Kuelekea mechi ya 'TPL' Stand Utd dhidi ya Simba SC, Mnataka Mfungwe Mabao Mangapi?

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,263
Kuelekea mchezo wa Tanzania Premier League TPL, kati ya Stand United dhidi ya Simba SC Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, Stand United chagueni wenyewe mnataka mfungwe mabao mangapi?

•••Kulipewa Mwana..Kulitaka Mwana SSC

Kwa jinsi hali ilivyo hivi sasa hapa nchini Tanzania katika duru hili la mwisho la ligi kuu, kwa timu zote zinazopambana na Simba SC, ni dhahiri hakuna hata timu itakayofua dafu kwa kuchukua alama kutoka kwa Simba SC, isipokuwa watapigania kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa.

•••Show ya Hatari Pamoja na Burudani SSC

Yanga SC walichagua upasuaji mmoja, lakini hizi timu zingine za Azam FC, Lyon na Lipuli FC naona upasuaji wa mara tatu tatu umetamalaki kwao.

•••Soka la Kiwango kilichothibitishwa na CAF

Kukutana na kikosi hiki cha Mnyama Simba SC ni hatari kwa usalama wa timu pinzani..Ni kikosi cha mafundi kweli kweli huku uwezo wa kila mchezaji mmoja mmoja ukichukua nafasi kunako kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.

Kocha wa Stand Utd Athuman Bilal ameongea mengi kuelekea mchezo utakaovurumisha uwanja wa Kambarage Stadium, siku ya Jumapili Machi 3, 2019 lakini tunamwambia ajiandae Kisaikolojia, kwani tayari barua ya kustaafishwa imeandaliwa...This Is Simba SC. NguvuMoja.

IMG_20190302_130749_476.jpeg
IMG_20190302_125340_467.jpeg
 
Hivi unakumbuka yale maneno aliyoyasema baada ya mechi ya watani wa Jadi...Utagundua alichokisema ni kweli

Simba SC inaogopwa sana....!
Leo kocha wa Yanga Zahera amesema timu plan yake akicheza na timu zingine sio sawa na akicheza na Simba."Kwa sababu kila mtu anajua Simba walivyo.Inabidi ucheze kwa kujihami".
 
Mtani soma Mwanaspoti sio maneno yangu ni ya Zahera. Ukweli inabidi usemwe. Unafikiri Zahera ana paki basi anapenda??
Anajua ukweli.
 
Kinachofurahisha chura wana mechi yao leo lakini hawaizungumzii. Wao wapo obsessed na Simba.
Hata kocha wao ana tabia hiyo hiyo.
Huwezi kukuta Patrick Aussems akizungumzia Yanga siku ambayo hachezi nayo.
Kocha aliyetimuliwa Azam Hans nae aliingia mkumbo huo huo.Nae akagoma kuingiza timu kwenye vyumba vya kubadilisha.Kilichomkuta ni historia.
 
Kinachofurahisha chura wana mechi yao leo lakini hawaizungumzii. Wao wapo obsessed na Simba.
Hata kocha wao ana tabia hiyo hiyo.
Huwezi kukuta Patrick Aussems akizungumzia Yanga siku ambayo hachezi nayo.
Kocha aliyetimuliwa Azam Hans nae aliingia mkumbo huo huo.Nae akagoma kuingiza timu kwenye vyumba vya kubadilisha.Kilichomkuta ni historia.
Ukiona wanakujadili ujue wanakukubali...SimbaNguvuMoja
 
Back
Top Bottom