Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Ifikapo tarehe 9 mwezi huu tunasherehekea miaka 51 ya Tanzania kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni. Katika kusherehekea huku si katika kufurahia tu na kuangalia gwaride na baadae kujirusha, bali jambo muhimu la kufanya ni kutathmini ni kipi tumekifanya na wapi tunaelekea na tutaelekea huko kwa njia zipi. Tathmini hiyo ndiyo itamfanya kila mmoja wetu kuchukua maamuzi juu ya mustakbali wa taifa letu.