Kuelekea mechi ya 'TPL' Simba SC dhidi ya Mbao FC, Moto wa Mnyama Kuendelea Kuwaka

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Moto wa Mnyama Mkali Simba SC, Mabingwa wa Nchi kuendelea Kuwaka tena kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania TPL, dhidi ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza.

Simba SC pamoja na kukusanya mapato ya alama tatu tatu kutoka kila timu hasa katika mzunguko huu wa mwisho, imemaliza maandalizi yake ya mwisho hivyo kujiweka tayari kwa mchezo huo siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri Stadium mkoani Morogoro.

•••Kulipewa Mwana...Kulitaka Mwana

Kikosi cha Simba SC, Mnyama Mkali chini ya Kocha Patrick Aussems kipo tayari kwa kipute hicho na kimeaahidi kufanya vema na kuweza kuibuka na ushindi hivyo kukusanya alama tatu sambamba na burudani ya aina yake.

Kikosi cha Simba SC ambacho kinaupiga mpira mwingi sana Tanzania kwa mechi za ligi kuu na za Kimataifa, kitaingia kwa tahadhari kwani Mbao FC walibahatisha kuchafua ubao mzunguko wa kwanza hivyo kwa maandalizi yaliyofanywa klabu ya Simba SC ni dhahir Mbao zitachanika.
IMG_20190330_084703_191.jpeg
IMG_20190330_065032.jpeg
 
Back
Top Bottom