Kuelekea mkutano wa CCM Dodoma, polisi yamiminika makundi kwa makundi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287

Jeshi la Polisi limeongeza askari na vifaa vyake Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM ambao unatarajiwa kumchagua Rais Magufuli kama Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Awali baraza la vijana wa CHADEMA walisema wangelisaidia jeshi la polisi kuzuia mkutano huo ili kuunga mkono kauli ya Magufuli ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, lakini kamanda wa polisi wa mkoa huo Lazaro Mambosasa akasema hawaitaji msaada na watawasweka ndani wote watakaoingilia mkutano huo
 
Huko ni kuwatisha vijana vita vina mbinu nyingi sana ili kuhakikisha ushindi.
Hii video nani kaishut kama si wao wenyewe na kuitupia huku ili kuwaogofya vijana.
 
Katika nchi yoyote, kulinda chama tawala is very much costing. Lakini hapohapo Historia huwa haidanganyi......
 
Huko ni kuwatisha vijana vita vina mbinu nyingi sana ili kuhakikisha ushindi.
Hii video nani kaishut kama si wao wenyewe na kuitupia huku ili kuwaogofya vijana.

Hawatishi mtu hapo walikuwa wakikagua na kuonyeshana barabara mbalimbali ambazo zitatumika na wajumbe wa mkutano
 
Jeshi la Polisi limeongeza askari na vifaa vyake Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM ambao unatarajiwa kumchagua Rais Magufuli kama Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Awali baraza la vijana wa CHADEMA walisema wangelisaidia jeshi la polisi kuzuia mkutano huo ili kuunga mkono kauli ya Magufuli ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, lakini kamanda wa polisi wa mkoa huo Lazaro Mambosasa akasema hawaitaji msaada na watawasweka ndani wote watakaoingilia mkutano huo

Huyo ndio Mambosasa katika ubora wake. Alikitetea chama na kukilinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom