Kuelekea NEC ya CCM Dodoma-Ajenda zafichwa

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Taarifa nilizopokea ni kwamba NEC ya CCM itakutana Dodoma kwa dharura kujadili kuhusu Kilimo. Wadadisi wa mambo wanasema kitendo cha kutanza kwa umma kuwa ajenda ni Kilimo ni katika kupunguza mjadala wa umma kuhusu kikao hicho kama ilivyokuwa kwa kikao cha Butiama. Lakini wachambuzi wa msingi wanasema ajenda zitakazojadiliwa ni Hali ya Maisha ya Watanzania baada ya kupanda kwa Bei ya Mafuta na Chakula, Tishio la Njaa, Suala la Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar-hatma ya kura za maoni, Ripoti ya EPA, na Ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Pinda kuhusu Richmond. Kwa mujibu wa Mjumbe mmoja wa NEC, kuna kundi la wajumbe lina nia ya kushinikiza maamuzi ya kihistoria katika kikao hicho

PM
 
Asante Paparazi Muwazi kwa kututonya kuhusu hili. Nimefurahi kusikia kuwa kuna kundi la wajumbe wa NEC ambao wana nia ya kushinikiza maamuzi ya kihistoria katika kikao hicho. Je ni kuwatimua mafisadi, kuua Azimio la Zanzibar na kufufua Azimio la Arusha, kurekebisha katiba ya CCM kuhusu kipindi cha Mgombea wao wa Urais wa Zanzibar na Muungano (one term, two terms)???. Yetu masikio na macho.
 
Ni kujihami baada ya mwaswahiba wao maaskofu kuanza kuonesha dalili za kuwachoka hao CCM?
 
Hiki ndiyo kile kikao kilichokuwa na agenda ya siri ambacho kilitakiwa kufanyika mwezi Mei... nadhani zaidi kuna yale ya Benki Kuu zaidi..
 
I wish sisiem wangetufanya tuache kuishi maisha ya wishes!
 
Hawana jipya wameishiwa posho ndo maana wanaitisha kikao.Maswala ya msingi ya kuzungumzia na kuyatekeleza hawana kabisa hawa.
 
Hawana jipya wameishiwa posho ndo maana wanaitisha kikao.Maswala ya msingi ya kuzungumzia na kuyatekeleza hawana kabisa hawa.

Mkuu nakubaliana na wewe, lakini Wtz tumezoeshwa kuishi kwa matumaini ingawa si malezi mabay lakini tabia hiyo ikizidi tunaweza kuwa kama Wazimbambwe - Mugabe mmoja anafanya atakalo na hakuna wa kumuuliza.

Naamini CCM hawana jipya sijui lini tutaamini kuwa hiki chama kamwe hakitafanya maamuzi ya kujenga nchi hii.
 
Back
Top Bottom