Kuelekea: Mkutano Mkuu wa CCM Tawi la Uingereza - Jumapili - Julai 26 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea: Mkutano Mkuu wa CCM Tawi la Uingereza - Jumapili - Julai 26

Discussion in 'Matangazo madogo' started by S. S. Phares, Jul 22, 2009.

 1. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu, nawaletea hii makala iliyoandikwa na mwanachama wa CCM Tawi la Uingereza. Hizi ni salamu zake kabla ya mkutano mkuu ujao.

  Matawi ya Nje: Hazina ya CCM

  Uanachama wa CCM katika Ulimwengu-Kijiji

  Tunaishi katika ulimwengu-kijiji. Katika ulimwengu huu wa sasa umbali hauwazuii watu kushirikiana katika masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Mapinduzi katika teknolojia ya habari na mawasiliano, usafiri na usafirishaji yamewawezesha walimwengu kufika kila pembe ya ulimwengu wanayotaka kuifikia. Ni kutokana na dhana hii ya utandawazi CCM ikaona ni vema ianzishe mashina na matawi nje ya nchi ili kuwafikia wanachama wake kwa urahisi. Mashina na matawi haya ya nje ambayo yameanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM ibara 22.1(ii) na 31.1 (d) yamefunguliwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi husika na za Tanzania. Hivyo basi ni mashina na matawi halali.

  Kuanzishwa kwa matawi ya nje kulipokelewa kwa mikono miwili na wanachama wa CCM wakiamini kuwa yatapanda mbegu bora ya ukereketwa na kuhuisha uanachama wa wana-CCM walioko nje ya nchi. Lakini juu ya hayo matawi haya yanawawezesha watanzania waishio ughaibuni na wanaotaka kuwa wanachama kupata kadi kwa urahisi kwani kabla ya utaratibu huu wa kufungua matawi nje ya nchi kila aliyetaka kuwa kujiunga na CCM ilimlazimu kurudi Tanzania ili kupata kadi. Kwa kuwa matawi ya nje pamoja na mashina yake yanaanzishwa na wanachama kwa hiari bila kusukumwa na mtu au chombo chochote cha chama basi ni dhahiri kwamba wanachama katika matawi haya wanayo nia thabiti, ari na moyo wa kuisoma, kuielewa, kuitekeleza na kuitetea siasa ya chama.

  Uimara wa chama chochote cha kisiasa siku zote uko mikononi mwa wanachama wake. Wanachama hai wenye elimu ya juu, ujuzi na vipawa katika fani mbalimbali hukiwezesha chama chao kufikia lengo lake kuu la kushika madaraka ya kuiongoza serikali. CCM inatambua kuwa uimara wake uko katika mikono ya wanachama wake hai kutoka katika umma wa watanzania ambao ndio hazina ya kweli ya uimara na uhai wa chama. Hivyo basi wanachama wa CCM walio nje ya nchi sawa na wenzao walioko Tanzania ni hazina kujivunia ya chama. Nalisema hili na wala lisinukuliwe vibaya au vinginevyo, kwamba pamoja na kuwa wanachama hai wengi, chama chochote cha siasa huitaji wanachama wasomi na wanazuoni katika fani mbalimbali wenye uwezo mkubwa wa kuyachambua mambo.

  Wasomi na wanazuoni hawa hushirikiana na wanachama wengine kuunda sera ambazo hutumika kukinadi chama wakati wa uchaguzi. Sera nzuri huzaa ushindi wa kishindo. CCM inalitambua hili ndio maana ikafungua matawi ya nje ili kuwapata wanachama wengi zaidi na hasa vijana wasomi wenye uzalendo wa hali ya juu ambao wako tayari kulitumikia taifa kwa moyo wote na nguvu zote ili kushinda vita dhidi ya umaskini, magonjwa na ujinga na kuliletea taifa maendeleo-endelevu.

  Baada ya kufunguliwa kwa tawi la CCM la Uingereza na kufuatiwa na matawi mengine katika nchi mbalimbali wamejitokeza baadhi ya watu wakisema uanzishwaji matawi hayo unayafanya matawi ya nje ya CCM yawe sawa na matawi ya vyama vya wapigania uhuru kama PoLISARIO cha Sahara Magharibi au ZANI, ANC, FRELIMO, SWAPO, MPLA na PAC wakati wa harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. Wanadai kwamba haifai kwa CCM kuwa na matawi ya nje huku wakitoa mifano ya mataifa makubwa kama Marekani kuwa vyama vyake vikuu vya siasa vya Republican na Democrat havina nje. Ukweli ni kwamba Republican na Democrat vina matawi yake London na Paris. Tukumbuke kuwa Tanzania ni nchi huru na mfumo wake wa siasa unavipa uhuru vyama vya siasa kuanzisha matawi nje ya nchi ili kuwafikia wanachama kwa urahisi na kuongeza idadi yao. Kwa mantik hiyo hakuna kosa lolote kwa CCM kuazisha mashina na matawi ya nje.

  Matawi ya Nje si Ubaguzi

  Wapo wengine wanaosema matawi ya nje yanaleta ubaguzi miongoni mwa watanzania waishio ughaibuni. Ni ubaguzi gani huo? CCM ni chama cha kitaifa wala si chama cha kidini, kimkoa au kikabila. Ni chama chenye historia ya kusimama kidete kupinga ubaguzi wa aina yeyote. Iweje leo kuanzishwa kwa matawi yake ya nje kutafsiriwe kuwa ni kuleta ubaguzi kwa watanzania waishio nje? Tukumbuke kwamba matawi haya yanafunguliwa na wana-CCM kwa hiari yaokama ambavyo wafanyavyo wana-CCM wa Chunya, Kondoa au Bunda. Lakini kuwa mwanachama wa CCM na kufungua tawi la CCM hakuwazuii wana-CCM kushirikiana wasio wana-CCM katika shughuli za kimaendeleo za uzalishaji mali, kijamii na kisiasa. Kufunguliwa kwa matawi hakuui udugu, urafiki na upendo kati wana-CCM na wasiokuwa wana-CCM. Sasa hii hoja ya ubaguzi inatoka wapi? Bila shaka anayesema hivi ndiye mbaguzi wa kwanza. Kwanini anawabagua wana-CCM kwa sababu tu wamefunga tawi London? Watu wa namna hii ni wa kuogopwa kama ukoma. Wanapanda mbegu chafu ya ubaguzi na inshallah dhambi hii itawatafuna wenyewe wasipoacha kuiendeleza.

  Ndio, tuko ughaibuni, na wote ni watanzania lakini kama ilivyo nyumbani – Tanzania kuwa wote watanzania hakuwazuii watu kuwa na itikadi tofauti za kisiasa na kufanya za chama chake bila kutishwa au kubughudhiwa ili mradi tu hawavunji sheria za nchi. Pale yapotokea masuala yanayohusu watanzania wote, mfano harusi, msiba, sherehe za kitaifa au kukutana na viongozi wetu wa serikali kitaifa, kama ilivyo nyumbani, wote tunajumuika kwa pamoja kama watanzania. Sisi sote ni ndugu. Ni marafiki. Ni majirani. Na pale watanzania wana-CCM wanapokuwa na jambo linalohusu chama chao basi nao wako huru kujumuika pamoja kichama. Ni haki yao ya kidemokrasia. Sasa kwa nini yawepo maswali kuhusu muda wana-CCM kukutana wanaupata wapi. Hili la kukutana au kufanya kazi za chama ni lao wana-CCM wanajua wataupataje muda kuhudhuria vikao vyao vya chama.

  Shutuma Dhidi ya Mabalozi

  Ni bora pia nikalizungumzia hili la shutuma dhidi ya mabalozi wa Tanzania ughaibuni kuwa wanawapendelea wana-CCM tu. Kwamba inapotokea akaja kiongozi wa kitaifa wana-CCM tu ndio wanaalikwa. Hizi shutuma si za kiungwana hata kidogo. Nitoe mfano wa balozi wetu nchini Uingereza Mheshimiwa Mwanaidi Maajar ambaye ameshutumiwa kwa kuwapendelea wana-CCM. Kwanza kabisa inabidi ieleweke wazi kabisa kuwa balozi Maajar haiwakilisha CCM ingawa ni mwanachama wa CCM. Yeye ni mwakilishi wa nchi na si vinginevyo na wala hachanganyi shughuli za CCM na zile za serikali. Pili balozi Maajar si mbaguzi wa kisiasa au kichama. Huwaalika watanzania wote kukutana viongozi wa juu wa serikali wanaokuwa Uingereza kikazi; na mara zote hutoa tangazo la mwaliko huo kwenye tovuti ya ubalozi wetu. Tatu balozi Maajar amejiwekea utaratibu wa kukutana na watanzania wote wenye shida ya kumuona kila mwezi. Na anapokutana nao sijasikia hata mtu mmoja akisema balozi alimuuliza kama ni mwana-CCM.

  Balozi hujishughulisha na suala linaloletwa mezani kwake. Haangalii chama atokacho mtu, dini yake au kabila lake. Juu ya hayo kama balozi Maajar angekuwa mbaguzi wa kisiasa basi asingefanya kila jitihada kuianzisha jumuiya ya watanzania waishio Uingereza ili kuwaunganisha watanzania waishio Uingereza kuwa kitu kimoja. Kama angekuwa mbaguzi wa kisiasa kwa nini asaidie kuanzisha jumuiya ya watanzania ili hali kuna tayari kuna tawi la CCM? Jumuiya hii ya watanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika nchi nyingine. Hongera sana balozi Maajar na viongozi wa jumuiya kwa kazi nzuri.

  Ni kweli kwamba miongoni mwa waanzilishi wa tawi la CCM la Uingereza ni ndugu Sharif Maajar ambaye ni mme wake balozi Maajar lakini hili la mume wake balozi kuwa mwanzilishi wa tawi halina uhusiano wowote na utendaji kazi wa balozi kama mwakilishi wa nchi. Haya ni mambo mawili tofauti kabisa. Kwa nini yanaowanishwa?

  Hitimisho

  Nitumie fursa hii kuwaomba wale wanao tafsiri kuanzishwa kwa matawi ya nje kama ni ubaguzi waache kuendelea kupanda mbegu hii ya uovu miongoni mwa watanzania kwani haijengi umoja, udugu, urafiki, upendo na mshikamano bali inabomoa. Matokeo yake ni kujenga uhasama, chuki na uadui miongoni mwa watanzania waishio nje mambo ambayo si mazuri kwetu, kizazi chetu na nchi yetu.

  Kwa wana-CCM walio nje na hata nyumbani wautumie muda wao wa ziada kuisoma zaidi na kuielewa, kuitekeleza na kuitetea siasa ya chama. Pia tutumie vipawa, elimu na ujuzi tulionao kubuni mbinu na sera mpya za kuijenga nchi yetu ili na kuboresha zaidi na zaidi elimu, huduma ya afya na kila sekta ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kwa kufanya hivi tutakiwezesha Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwa madarakani.

  Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

  Kamaradi Amani Millanga
   
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  Kama si harakati za matapeli na mafisadi kulinda maslahi yao, tawi lenu halina sababu za kuwepo huko UK. Mnachojaribu kufanya ni kuhamishia uswahili wenu wa kisiasa katika nchi za watu ughaibuni ili mjifiche humo na kuendelea kuliibia taifa. Hakuna middle class yeyote asiyekuwa mchumia tumbo anaweza kujipendekeza kwa bei rahisi namna hiyo.

  Waulize watishi kwa nini hawajafungu tawi la Labour au Conservative hapa Dar? Tafadhali tumia jibu lao kujitathmini iwapo kitendo mnachofanya ni sahihi.
   
 3. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Duuh!! kweli sijawahi kuona tawi la Demotratic au Republic nchini Tanzania.halikadhalika sijawahi kuona Labour au conservative wakishinda Dar-Es=salaam au Arusha.

  kukiwa na uchaguzi mkuu wa Marekani basi wamarekani wote bila kujali vyama vyao watakutana ubalozini mwao.

  hakuna nchi yeyote ya Africa yenye matawi ya chama Tawala ulaya au Marekani, sijawahi kusikia Waghana wakifungua matawi ya chama chao tawala zaidi ya NGO za kimajimbo.
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hii ni mojawapo ya sababu zinazofanya mataifa mengine yatuone Watanzania wakati mwingine kama hamnazo. Nitamuelewa Mtanzania mwenzangu nikikutana naye ughaibuni akaniambia yeye ni mpenzi ama hata mkereketwa wa CCM - hi ni sawa na inakubalika. Lakini sitamwelewa hata siku moja Mtanzania mwenye akili timamu akiniambia yeye ni mwananachama wa tawi la CCM nje ya nchi. Huyo atakuwa ana matatizo makubwa na bila shaka anasukumwa zaidi na ujinga, unafiki na ugonjwa wa tamaa.

  Kwanza, simtegemei Balozi makini anayewakilisha taifa la Tanzania kujishughulisha kwa namna yoyote na haya mambo ya kijinga ya kuwagawa Watanzania ugenini kwa misingi ya itikadi. La pili, chama kinachobariki uundwaji wa matawi haya ugenini lina lengo la kuwabagua Watanzania katika matabaka na inafaa usajili wake ufutwe mara moja. Tatu, serikali inayoruhusu mambo haya kufanyika nje ya mipaka yake ni serikali isiyolinda usalama wa raia wake kwa kuhatarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.

  Watanzania naomba hapa tuwe na msimamo moja tu nao ni kuutokomeza huu ujinga unaowatafuna wenzetu hasa huko Uingereza. Mpiga kura siyo lazima awe mwanachama lakini ni vizuri awe na uhuru wa kukipigia kura chama chochote anachoridhika kitalinda na kutetea maslahi ya taifa. Matawi ya CCM nje ya nchi yanatia aibu na kwamba huyu anayejiita Kamaradi Amani Millanga anathubutu kumwaga huu upupu hadharani, inaonyesha Watanzania how we view important issues upside down.
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Naelewa kwa nini mnatilia mashaka kuwepo kwa tawi la CCM Uingereza.

  Ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini lazima muilinganishe Tanzania (Watanzania) na nchi zingine, kana kwamba Tanzania haina uwezo wa kujifanyia mambo yake yenyewe bila kuiga kutoka USa, UK au Ghana?

  Kujifunza kwa wengine ni kuzuri lakini pia tuwe na uelewa na misimamo yetu wenyewe.
   
 6. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa inabidi ieleweke wazi kabisa kuwa balozi Maajar haiwakilisha CCM ingawa ni mwanachama wa CCM.
  --------------------------------------------------------------------------
  Mume na mke Kuwa mwanachama wa CCM na wakati huohuo Mke kuwa balozi wa Tanzania ni conflict of interest...Kivipi? Yeye akiwa kama balozi, ni balozi au mwakilishi wa nchi nzima, na malipo yake ni kutoka walipa kodi wa kitanzania... iweze leo awe balozi na wakati huohuo ni mwanachama wa chama fulani... yeye mama Majaar ni mwanasheria na ukimuuliza hili anajua fika kuwa kama ccm wakimtaka kufanya ya ki-ccm itabidi akubaliane nao na si vinginevyo...

  Unaposema
  -------------------------------------------------------------------
  Yeye ni mwakilishi wa nchi na si vinginevyo na wala hachanganyi shughuli za CCM na zile za serikali.
  -----------------------------------------------
  Ushahidi wa sentesi hiyo uko wapi? una uhakika gani kama siasa za CCM hazichanganyi na mambo ya uwakilishi... Kwa utafiti niliofanya wa haraka haraka ni kwamba 75% ya wale wote wanaopewa mialiko ni wanachama wa CCM...hata ukiangalia mikutano wanayofanya viongozi wa kitaifa hapa UK utagundua kwamba waTanzania wengi wanaohudhulia either wana jezi za ccm wakiwa wamezivaa au wana kadi za ccm ingawaje hili si kosa...
  ---------------------------------------------------------
  Pili balozi Maajar si mbaguzi wa kisiasa au kichama.
  --------------------------------------------------------------
  Umejuaje?  Huwaalika watanzania wote kukutana viongozi wa juu wa serikali wanaokuwa Uingereza kikazi.
  --------------------------------------------------------------
  Mbona mimi bado sijaalikwa na ubalozini nimejiandikisha, email yangu wanayo, anuani yangu wanayo na number zangu za simu wanazo... ni mialiko gani unayozungumzia hapo ambayo watanzania wote huwa hualikwa?
  --------------------------------------------------------------------
  na mara zote hutoa tangazo la mwaliko huo kwenye tovuti ya ubalozi wetu.
  -----------------------------------------------------------------
  Welcome to Tanzania High Commission UK Website Mbona sioni matangazo au tangazo hata moja katika hostoria ya website hiyo... hata ukiangalia link ya Diaspora hakuna tangazo lolote linalosema kwamba kuna mikutano...
  Welcome to Tanzania High Commission UK Website

  Ni hayo tu
   
 7. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Your statement is very powerful. It shows how independently your thoughts are. Ili tuendelee tunahitaji watanzania ambao watakuwa na mawazo ya ubunifu na waweze kuhimizwa kutumia ubunifu wao. Watanzania tunaweza kuwa na mambo mengi ambayo wengine watajifunza kutoka kwetu.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Nonsense!
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Haya matawi yanayo fungulikuwa ughaibuni ni wanachama kujikomba komba kwa mafisadi ambao watawala wa nchi ili nao makaratasi yakiisha wakirudi TZ angalau wafikiriwe post nzuri nzuri kwenye chama na kiserikali.
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndio CCM tunayoota humu kuiondoa madarakani! Sio rahisi hivyo.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Walau tungelikuwa nchi ya kwanza kufanya kitu fulani na hicho kitu kiliingizie Taifa kodi. Pundamilia, waweza kuweka hapa bayana, jinsi Tanzania inavyofaidika na kuwepo kwa tawi la CCM UK?

  Mipingo kweli tuna matatizo sana. Ni au hatufikiri kabisaa..... na tukifikiri na kuanza kufanya mambo, ni Pwagu na Pwaguzi (Ntakukumba mwenzio..) Mie nasema siku zote heri walau tungelianzisha vibali na kodi kwa malaya na Posta zijengwe cafe za kuvutia bangi. Kodi ingelikusanywa na akina mama wasingelizalia kwenye sakafu.

  Cha kushukuru Mungu ni kuwa kwa sasa mambo yanafahamika haraka sana na si kama wakati wa JKN. Siku ikifika mafisadi na umma wao wataumbuka na umoja/vyama vya siasa ugaibuni, vitakufa natural death.
   
 12. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nahisi ndugu yangu una ushabiki ule wa kutetea na kutaka kulinda maslahi ya Baba, Mama, Kaka, Dada, Shangazi, Mjomba, Binamu etc ambao wako ndani ya uongozi wa juu wa CCM ama Serikali. Vinginevyo sioni sababu iliyokufanya hata uwaze jambo kama hili. It is a shame!

  Eti tuwe na msimamo wetu wenyewe kwa kufungua tawi la CCM Ulaya! Mama mia!
   
 13. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Huyu atakuwa bwana John Lusingu tuuuu wa reading

  kama kawaida yao...udini watakataaa...WAISLAM HAKUNA! wakiambiwa wakabila watapinga lakini humo wamo WACHAGGA na WAJALUO ndio wamejazana...hii yote kutaka kumchafua Balozi Mwanaidi a mbaye alitakiwa awe neutral lakini wapi! Mumewe ndiye kinara wa kufungua haya matawi as if hana shughuli nyingine mjini

  badala ya kuunganisha watu Balozi anakuwa mstari wa mbele kuwagawa waTanzania...mbona kwenye mikutano ya CUF haji?

  I wonder kama kesharudisha ile kadi ya CHADEMA maana tunaambiwa kuwa balozi ni mmoja ya waanzilishi wa CHADEMA


  Chama Cha Mapinduzi - Tawi la London - Uingereza
   
 14. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Wakati watu wanaenda ili wawe exposed wengine wakienda nje ndio wanazidi kudumaa kiakili
   
 15. S

  Siao Member

  #15
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikionaga hizi habari za ccm huku uingereza huwa najisikia kichefuchefu kabisa.

  huwa ninasemaga wale premature premature premature..wametokea tena.

  Mimi nipo hapa jirani kwenu - ujerumani, upumbavu gani huu tena jamani!

  sawa, ccm imewafikisha hapo ninyi wachache kwa gharama za wengi..., policy yenu hiyo ya kiccm inawasaidia kunywa damu za watanzania maskini... ndivyo ccm wanavyofanya na ninyi igeni hivyo...!

  Lakini kama Rome ilivyoanguka, na Unazi ukaanguka, Alexander the Great akaanguka, CCM imeshaanguka...


  Aibu na iwe kwenu... mnapoitetea ccm - walionacho nakutusahau sisi tulio wengi maskini.

  Na kweli Mjinga hana aibu...!
   
 16. S

  Siao Member

  #16
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ndio ulimbukeni uliovuka mipaka...!


  Sina haja ya kujua utashi wa balozi na na timu yake.... kama hali ndio hii it is clear, tuna mabalozi wengu tu basi ambao ni magazeti kwenye hizi mnazoziita balozi...!

  kwa herini.

  ama kweli kusoma ni kitu kimoja na kuelimika ni kitu mbo lingine...!

  Hatukufundishwa wote jamani kuwa "the best thing in the world is not so much what you have done for your self, but for others."? Sasa hawa wanapojinufaisha wenyewe kwa kuunda kikundi cha kiitikadi ya kichama ili kuwanufaisha wenyewe na kuwatenga wale wenye itikadi tofauti, huu sio ulimbukeni?

  Nyerere angekuwa hai angewachapa bakora!

  Kwamba mlienda darasani wakati huo ni kweli, lakini kuwa kila kitu pia mlikremu pia ni kweli!

  shame upon us all on this!
   
 17. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ah, kumbe yale yale! Nilijua kuna mwenye 'maslahi' ambaye ndiye engineer wa wazo hili hasi la kufungua matawi ya CCM kwenye nchi za watu! Waliojaa UK hasa Reading mbona wengi ni 'wakimbizi wa kiuchumi' toka Tanzania na wala hawatarajii kurudi kuja kupiga kura? It is just a waste of energy.
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hivi habari za London na CCM zina umuhimu gani wa kuja hapa jamvini ? Tuna faida kweli na habari ? Au hawana mtandao wa kuelezana basi inabidi waje hapa ? Au ndiyo wako kazini kuonyesha akina Malecela kwamba wako hai na mambo yao yaandaliwe ?
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamaa mjinga sana huyu tokea akiwa Mwenge Secondary miaka ya 90's! Hawezi kufikiri ni Mzee wa kupenda slope sishangai anachokifanya sasa ndivyo alivyo!
   
 20. Bob1

  Bob1 Member

  #20
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza tujue nini dhamira ya ndugu zetu hawa kufungua matawi.Niwazi kuwa ni njia mojawapo ya kutafuta kujulikana na kujijengea base ili kunasa nafasi katika chama,kuna baadhi yao sio wakazi halani and they want protection and may other factors.Na tanzania watawala kutoka CCM it good news manake ni njia mojawapo ya ku hold waliokua nje ya nchi ili wasi hoji uhalali wa shughuli zao.
  Jambo linalosikitisha kila mambo mengi yanayotoke UK (london) ambayo ni ya kitaifa,hilo genge lilioshika hayo matawi husaidia kufanya jambo (shuhuli) hilo iwe na sura ya ki-CCM na kinachosikitisha kabisa ni wazi fedha za walia kodi Tanzania naamini zina tumika ku fund shuhuliza za matawi haya.
  Nini kifanyike ndio iwe Debate..
   
Loading...