Kuelekea msimu wa sikukuu; nawakumbusha watumiaji wenzangu

Oct 5, 2015
88
476
KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU; NAWAKUMBUSHA WATUMIAJI WENZANGU.

Kanuni za kunywa mvinyo kistaarabu
"Mvinyo ni kama maisha kwa watu, ukinywa kwa kiasi. Maisha yafaa nini bila mvinyo? umeumbwa ili kumpa mwanadamu amani ya nafsi" Sirah 31:27

Kanuni 1. Know your type/Tambu aina yako.

Kama unakunywa bia, kunywa bia ya aina moja. Kama unakunywa wiski, kunywa wiski ya aina moja unayoipenda, kama ni spirit, au Gin au Grants unywe hiyo. Ukitaka mchanganyo (Cocktail) hakikisha una utaalam wa kichanganya au umechanganyiwa na mtaalam. Au unaweza kuchanganya vitu visivyo na kilevi unavyojua; mfano matunda (nanasi, chungwa, berries, lemon), Whiskey sour, ice, Ginger highball, Bourbon Vanilla shake, Mint Julep, Irish cofee nk.
Jambo la msingi hapa ni kutokuchanganya mavitu usioyajua! kumbuka; pombe ni kemikali, unapochanganya bila utaratibu unaweza kutengeneza kemikali zenye madhara makubwa.

Kanuni 2. Know your Limit/Tambua kiasi chako

Kwani wewe unalewa ngapi? au Mizinga mingapi? jitambue! kipindi hiki cha sikukuu ni kipindi hatari kwa watumiaji, kama ilivyo kipindi cha kampeni kwa wanasiasa. Ni vema ukatambua kiasi chako ili ukishaona mabadiliko unachukua stahiki. Kama ni kukabidhi funguo za gari, kama ni kutoa taarifa nyumbani kwamba upo mahali flani, kama ni kulegeza mkanda wa kiuno utajua mwenyewe. Vizuri ni kuachia hapo, lakini kama hutapenda kufanya dhambi ya kuachia njiani, basi ni vema ukajiandaa kwa uslama wako, ili ukizima ujue unafanya nini.

Kanuni 3. Know your place & Company/Tambua ulipo na tambua kampani lako

Unakunywa wapi? baa gani, chimbo gani? na kina nani? Ni lazima kutambua mazingira salama kwa ajili ya mvinyo. Obvious, unahitaji marafiki lakini ni vizuri wakawa marafiki wa muda mrefu (old friends). Wale washkaji sawa na kaka au dada yako. Na bila shaka wamewahi kukubeba wakati fulani ulipozima, au uliwabeba! Au wameshawahi kusafisha matapishi yako wakati wewe ukiwa hujitambui. Na, ulipostuka ulijikuta salama. Hao ndio watu wa kunywa nao msimu huu! Sio wale washkaji walikuachaga mwenyewe ukastuka huna kitu mfukoni! hao ni masnichi, wateme. ujue sisi watumiaji tupo kama jeshi, hatupaswi kutupana. Lakini muhimu zaidi, ujue location, kariri longitudes na latitudes za hapo ulipo, Greenwich's line ipo east au west? equator ipo south au north? You got to know that; kwa sababu hao ulio nao hata kama ni baba na mama, nawo si wanatupia? eeh! lolote laweza kutokea. Sasa ukishajua mahali ulipo, ukishachora ramani yako basi una-relax. likitokea ka kutokea unajua pa-kutokea. Na ukumbuke pia, kanuni hii sio kwa faida yako tu, bali pia kwa faida ya hao ndugu zako katika mvinyo. Msaada unaweza kupewa, au wewe kutoa msaada, yote yanawezekana.

Kanuni 4; Know your Time/Tambua muda wako/ratiba yako

Unakunywa muda gani? Kuna majamaa yapo likizo sasa hv na hayana -homework, hawana familia. waache wajidunge wanavyotaka ila ukipata wasaa wakumbushe kanuni hizo hapo juu. Pengine kanuni hii haiwahusu! Inakuhusu wewe mwenye familia, kibarua/ajira/kazi na mipango mingi mizuri ya baadae. Lakini maisha yafaa nini bila mvinyo? Kwa hivyo ungependa kupata kwa kiasi, damu ya mkombozi. Katika mazingira hayo, basi ni vema ukakumbuka ratiba yako. Maliza malengo yako ya siku, maliza kupanga malengo ya kesho, kisha jiachie! na ili kesho uamke vizuri, kumbuka kuzingatia kanuni zingine zilizopita, ili ndoto zako zitimie kwa wakati.

Mambo mengine ya msingi.
1.Chakula! Kula chakula cha kutosha hasa hasa , ugali, nyama, mchemsho, matunda ya kutosha na maji mengi, kisha pumzika kwa muda, halafu anza kulipa kodi.

Mchanganyiko wa matunda unaweza kwenda sambamba na kinywaji chako kama upo nyumbani. Matunda yanarudisha maji na vitamin zinazopotea unapokunywa pombe.

2. Mazoezi; mazoezi ya viungo vya mwili ni muhimu kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na kuondoa sumu ikiwa ni pamoja na masalia ya kemikali zilizopo kwenye pombe. Lakini pia mazoezi yanakupa uwezo wa kuvumilia kiasi kikubwa zaidi cha pombe, na kuisafisha mwilini kwa haraka zaidi.

3. Afya; Tafadhali, hata kwa kufuata kanuni hushauriwi kutumia pombe kama una changamoto za kiafya kama kisukari cha muda mrefu, mgandamizo wa damu kwa muda mredu, matatizo ya figo, moyo nk.

Nyongeza.
Pombe inakupa uhai mwanzoni, inakuchangamsha (stimulant) na ukizidisha inakuzubaisha/kukulevya (depressant), na kukusahaulisha maizingira uliopo na kukupotezea kumbukumbu (Amnesia)
Pombe inaongeza dalili za vidonda vya tumbo
Pombe inahusigwa na kansa nyingi, ikiwemo kansa ya ini, tumbo, utumbo nk.
Pombe inahusishwa na kufeli kwa figo (renal failure) na matatizo ya moyo (alcohol Cardio-myopathy)
Pombe inaweza kupelekea kuishiwa maji mwilini.

kumbuka! unaweza kufa bila kuwa na matatizo hayo hapo juu! usitafute kisingizio cha kutokulipa kodi.

"Ulevi, huongeza hasira za mpumbavu na majeraha, humpunguzia nguvu na kumuongezea vidonda" Sirah 31:30

Nawatakia ulevi mwema usio wa kipumbavu
Asante!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom