Ndugu zangu wahandisi watanzania "Local Engineers" tunapoelekea kwenye mkutano wa wahandisi wa mwaka utakaofanyika tarehe 29 na 30 mwezi huu tuwaze kuwa na chombo kinachoweza kutukutanisha sisi wahandisi wazalendo tujadili changamoto zetu tutizame ni kwa namna gani tunaweza kuzipatia ufumbuzi.
Binafsi huwa inaniuma sana pale ninapotazama vyombo vya habari nikasikia mtu fulani ametengeneza kitu ambacho kinachukua attention za vyombo vya habari lakini hawa wote huwa ni wale "mbumbumbu" kwenye sekita ya uhandisi kwa maana ya wote wanaochukua heading za kuvumbua vitu vya kihandisi ni darasa la saba. Sijawahi kusikia mhandisi amevumbua au kutengeneza kitu chochote. Huwa najiuliza hivi wahandisi watanzania tuna tatizo gani? Je ni kweli hatuwezi au kuna mazingira ambayo hayajakaa sawa na sisi wenyewe tunaona tatizo liko wapi? Ukitazama nchi kama china, india n.k unaona products za kihandisi za kufikirisha lakini sisi hakuna kitu.
Mimi Binafsi nimefanya kazi kwenye Construction industry kwa Karibia miaka 15, kuna mambo mengi nimejifunza kupitia sekita hii ambayo pengine watunga sera wanayaona kwa mtizamo tofauti na mimi niliyeko site. Kila mhandisi yuko kwenye sekita yake pengine kwa miaka kadhaa na wengine sekita tofauti na kila mmoja aliko anaiona sekita hiyo kwa mtizamo tofauti na walioko nje ya sekita hiyo. Ni wazi kuna haja ya sisi kukaa pamoja kujadiliana changamoto zetu na fursa zetu tuone tunaweza kwendaje mbele.
mfano
1. Wakulima wamewekewa Dirisha TIB, je Sekita kama ya Ujenzi "Construction" kweli hahiitaji dirisha TIB? au kuundiwa benki ambayo inatoa dhamana Bonds kwa wadau, inatoa mikopo kwa utaratibu maalumu kama kuwalipa suppliers wa materials n.k
2. India wakitoa mkopo kwetu katika ujenzi wanatubana wakandarasi, materials, washauri wanatoka kwao, yaani mataifa mengi ya nje yakitukopesha yanatubana vifaa mnanunua kwao au kwa washirika wao na services hivyo hivyo. Hatuna tatizo na hili ila tatizo letu ni kuona fedha zetu wenyewe hazijawekewa utaratibu. Sisi tukikusanya kodi zeti, tukikopa benki ya maendeleo ya afrika bado kazi hatutoi kipaumbele kwa watu wetu na vitu vyetu, wakandarasi watatoka nje, bidhaa zitatoka nje hata kama hapa nchini nzinazalishwa. Sisi wahandisi tuko field tunaona kila kinachofanyika kwa mataifa ya nje na wanakifanya kwa staili gani na tunao uwezo wa kutoa mapendekezo yetu kwa watunga na wasimamia sera nini cha kufanya kwa wakati gani katika hili.
3. Wahuni ndio wanabeba taswila ya wahandisi tanzania. Sekita kama ya ujenzi ni sekita ambayo ina fedha nyingi sana zinazonguka huko hasa kutoka serikalini. Fenzi kuwa nyingi kumevutia watu wengi hasa wahuni wanaoona huku kuna fedha na wanafanya kila namna kuzichota fedha hizi. wahuni hawa wamekuwa wakifanya ujanjaujanja mwingi tu, lakini ujanjaujanja huu wanaoufanya unabaki kuwa matope kwa wahandisi hasa wazalendo. Kila viongozi wakisimama kwenye majukwaa ni kuonyesha kutokuwa na imani na sisi, kila mwananchi wa kawaida akiongea ni kuonyesha wahandisi wazalendo hamna kitu. Sisi wahandisi tulioko kwenye sekita hizi tunajua matatizo yako wapi na tunaweza tukikaa pamoja kutoka na mapendekezo yatakayo turejeshea heshima na kuaminika na mbinu za kuwadhibiti wahuni wanaotuchafulia taaluma yetu.
4. Kila mwaka serikali hutoa fedha za tafiti, ni kwa bahati mbaya sana hatuoni bidhaa za kihandisi zenye kufikirisha. Labda niulize ni taasisi gani hapa nchini ambayo mhandisi anaweza kukaa mitaani akifanya shuguuli zake, akapata mawazo ya kuboresha jambo fulani au kutengeneza kitu kinachofanana na vile vinavyotengenezwa nje akakubaliwa kudhaminiwa? Taasisi tunazoziona ni zile za kufundisha na hawa wameweka ukiritimba kuwa tafiti zinafanywa na wanataasisi tu. Sasa zile product fikirishi watu wazibuni kwa fedha zao za mfukoni ?
Yapo mengi ambayo wahandisi wazalendo tunaweza kukaa kujadili na tukabadili taifa letu kiuchumi tunahitaji kuunda chama cha wahandisi wazalendo, Local Engineers Association in Tanzania (LOEAT) Tukutane mkutano wa wahandisi 29/30