi misimamo yetu, tumpeleke 'mtu wetu' ikulu ya Magogoni?!.
Nawatakia Jumamosi Njema.
Pasco